Ibada ya wafu ya muigizaji Pretty Mutave kufanyika hapo kesho huku mazishi yakiwa ni ya Jumamosi

Muigizaji Pretty Mutave ambaye alifahamika sana kupitia kwa kipindi cha Maza, Aziza, Moyo na miongoni mwa vipindi vingine atazikwa nyumbani kwao Kibwezi kaunti ya Makueni mnamo Jumamosi wiki hii.

Duru za habari ziliarufu kuwa Mutave aliaga dunia alipokuwa anapelekwa hospitali huku akiwa mgonjwa tangu Machi mwaka huu.

Mwanahabari Rashid Abdalla aomboleza kifo cha muigizaji Pretty Mutave

Pretty-2-324x235

Ibada ya wafu ya mwendazake Mutave itafanyika hapo kesho katika eneo la Swahilipot kaunti ya Mombasa ambapo watakaohudhuria watavalia mavazi ya rangi nyeupe na nyekundu, ibada hiyo itaanza saa kumi jioni hadi saa kumi na mbili jioni.

Ujumbe kutoka kwa kamati ambayo inatayarisha mazishi yake ilisoma hivi;

“Mwili wa mwendazake utasafirishwa Ijumaa mbele ya mazishi ya Jumamosi, kwa mpangilio wa kusafiri kila mmoja wetu anapaswa kujiandaa kwa mapema, tukingoja uamuzi wa jamaa zake ili tuweze kuwajuza mambo na usafiri.”

Pretty-Mutave66-696x418

Siwezi amini haya,’Muigizaji Luwi amuomboleza Pretty Mtave

Mwendazake aliaga dunia mnamo Septemba 15, huku mashabiki, marafiki wakituma risala za rambirambi.

Mungu na azidi kuilaza roho yake mahali pema peponi.

Siwezi amini haya,’Muigizaji Luwi amuomboleza Pretty Mtave

Kumpoteza umpendaye au rafiki yako ni jambo ngumu sana na la huzuni huku familia ya kipindi  cha Maza, Moyo na Aziza wakimuomboleza mmoja wao Pretty Mutave ambaye aliaga dunia mnamo Septemba 15.

Waigizaji wenzake,marafiki na wakenya walituma risala za rambi rambi zao kwa familia huku wengi wakimsifu.

Muigizaji mwenzake wa kipindi cha Maza Luwi Capello, kutokana na ujumbe wake wawili hao walikuwa wanataniana na hata kuwa marafiki wa karibu sana.

0D375641-C756-483E-B37F-E5281EB3E41D

Kupitia kwenye ujumbe huo Luwi alisema kuwa hajaamini ya kuwa Pretty hayupo tena.

“Nilikuwa nakuita Pretty Pretty, bado sijaweza kuamini haya, wacha Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi kwa kweli maisha ni mafupi.” Luwi aliandika.

Mungu azidi kuilaza Roho yake mahali pema peponi.

Mwanahabari Rashid Abdalla aomboleza kifo cha muigizaji Pretty Mutave

Mwanahabari wa runinga ya Citizen Rashid Abdalla anaomboleza kifo cha muigizaji Pretty Mutave, kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Rashid alimsifu muigizaji huyo kwa kipaji cha uigizaji.

Huku akiposti picha yake Rashid aliandika ujumbe ufuatao,

#sisemikitu Japo kazi ya Mungu haina makosa lakini msiba hauna mazoea. @prettymutavekipaji chako kikawe nuru kwa malaika. Mola ailaze roho yako pema peponi Inshallah. Heshima na kipaji chako vitadumu milele”. Aliandika Rashid.

Kifo cha Muigizajii huyo hakijabainika, alikuwa kwenye mitandao ya kijamii huku akiacha kuonekana kwenye mitandao hiyo mwishoni mwa mwezi jana.

Mutave alifahamika sana kupitia kwa kipindi cha Maza kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic East, na pia kwenye kipindi cha Aziza ambapo Rashid Abdalla na mkewe Lulu Hassan ndio wazalishaji wa vipindi hivyo.

YQlk9kpTURBXy9iZDAxNWM5NmY2ZTcxMTI4YjY5YzAwYzA3OGY4MDllNy5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.