Viongozi wa Ukambani waapa kupinga mswada wa ugavi wa fedha katika bunge la Seneti

Maseneta kutoka Ukambani sasa wameapa kupinga vikali mswada wa ugavi wa fedha utakaorudishwa ndani ya bunge la seneti wiki hili kwa mara ya saba mfululizo.

Wakiongozwa na seneta wa Makueni Mutula Kilonzo ,viongozi hao sasa wamekashifu hatua ya vyama vya kisiasa nchini kuendelea kuwashinikiza maseneta kuunga mkono mswada ambao unanuiya kuhujumu mfumo wa ugatuzi nchini.

Jumanne maseneta wanatarajiwa kurejelea vikao vyao vya kawaida na kujadili mswada huo katika hatua ambayo imenasemekana kuewa huenda ikaashiria msimamo wa kisiasa nchini.

Raila Odinga kuwarai Maseneta kuunga mkono mfumo mpya wa ugavi wa fedha kwa kaunti

Maseneta hao ambao wametoka madeneo tofauti ya Mashhariki mwa Kenya,wamemkashifu kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kwa kujaribu kuwashurutisha kuunga mkono mswada huo.

Kwa kauli moja sasa wamesema kuwa hawatashinikizwa kufanya uamuzi wao kivyovyote vile.

 

 

Maseneta sasa watalazimika kujadili mapendekezo yaliyoewasilishswa na seneta wa Nairobi Johnson Sakaja ambayo yanapania kutafuta suluhisho kwa mgogoro unaoenfdelea wa ugavi wa fedha .

 

Lampard ashutumu uongozi wa Premier league kwa kuanzisha msimu ujao mapema

Mkufunzi wa Chelsea ameshutumu vikali hatua ya usimamizi wa ligi kuu ya Uingereza wa kuanzisha msimu mpya wa mwaka 2020/2021 septemba 12 akisema asilimia kubwa ya wachezaji hawatakuwa na muda wa kupumzika baada ya kushiriki michezo ya mabingwa bara Ulaya na Uropa.

Chelsea watakuwa wakicheza dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wiki hii kwa awamu ya mkondo wa pili katika mechi za Champions league. Munich wanaingia katika mchezo huo wakiwa na  matumaini makubwa ya kufuzu kwa awamu ya robo fainali baada ya kushindi mkondo wa kwanza kwa magoli 3-0 ugani Stamford Bridge.

Premier League start date too early for Chelsea, Lampard says

Drogba awasilisha nyaraka zake za kuwania urais wa shirikisho la soka Ivory Coast

Lampard amesema kuwa kutokana na michezo hiyo inayoendelea, huenda asilimia kubwa ya wachezaji hawatakuwa na muda wa kupumzika kutokana na ratiba mpya ya EPL msimu mpya.

 

Wachezaji Cesar Azpilicueta, Christian Pulisic na Pedro watakaso kushiriki mtanange huo baada ya kujeruhiwa wakati wa fainali ya kombe la FA Jumamosi dhidi Arsenal mechi waliyopoteza magoli 2-1 .

 

Obare aachiliwa kwa dhamana ya laki moja

Mwanablogu  mzushi wa humu nchini Edgar Obare ameachiliwa kwa dhamana  ya shilingi laki moja na mahakama ya Kiambu. Obare ana chaguo la kulipia bodi ya thamani ya shilingi laki tatu baada ya kushtakiwa kwa madai ya kufichua taarifa za siri za mwanamke Natalie Wanjiru Githinji  almaarufu  Natalie Tewa.

Obare alifikishwa katika mahakama hiyo ya Kiambu mapema Jumatatu na kukana mashtaka dhidi yake ambayo yalikuwa yamewasilishwa na mlalamishi.

‘Maisha ya watu yanawahusu nini?’ Natalie Tewa ajibu madai ya kununuliwa gari na Joho

Obare aliwakilishwa  na mawakili   Titus Munene Kinyua na Ojijo Kepher.

Edgar Obare afikishwa katika mahakama ya Kiambu

Kesi hiyo sasa inatarajiwa kutajwa mnamo Agosti 21 huku ikirejelewa Novemba 2 mwaka huu.

Ifahamike kuwa Obare alitiwa mbaroni Ijumaa akiwa  katika kaunti ya Kisumu na makachero kutoka DCI ili kujibu mashtaka yaliyokuwa yanamkumba.

 

Watu 544 wapatikana na virusi vya corona huku 13 wakiaga dunia – Aman

Watu 544 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli za watu 2,653 kupimwa chini ya saa 24.

Idadi hiyo sasa inafanya taifa kuwa na watu  22, 597 walio na virusi hivyo kufikia sasa.

Aidha wagonjwa wengine 13 wametangazwa kufariki na kufikisha watu 382 waliofariki kufikia sasa kutokana na ugonjwa huo

Katibu wa utawala wa wizara ya Afya  Rashid Aman amesema kuwa watu 263 waliokuwa wamelazwa katika hospitali tofauti nchini wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha watu  8,740 waliopona.

Image

Aman pia amethibitisha kuwa wahudumu  wanane  wa afya hadi kufikia sasa wamefariki kutokana na virusi hivyo huku  wa hivi punde kupoteza maisha yake akiwa Mariam  Awuor kutoka kaunti ya Kisii.

Kati ya visa hivyo vipya Nairobi imeandikisha visa 412 , Kiambu 27, Machakos 17, Kajiado 17, Garissa 16, Uasin Gishu 14, Mombasa 9, Nakuru 8, Nyeri 5, Narok 5, Makueni 4 Laikipia 2, Muranga, Kilifi, Busia, Embu, Bungoma, kisii, Kwale na  Meru  zote zikiwa zimeandikisha kisa kimoja.

Wakati huo huo Aman akana madai kuwa kuna baadhi ya wahudumu wa afya ambao wamekosa kulipwa mishahara yao akisema serikali kuu pamoja na zile za kaunti  nchini zimekuwa zikishirikiana ili kufanikisha malipo ya wahudumu hao  .

Image

Serikali ya Homa Bay yasubiri ripoti ya kubaini kilichosababisha kifo cha Mariam Awuor

  Ameongeza kuwa serikali imeweka mikakati mwafaka ya kuajiri wahudumu zaidi ili kusaidiana na wenzao wanaokabiliana na janga hilo.

Amesisitiza umuhimu wa wakenya kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kama njia ya kupunguza msambao wa corona.

Akisoma takwimu hizo mpya za maambukizi ya corona, Aman ametuma risala za rambirambi kwa familia ya Mariam Awuor ambaye alitangazwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

 

 

Nitakushughulikia vilivyo! Wetangula na wenzake wamuonya Eseli Simiyu

Seneta wa Bungoma Moses Wetangula amewaongoza wenzake ndani ya chama cha Ford  Kenya kumuonya  mbunge wa Tongaren Eseli Simiyu na mwenzake wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi dhidi ya kuendesha shughuli za chama hicho kwa niaba ya viongozi.

Katibu mtendaji wa kitaifa wa chama hicho Chris Mandu amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya viongozi wao hawali ,akihoji kuwa mawakili wa Ford Kenya wamepewa ruhusa ya kuwasilisha kesi dhidi yao mahakamani iwapo hawatakoma kuingilia maswala ya chama hicho.

Wetangula’s Ford Kenya cautions Eseli, Wamunyinyi against purporting to represent party

Raila Odinga kuwarai Maseneta kuunga mkono mfumo mpya wa ugavi wa fedha kwa kaunti

 Mandu amesema kuwa licha ya mahakama kutoa uamuzi wa kusimamisha kung’atuliwa mamlakani kwa Wetangula -Eseli na Wamunyinyi wamekuwa wakieneza propaganda kuwa wao ndio viongozi  wapya wa chama hicho.

Mahakama kuu Juni 25 mwaka huu ilitoa uamuzi wa kupinga kung’atuliwa kwa Wetangula kama Kiongozi wa  chama cha Ford Kenya.

Wakati uo huo Mandu amedhibitisha kuwa chama hicho kimefanya uchaguzi wa katika maeneo mbali mbali nchini na unasubiri kuhidhinishwa hivi karibuni na bodi kuu ya chama hicho.

 

Raila Odinga kuwarai Maseneta kuunga mkono mfumo mpya wa ugavi wa fedha kwa kaunti

Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga sasa anapania kufanya kikao na Maseneta ili kuwarai kuunga mkono mfumo mpya wa ugavi wa pesa kwa kaunti 47 unaopendekezwa na hazina ya kitaifa.

Odinga, Peter Kenneth na David Murathe wamefanya kikao cha faragha katika boma la katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini  COTU Francis Atwoli kama njia ya kutafuta suluhisho kwa mgawanyiko unaoshuhudiwa ndani ya seneti kwa sasa.

Mswada wa kujadili ugavi wa fedha katika bunge la seneti umeahirishwa mara sita mfululuzo sasa baada ya maseneta kuupinga kwa kauli moja kuwa huenda baadhi ya majimbo nchini yakapoteza pesa nyingi, hivyo kulemaza shughuli za maendeleo.

Comer President candidate Peter Kenneth with ODM leader Raila Odinga on Sunday.

Idara ya polisi yazindua mfumo wa kidijitali wa kurekodi visa

Akizungumza na  Gazeti la The Star,  Kenneth amesema kuwa wamefanya kikao hicho ili kubaini namna ya kusitisha mgawanyiko unaoshuhudiwa kwa sasa ndani ya seneti.

Ameongezea kuwa Raila ameahidi kuwashinikiza maseneta kutoka mrengo wake ili kuunga mkono mswada huo, jambo ambalo amesema litafanikishwa kwa ushirikiano na kiongozi wa wachache James Orengo.

Ameongezea kuwa mazungumzo yao pia yamegusia maswala kuhusiana na handshake baina Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

ODM and Jubilee leaders at Cotu chairman Francis Atwoli's home in Kajiado on Sunday.

Kati ya maseneta 25 walioupinga mswada huo, 18 walikuwa wa mrengo wa Nasa unaongozwa na Raila Odinga  huku wengine wakitokea katika chama cha Jubilee.

Wiki jana, Kiongozi wa wengi  katika seneta  Irungu Kang’ata alisema kuwa atahakikisha mswada huo unapasishwa wakati bunge hilo litakaporejelea vikao vyake  siku ya Jumanne.

 

 

Idara ya polisi yazindua mfumo wa kidijitali wa kurekodi visa

Idara ya polisi nchini sasa imezindua mfumo mpya kidijitali wa kurekodi  visa almaarufu OB ambao utafanikisha utendekazi wao nchini kama njia ya kuboresha huduma kwa wote.

Mfumo huo sasa utawafanya wakenya kupokea nakala ya ripoti kupitia barua pepe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i amesema maafisa wa polisi watakuwa na miezi 18 pekee kufahamu namna mitambo hiyo inavyofanyakazi.

Matiang’i amesema kuwa serikali inapania kuboresha huduma za idara ya polisi nchini kwa kutupilia mbali mfumo wa analogi ambao ulikuwa unachukuwa muda mwingi.

Fred Matiangi

Amesema visa vya  kila mara  vya kupotea kwa faili havitakuwepo kwani mfumo huo unalenga kuziba mianya hiyo.

Matiang’i pia amehoji kuwa watakaokuwa wakiwasilisha malalamishi yao kupitia mfumo huo watakuwa wakilipa na kupewa risiti papo hapo.

Edgar Obare afikishwa katika mahakama ya Kiambu

Idara ya polisi imekuwa ya hivi karibuni kuzindua mfumo huo  baada ya Jaji mkuu David Maraga kuongoza wafanyakazi katika idara ya mahakama nchini kuzindua mfumo ambao utawawezesha wakenya kuwasilisha kesi zao mitandaoni pasi na kufika katika mahakama mbalimbali nchini.

Kwa upande wake inspekta Mkuu wa polisi Hillary Mutyambayi amesema mfumo huo utafunga mianya yoyote ya kujaribu kuhitilafiana na taarifa zitakozokuwa zinawasilishwa katika vituo tofauti vya polisi.

 

Serikali ya Homa Bay yasubiri ripoti ya kubaini kilichosababisha kifo cha Mariam Awuor

Serikali ya Homa Bay sasa imesema itasubiri mwili wa mhudumu wa afya aliyefariki Mariam Awuor kufanyiwa upasuaji kubaini iwapo mhudumu huyo alifariki kutokana na  virusi vya corona.

Waziri wa afya kaunti hiyo Richard Muga amewataka manesi pamoja na wahudumu wengine wa afya kuendelea kuchapa kazi pasi na uoga wowote.

Muuguzi mkenya aaga dunia siku chache baada ya kupona covid-19

Mariam Awuor anasemekana kufariki Jumapili asubuhi kutokana na matatizo mengine ya kiafya licha ya kupona kutokana na virusi vya corona.

Majuma mawili yaliyopita, Awuor alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU baada ya kudaiwa kuwa alikuwa ameambukizwa virusi hivyo.

Nurse Marian Awuor who died at Kisii County Referral Hospital when she was recovering from covid-19

Fahamu watu maarufu walioangamizwa na corona kufikia sasa

Mwendazake  alikuwa na umri wa miaka 32 na  alikuwa anafanya kazi katika kituo cha afya cha Rachuonyo Kusini eneo la Oyugis na alikuwa mimba ya miezi mitatu.

Hii leo wauguzi wenzake wametaka serikali ya kuanti hiyo kuelezea ni nini kilichopelekea kifo chake.

Chini ya muungano wao wa wahudumu wa afya KNUN, katibu mkuu wa muungano huo George Bola amesema kuwa Awuor alijifungua vyema licha ya kufanyiwa upasuaji.

Amesema taarifa za kifo cha mwenzao ni za kushtusha kwani walikuwa wanatarajia kuwa ataruhusiwa kuondoka hospitalini hii leo.

 

Drogba awasilisha nyaraka zake za kuwania urais wa shirikisho la soka Ivory Coast

Maelfu ya watu wajikusanya nje ya afisi za Soka katika taifa Ivory Coast pale mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Didier Drogba alipokuwa anawasilisha karatasi zake za kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka la taifa hilo la Afrika ya Magharibi

Drogba wa miaka 42 ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika ni miongoni mwa wawaniaji wanne ambao wanataka kuwa vinara wa shirikisho la soka la  taifa hilo.

Drogba submits candidacy to become Ivory Coast FA president

 

Kando na kupata uungwaji mkono wa vilabu vitatu kati ya vilabu 14 vinavyoshiriki  ligi kuu ya taifa hilo, ni sharti mchezaji huyo wa zamani apate uungwaji mkono wa vilabu viwili vinavyoshiriki katika ligi ya daraja ya pili na pia kuungwa mkono na watu  watano kutoka vitengo tofauti vikiwemo Makocha, Madaktari, uongozi wa sasa wa shirikisho hilo na wachezaji wenza wa zamani wa taifa hilo pamoja na waamuzi.

Drogba aliwasilisha karatasi zake mida ya saa  kumi na moja jioni na kupokelewa na mashabiki wake waliokuwa wanamngoja nje ya afisi kuu za shirikisho la michezo katika taifa hilo.

 

Edgar Obare afikishwa katika mahakama ya Kiambu

Mwanablogu  mzushi  Edgar Obare Jumatatu amefikishwa katika mahakama za Kiambu baada ya kutiwa mbaroni wiki jana.

Obare anakabiliana na makosa ya kuweka wazi data za kibinafsi za  mwanamke Natalie Wanjiru anayefahamika kama Natalie Tewa.

‘Maisha ya watu yanawahusu nini?’ Natalie Tewa ajibu madai ya kununuliwa gari na Joho

Akiwa mbele ya mahakama hiyo, Obare amekana mashtaka dhidi yake huku akisubiri kubaini hatima yake wakati ambapo mahakama hiyo itakaporejelea vikao vyake saa  nane mchana hii leo.

Obare alitiwa mbaroni Ijumaa akiwa Kisumu na maafisa kutoka DCI ili kujibu  mashtaka dhidi yake.

Edgar Obare arraigned at Kiambu Law Courts, charged with disclosing personal data

Kenya yabadili hatua yake na kuruhusu ndege kutoka Uingereza na Amerika kutua nchini

 Yanajiri haya baada ya kushtumiwa kwa kuandika ujumbe kwenye  mtandao wake wa Instagram kuwa mwanamke huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanasafiri Dubai kumtembelea kiongozi wa ODM Raila odinga ambaye alikuwa amelazwa hospitalini.

Miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni mbunge Junet Muhammed na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.

Obare alilazimika kukesha katika kituo cha polisi cha Gigiri Wikendi kabla ya kufikishwa mahakamani hii leo.