PATANISHO: Jamaa kazi ni kunitesa na hadi paka hajawahi peleka kwetu

Japhet kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Sarah.

PATANISHO: Nasikitika Nilimuibia Tajiri Wangu Elfu Tisa

 

Mke wangu ametoweka miezi minne sasa na nikimpigia anadai atakuja lakini amekuwa muongo sana.

Mke wangu alipata ujumbe kwa simu yangu lakini haukuwa wangu lakini pia nilipata ujumbe kwa simu yake ya mapenzi huku wakizungumza na jamaa fulani wapatane na hapo tukakosana.

Ujumbe aliopata ulikuwa umetumwa na jamaa fulani mfanyikazi mwenzangu akiungumza na mpenziwe.

Kumuuliza akadai kuwa aliponipata sikumwambia chochote na kwa hivyo kila mmoja ajishughulishe. Alidai Japhet ambaye amekuwa kwa ndoa kwa miaka saba.

PATANISHO: Mke wangu alikuwa anakatiwa na caretaker

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Alipopigiwa Sarah alikiri Japhet alikuwa na shida ya kukwepa majukumu ya nyumba.

“Hataki kusomesha mtoto, ukimwambia mambo ya kujenga nyumbani hataki, tumeoana miaka saba na huyu mwanaume hajui kwetu lakini anataka niishi Nairobi bila kushughulika na mambo ya nyumbani.” Alieleza Sarah.

Hata haikuwa mambo ya mpango wa kando, nilitoka nyumbani na pindi tu nilipofika nyumbani majirani walinipigia kunieleza alikuwa na vituko chungu nzima huko Nairobi.” Aliongeza.

Paka Mwitu Ashambulia Na kuumiza Watu Wawili Rongo

Watu wawili wanauguza majeraha katika hospitali ya gatuzi dogo la Rongo baada ya kushambuliwa na paka wa mwituni wakiwa njiani.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, paka huyo aliwashambulia wawili hao David Ododa na Joyce Atieno Otieno baada ya kutokea kwenye shamba la miwa lililokuwa karibu na barabara hiyo ambayo walikuwa wakipitia.

Mmoja wao Joyce Atieno Otieno alishambuliwa na paka huyo ambaye alikwama kwenye mguu wake na alipopiga mayowe David Ododa pia alishambuliwa na paka huyo alipokuwa akijaribu kumnusuru Bi Joyce kutoka kwa mnyama huyo.

Wawili hao wanaendelea kupata matibabu huku polisi wakitaka shirika la huduma la wanyama pori KWS kumkamata paka huyo ambaye alitorokea kwenye shamba moja la miwa.