Kamanda wa polisi aliyemshutumu Sonko kwa kumshambulia aletwa Nairobi kuwa mkuu wa Polisi

Rashid Yakub amehamishwa hadi  Nairobu kuwa mkuu wa polisi kutoka kwa Philip Ndolo.

Mabadiliko hayo yameangazwa siku ya jumamosi  na Ndolo ataelekea Nyeri kuwa naibu kamanda wa chuo cha mafunzo ya polisi Kiganjo .

Yakub alikuwa kamanda wa polisi wa pwani na  disemba mwaka jana alimshtumu gavana wa Nairobi Mike Sonko kwa kumshambulia wakati Sonko alipokuwa akikamatwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Voi  kuhusiana na kesi ya utoaji  zabuni  ya shilingi  Milioni 357 .

Baadaye Yakub aliamua kuondoa kesi hiyo dhidi ya Sonko

 

 

Ajali inayohusisha magari manane yasabisha msongamano Nairobi

Magari manane Alhamisi asubuhi yalihusishwa katika ajali ya barabara ya Thika katika eneo la Kituo cha Polisi cha Muthaiga.

Ajali hiyo mwanzo ilisababishwa na mabasi mawili ya kampuni ya Virginia Coach na basi la Mwiki Sacco kabla ya magari mengine kuhusishwa.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Nairobi Philip Ndolo amesema kwamba basi la kampuni ya Virgnia iliteleza na kugonga  vichuma kando kando mwa barabara telezi kutokana na mvua kubwa unaonyesha.

“Kulikuwa kunayesha na mojawapo a mabasi likateleza barabarani…kisha basi la Mwiki Sacco likagonga hilo basi,” Ndolo amesema.

Ndolo alisema kutokana na mvua kubwa,  hali ya barabara si shwari na madereva wameshauriwa kuendesha kwa utaratibu

Madereva wanaoelekea maeneo ya Ngara wameshauriwa kutafuta njia mbadala ili kuepuka eneo hilo la ajali.

Ndolo anasema kwamba hakuna majeruhi katika ajali hiyo.

Kipchoge Awasili Kimyakimya, Fahamishwa Mbona Hatachinja Ng’ombe Kusherehekea