Hali ya umaskini yasababishia Ashley na Joyce kujitosa katika ukahaba

Katika kipindi cha Bustani La Massawe kitengo cha Ilikuaje, wageni katika studio walikuwa wawili Ashley na Joyce ambao wamekuwa katika uraibu wa ukahaba kwa muda mrefu. Wawili hawa wana sababu zao zilizowafanya wajitose katika kazi hii.

Soma mengine hapa:

PATANISHO: Atafute bibi mwingine kwani siwezi rudiana naye!

Ashley, 22, baada ya kumpoteza mama akiwa kidato cha pili alipata pigo la kimaisha na kujipata katika tandabelua huku akilelewa na baba wa kambo.

Baba huyu ndiye alimuingiza katika ukahaba. Kazi hii alikuwa anaifanya ili kumsitiri kakake mdogo pamoja na mahitaji yake ya kila siku.

“Nilipoteza mama nikiwa kidato cha pili miaka minne iliypita. Hapo nikaanza kujipata katika matatizo kidogo. Babangu wa kambo alinipeleka katika danguro ili niingize pato la kila siku.”

Binti hawa wanasimulia jinsi wanavyojipata katika matatizo kazini yao huku wakitaja wanapolisi kama changamoto kubwa. Hali kadhalika wameweza kufunguka jinsi wapo katika mahusiano na wanapotumia ujanja kuwafanya wanaume wao wasijue kazi wanayoifanya.

Pata uhondo hapa:

Former KU VC Olive Mugenda shows off daughter after graduating with PHD

Huwa wanapata kipigo kikali kutoka kwa wateja wao na wengine kukosa kuwalipa katika vyumba vya kukodi.

Joyce alianza ukahaba baada ya ufukara katika nyumba yao kukita mizizi.

Anasimulia kisa na ambapo alibakwa na marafiki wake wanne wakitoka shuleni na hapo akapata ujauzito.

“Nimelelewa na single mum na nyumbani tuko watoto watano. Mamangu anafanya kibarua na kuzungusha nguo. Ikafika kipindi tunatoka shuleni saa kumi na mbili mimi na marafiki zangu tukapatana na wanaume watano na wakatubaka na hapo nikapata mimba.”

Hatimaye wawili hawa wamejutia kuwa maisha yao yalizama katika usiku wa giza totoro na kutoa nasaha kwa wanadada wasiufuate mtindo huu.

Soma hadithi nyingine hapa:

This is why you should update your WhatsApp now!

Jombi ahofia usalama wake baada ya kuchepuka na bibi ya ndugu mdogo

Jacob alipiga simu katika kipindi cha Patanisho ili asaidiwe na watangazaji wa kipindi hicho Gidi na Ghost ili aweze kupatana na ndugu yake mdogo. W

awili hawa wamekuwa hawapatani baada ya Jacob kumwendea kinyume na kuwa mara kwa mara anachepuka na bibi yake. Kisa hiki kilifanyika jumamosi ya wiki jana.

“Ndugu yangu nilikuwa namuibia bibi yake. Sasa nilikuwa nanyemelea bibi ya ndugu yangu mdogo.Nimekuwa nikinyemelea kama mwaka mmoja. Unajua yeye ni mtu wa masafari. Bibi yake aliniambia jamaa hayuko karibu anasafiri  Mombasa.”

Soma mengine hapa:

Noisy couple screaming in lodging skip court date

 Habari za Peter kusafiri Mombasa zilipokelewa kwa shangwe na wawili hawa kwani wangepanga kutoka kwenye klabu na kujivinjari. Siri hii ya mwaka mmoja ilitoboka wakati Peter nduguye aliamua kwenda safari ya Mombasa.  Jacob alijua mdogo wake huwa katika safari za kila siku kwa hivyo akapanga na mkewe wafike klabu kulewa pombe na kujivinjari kama desturi.

“Tulikuwa tumetokea kunywa mbili tatu. Mimi niliskia mtu akikuja na akatupiga makofi na kuniuliza mbona namfanyia hivo.”

Peter alipigiwa simu na msamaria mwema aliyewaona wawili hawa na kumtaka afike klabu ajionee hali halisi ya mambo.

Ilibidi akaikatisha safari yake ya kwenda mombasa.  Alifika kwa hasira na kuwapiga makofi baadae, huku watu wakipata kuona sinema ya mchana. Baadaye alimchukua mkewe wakaenda nyumbani ili kujiepusha na aibu.

Soma hapa:

Patanisho: Bibi amtoroka bwanake baada ya kuuza shamba

Sasa Jacob anasema kuwa maisha yake yamo hatarini kwani Peter anapendekeza wakutane nyumbani katika kikao ili wazime tofauti zao na kujadili swala nzima mwanzo mwisho. Kikao hiki kinapendekezwa kifanyike nyumbani kwa  baba yao na ndugu mkubwa ambaye ni mwanapolisi.

Kulingana na Jacob huenda akapata kichapo kikubwa kutoka kwa ndugu yao mkubwa. Anataka waweze kusameheana kabla kikao hicho kufanyika

Alipopigiwaa simu na Gidi, Peter alieleza kwa machungu jinsi alivyojitolea kumpeleka shuleni bibi yake, baadae akapata ajira. Anasimulia jinsi amekuwa akiacha watoto na upweke na kuenda kulewa na ndugu yake mkubwa

Amekuambia makosa yake? Unajua kama sio nyinyi singeshika simu. Huwa naskia umbeya nasema kuwa hawezi fanya fanya hivo na bibi yangu. Nimesomesha bibi mpaka akaingia kazini halafu akuje kumnyemelea. Huyo mtu amenichezea kwa miaka mingi.  Imagine wanaacha watoto na kuenda klabu,” alihadithia Peter.

Wawili hawa walisameheana na kupanga wakutane nyumbani ili kumaliza kabisa tofauti zao.

Patanisho: Bibi amtoroka bwanake baada ya kuuza shamba

Katika Patanisho leo Peter, 41, alipiga simu katika kipindi kinachopendwa sana na kinachoruka katika kituo cha utangazaji cha Redio jambo kila siku.

Kwa njia ya kutuma ujumbe Peter alieleza  wazi wazi kuwa amekuwa katika matatizo yanayoikumba ndoa yake ya miezi 6 tangu mwaka jana.

Hawahitaji Patanisho! How Rashid Abdalla resolves disputes with wife Lulu Hassan

Ndoa yake na Caroline ilizama katika giza totoro kipindi na ambapo aliuza shamba lao. Baada ya Peter kuuza shamba, mkewe alimtaka abomoe nyumba waliokuwa wanaishi ili wayachukue mabati wakajenge nyumbani kwao.

Ili waweze kuukamilisha mjengo, wawili hawa walihamia jijini Nairobi na kukodisha chumba. Ndoa yao iliingia shubiri na wakatengana  huku Caroline akimpotelea Bwana peter.

Mtangazaji Ghost alimpigia Caroline simu ili apate kusikiliza kesi hiyo kutoka kwake. Mwanamke huyu ambaye hana mtoto na Peter alichukua simu na kunyamaza ikiashiria ghadhabu aliyo nayo kwa bwanake.

Soma mengine hapa.

Patanisho: Bi Terry amfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike

Peter alionekana amechoshwa na maisha ya upweke na kutokwa na maneno mengi. Hata hivo aliyasema ya moyoni kwa mpenzi wake huku akiamini anamskiliza

“Kama nilikukosea unisamehe. Naomba msamaha turudiane tuishi kama bwana na mke.Najua ulikasirika kwa sababu nilichukua simu yako ila naomba msamaha wako.”

Ghost alijaribu kumuuliza ni kwa nini bibiye amenyamaza na Peter akaeleza kuwa hayo ni mazoea yake.

“Huwa anapokea na haongei . Naomba msamaha kwake kabisa anisamehe. Najua nilinyanganya yeye simu lakini nitamrudishia.”

Peter alikiri yeye kuwa ana macho ya nje katika mahusiano kumechangia mkewe kumkimbia

“Unajua ile tamaa ya kuwa na wanawake wengi iliniingia lakini nitaacha uasherati. Najua kuishi bila mwanamke ni kitu ngumu sana.”

Patanisho: Bi Terry amfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike 

 

Kiprono, 28, aliwasilisha tatizo linalomsumbua na kumfanya kutatizika maishani kutoka mwaka jana mwezi wa Oktoba.

Baba huyu wa watoto wawili alikosana na bibiye Terry  na akatoroka na kuenda kwao. Mzozo huu ulianza kutokota na kurindima moto kipindi bwana huyu alipoanza kumshuku kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na wateja aliokuwa anawauzia chakula katika kibanda chake.

Soma mengine hapa.

Man begs Martha Karua for daughters hand in marriage

Wateja wake walikuwa mafundi wa mjengo uliokuwepo karibu na kibanda chake  na habari zilienea na kumfikia Kiprono huenda mkewe akawa anachepuka na mafundi hao. Wivu mwingi ukamwingia na akaanza kumshuku sana na kuanza kudadisi tetesi hizi ili aweze kuufahamu ukweli wa mambo.

Alifika nyumbani kwake saa mbili za usiku na kumkosa chumbani huku watoto wao wawili wakiwa katika hali ya upweke.

Hapa hakusita na akaamua kumpigia simu mkewe ili kujua aliko. Mama Derrick hakuchukua simu ila aliikata. Alikuwa na mafundi wake kwenye mjengo akiwauzia chakula na alihofia kuenda nyumbani kama amechelewa kwani bwanake angemchapa.

Jombi atumia gundi kumfunga mkewe sehemu za siri

Kwenye laini ya simu na kituo cha Redio Jambo kipindi kinachoruka kila asubuhi patanisho alionekana mwenye masimango na kusononeka kwani alikuja kupata ulikuwa udaku wa majirani uliofanya amshuku mkewe. Hadithi hizi za udaku wa majirani zilitia shubiri ndoa yake ya miaka 5.

Baada ya kutoroka na kwenda kwao, mama Derrick alirudi anapofanyia kazi na kumfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike ambaye walijuana kipindi na ambapo alikuwa anawatembelea nyumbani kwao. Kiprono aliichukua namba yake ya simu  na kuanza kumtongoza.

Man accused of beating wife over sukuma wiki turns anger on investigating officer

“Alinipata naye kwa chumba cha kukodisha na akaanza kulia. Hata hakumpiga cousin yake.”

Alipopigiwa simu na Gidi, mama Derrick alifunguka mwanzo mwisho kuhusu jinsi bwanake alisaliti penzi lao.

“Huyo alinikosea sana. Yaani ananiacha amenimalizia na kuenda kwa cousin kufanya naye sex. The same day !” alishangaa Terry.

“Si hata wewe uanweza mpatia miaka 10?” aliuliza Terry.

Akionekana kusimama kidete na msimamo wake Bi Terry alisema atarudi baada ya muda alioutaja mbeleni.

Nilipigwa na mke wangu mja mzito na akuniuma mgongo

“Nishamsamehe lakini hiyo miaka 10 kwanza iishe…yaani nikapata macd kwa nyumba. Sijui alikuwa ameniwekea nikuje kuona ama?”

Kiprono alimsingizia shetani kwa majaribu ya kutoka na binamu wa Terry kimapenzi

“Gidi hiyo ni shetani tu ata mimi sikuelewa vile kitu yenyewe ilihappen mwongeleshe apunguze miaka Gidi .” aliomba Kiprono.

Ninapotaka kujiua msichana wangu huwa anatokea – Njambi

Muigizaji Njeri Gachomba ambaye anaigiza katika kipindi cha House helps of Kawangware almaarufu Njambi, ameweza kuweka wazi vile ameweza kupigana na mawazo tangu alipokuwa na miaka 15.

Njambi huwa anapendwa kwa tabia yake ya kuburudisha, lakini si wote wanajua nyuma ya tabasamu na kicheko chake ni mwanamke ambaye anapigana na changamoto zote ili kupata mwelekeo.

Ilikuaje: Sijawahi sikia pengo ya kutokuwa na baba mzazi – Mammito

Njambi
Njambi

Aliweka picha katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kuandika ujumbe kuwa hiyo picha aliichukua wakati alipopoteza kila kitu alikuwa anasema ni chake.

“Nakumbuka picha hii niliweza kujipiga wakati kila kitu ambacho nilikuwa nimefanyia kazi kiliweza chukuliwa,

“Nilikuwa nimeketi kwa ngazi walipokuwa wakichukua kila kitu kutoka kwa nyumba yangu, mama yangu alikuwa na mawazo mengi na ndugu yangu @kenyan-twist kwa kawaida alikuwa ananifurahisha,

“Nakumbuka vile alikuwa ananiambia kuwa nilikuwa na bafu yangu katika nyumba yangu ya kulala na sasa nitaanza kutumia choo na kila mtu.” Alieleza Njambi.

Aliongeza na kusema kuwa alisikia kuwa maisha yake yamefika mwisho, na kusema Tamara mtoto wake aliporudi kutoka shule aliuliza bidhaa zao zi8ko wapi hasa vitu vyake vya kuchezea (toys).

47582287_526379424532233_4213355454874993200_n(2)

Njambi aliongeza na kusema vile alivyopigana na shida ya mawazo ya akili.

“Anyway, It wasn’t supposed to be a long post but anyways since am half way……

Can I just say something about depression and how sad it is that young people are ending their lives because of love, money and jobs.

I tell people life is never that serious, you loose some you gain some ..

I’ve been depressed since I was 15yrs I had family drama, I had self esteem, I felt unloved, unwanted, I felt like I meant nothing to anyone,

I’ve tried it all taking pills, countless times I’ve tried to commit suicide, I’ve wanted to jump off my balcony a million times.

I’ve scars coz I used to cut myself…. But every time I try shit, there comes Tamara complaining about something I said I’ll do and I didn’t.” Njambi alisema.

Aliendelea na kusema..

“If you ever feel depressed and you feel like you want to end your life please find a purpose, every one has a purpose for living,

I think the reason am still alive am still surviving is because of someone somewhere who is going through a lot and has no one to talk to, my DM is always open.

I understand, I know how it feels to be worthless, to have self esteem, to feel unloved I know… I am where you’re…. I get tattoos or piercings just to numb my pain…

 I don’t know why I find pleasure and comfort in pain….. And to friends please check up on your person. We depressed people don’t know how to talk, how to talk about our problems .

We might look alright but deep down we’re dying. I know I smile alot, I joke alot but when I am alone, I am empty. Plus, depression is making me so fat 🙊🙊.” Aliongeza Njambi.

 

 

Ilikuaje: Sijawahi sikia pengo ya kutokuwa na baba mzazi – Mammito

Eunice Wanjiku Njoki almaarufu Mammito ni mjeshi wa kipindi cha Churchchill, na ambaye amelelewa na mama pekee katika maisha yake.

Mammito akiwa katika mahojiano na mtangazaji Massawe Japanni alisema kuwa mama yake alikuwa anatia bidii kuhakikisha ameenda shule na pia kumlea ipasavyo.

“Nimelelewa Kibra na mama pekee, mama yangu aliweza kuhakikisha amenilea mzuri nimeenda shule,

“Nakumbuka siku moja mama yangu aliweza kulia mbele yangu kwa sababu hakuwa na pesa ya kulipa karo yangu ya shule nikiwa shule ya upili,

“Ilinibidi nitoke shule ya kulala na nirudi katika shule ya kurudi nyumbani kila siku, sijawahi sikia pengo ya kuwa sina baba,

“kwa sababu mama hajawahi nieka katika hali ile ya kujiuliza kwanini baba yangu hayuko karibu.” Akieleza Mammito.

mammito
comedian Mammito Euniece

Mcheshi huyo ni kifungua mimba wa familia ya watoto watatu, huku akisema kuwa maisha ya ‘ghetto’ si rahisi na aliweza kulelewa na shida nyingi sana.

Akiongeza mcheshi Mammito alisema kuwa hajui baba yake na wala hajawahi sikia pengo kuwa hana baba kwa maana mama yake amekuwa naye kwa kila jambo.

“Mimi sijawahi jua baba yangu wala sijawahi sikia ile pengo ya kuwa sina baba mzazi, sijawahi uliza mama yangu sababu ya kuachana na baba yangu,

“Najua alikuwa na sababu kubwa ya kuachana na baba yangu, huwa tu namuuliza na mzaa baba yangu ni nani, na pia sijawahi jua sababu kuu ya wao kuachana,

“Sipendi kurudisha mama yangu nyuma kwa kumuuliza maswali hayo inaweza kuwa alipitia changamoto nyingi ndio maana waliachana.” Mammito alisema.

Mammito alisema kuwa alianza kazi ya ucheshi akiwa na miaka 22, na alijua kuwa ana talanta ya ucheshi tangu utotoni kwa maana aliweza kumsumbua mama yake sana.

Pia alisema kuwa alikuwa na matumaini kuwa ataweza kutoka katika maisha duni na kuwa mtu wa maana.

“Nilianza kazi ya ucheshi nikiwa na miaka 22, na pia nilianza uhusiano wa kimapenzi nikiwa nimemaliza shule ya upili, kisha baadaye nikaweza kuumizwa roho.” Aliongea Mammito.

 

 

Waathiriwa wa ajali ya ndege hawatawahi patikana – CEO Ethiopian Airlines

Ni kilio ambacho jamii za waathiriwa wa ajali ya ndege ya Ethiopian ET 302 iliyoanguka baada ya kuong’o nanga wanalia mioyoni mwao na huzuni ambao wanao, kwa kuto pata mili ya watu wao katika tukio la ajali hiyo.

Ni majivu tu na baadhi ya viungo vya mili yao ambavyo vimesalia kama ukumbusho wa wana jamii, jana jamaa zao waliweza kufika katika tukio la ajali hiyo lakini matumaini yao yaliambulia patupu.

Ahmed Khalid alikosa kusafiri na ndege ya Ethiopian iliyofanya ajali

53320153_419773955259491_2899677319877867493_n(2)

Baadhi ya mili ya watu 157 wakiwemo wakenya 32, waliohusika kwa ajali hiyo haitawahi onekana wala kutambulikana na hata kuzikwa kwa sababu waathiriwa hao waliweza kuchomeka hadi kuwa majivu.

Katika mahojiano kwa runinga ta BBC na CEO wa Ethiopian Airline, Tewolde Gebremariam aliweka wazi kuwa mili mingi ilichomeka na moto na baadhi ya viungo ndivyo vimeweza kupatikana.

0_People.walk.at.the.scene.of.the.Flight.ET.302.plane.crash.near.the.town.of.Bishoftu

“Wakati nilipowasili katika tukio la ajali, ndege ilikuwa kabisa chini ya ardhi na hakukua na ishara ya ndege hiyo ardhini,

“Ilitubidi tuanze kuchimba ili kutoa mabaki ya ndege hiyo na tukaanza kutafuta mili ya waathiriwa,

“Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hatukuweza kupata mili yeyote, tumeweza kupata baadhi ya viungo ambavyo ni vidogo sana,

“Hiyo ndiyo changamoto ambayo tuko nayo kwa sasa.” Alieleza CEO Tewolde.

R.I.P: Familia kuomboleza kifo cha rubani wa ndege ya Ethiopian Yared

Cedric Asiavugwa ambaye alikuwa miongoni mwa waathiriwa hao, alikuwa anaishi Washington DC na alikuwa amekuja katika  mazishi ya mama mkwe wake.

Cedric Asiavugwa
Mwenda zakeCedric Asiavugwa

Baba yake Thomas Govedi akiongea katika mahojiano na stesheni moja nchini alisema kuwa alizidiwa na habari hizo za kuhuzunisha,  lakini aliongeza na kusema hatakama ni kidole ambacho watapata wataweza kukizika.

“Ata kama ni kidole tutapata tutakizika.” Aliongea Timothy.

Cedric ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Georgetown na ambaye alikuwa anasimea sheria, alikuwa aweze kuhitimu baada ya miezi miwili.

Ujumbe wake wa mwisho aliandikia mke wake akimpa faraja kwa kumpoteza mama yake, ufuatao ni ujumbe ambao alimtumia mke wake.

“THE GREAT AND SAD MISTAKE OF MANY PEOPLE — AMONG THEM EVEN PIOUS PERSONS — IS TO IMAGINE THAT THOSE WHOM DEATH HAS TAKEN, LEAVE US.

THEY DO NOT LEAVE US. THEY REMAIN! WHERE ARE THEY? IN DARKNESS? OH NO! IT IS WE WHO ARE IN DARKNESS.

WE DO NOT SEE THEM, BUT THEY SEE US. THEIR EYES, RADIANT WITH GLORY, ARE FIXED UPON OUR EYES . . .

OH, INFINITE CONSOLATION! THOUGH INVISIBLE TO US, OUR DEAD ARE NOT ABSENT. THEY ARE LIVING NEAR US, TRANSFIGURED INTO LIGHT, INTO POWER, INTO LOVE.” Aliandika.

 

 

Polisi kumpiga mke wake risasi baada ya mgogoro wa kifamilia

Afisa wa polisi wa Utawala alimpiga mke wake risasi. Hii ni baada ya kuwa na mgogoro wa kifamilia eneo la Navakholo kaunti ya Kakamega.

Kisa hicho kilitokea Alhamisi usiku, inamaana polisi huyo hajui kutumia silaha yake ipasavyo?

Bride dies from a mystery illness on honeymoon just six days after wedding

Polisi huyo aliweza kutoweka baada ya kumuuwa mke wake ambaye ni mwalimu katika shule ya upili ya Navakholo, wakazi waliweza kuandamana baadaye na kuwazuia polisi kuchukua mwili wa marehemu.

unnamed(5)

Walisema kwanza matakwa yao yaweze kutimizwa kwa polisi kumleta muuaji huyo kwanza ili waweze kubali mwili wa marehemu kuchukuliwa.

Iliwabidi polisi waweze kuwatawanya wakazi hao ili waweze kuchukua mwili huo, hali jawekwa wazi kwanini wapenzi hao waliweza kuwa na mgogoro uliosababisha kifo hicho.

Wizara ya elimu kufanya uchunguzi katika shule ya upili ya Kangaru

CID wa kaunti ya Kakamega John Onyango alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa polisi huyo hajaweza kukamatwa.

“Hatujui polisi huyo aliweza kupiga risasi ngapi, lakini polisi wako katika tukio la kisa hicho.” Alisema John.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kakamega.

KWINGINEKO: Nikuwa…

Watu watatu wamefariki kufuatiana mapigano mapya kati ya Borana na Gabra katika eneo la Haro Giresa kata ndogo ya Saku.

Wengine walipata majeraha ya risasi baada ya mapigani Jumatano, waliweza kupelekwa katika hospitali ya Marsabit kwa matibabu, polisi wa usalamu wametumwa katika maeneo hayo ili kutuliza jambo hilo.

Msichana wa 11 kunajisiwa katika kaunti ya Samburu

crime_scene_tape

OCPD wa eneo hilo la Marsabit Benjamin Mwanthi alithibitisha kisa hicho na kuwaambia wananchi waweze kutulia kwa sababu polisi wanashughulikia kisa hicho.

Zidane secures his first Madrid signing since return as they announce Militao

Mwenyekiti wa baraza la madhehebu Mohamednur Kuli aliwaambia wakazi kuwa waweze kuwa na amani kwa sababu umoja na amani ndio unaweza kuleta maendeleo katika eneo hilo.

Mvutano kati ya jamii hizo mbili umekuwa kwa muda mrefu na ambao umeweza kufanya watu wengi kufariki hapo awali.

 

Siyuko hapa kwa ajili ya biashara ya nyani – Magoha awaambia wabunge

Waziri mteule wa elimu Prof. George Magoha alisema kuwa hataki kazi yoyote kama wabunge wataingililia kazi anayofanya, aliongeza na kusema kama wambunge hao wanafikiria ameenda kufanya biashara ya nyani waweze kuweka kazi yao.

Mpasuaji, profesa na mwanabiashara Magoha alisema kuwa hajawahi shindwa na kitu chochote na hataweza kuvumilia ‘Monkey business’ kama atachukua usukani katika wizara hiyo.

Education CS nominee Prof George Magoha during his vetting at County Hall on Thursday
George Magoha

“Katika miaka yangu yote ya upasuaji, naweza jivunia nikisema kuwa hakuna mtu yeyote ambaye alikufa akiwa katika meza ya operesheni,

“Na nikishindwa katika nafasi hii itakuwa mara ya kwanza, na sikuweza kutetea uteuzi wangu bali ni utalaamu wangu,

“Kama hilo ndilo mnataka basi nitawatolea, lakini kama kuna shughuli ambazo hazieleweki mnaweza kuweka kazi yenu.” Magoha aliwaambiwa wabunge alipokuwa kwenye mkutano kwa uteuzi.

Waziri huyo alisema kuwa anapenda kufanya kazi kutoka upande wa nyuma kuenda mbele, alionyesa ujasiri wake kuwa ataweza kuleta ubora katika sekta ya elimu.

“Ninapo weka macho yangu kwa kitu fulani, kwanza ninaangalia ninachotaka kufikia, alafu kutoka hapo ninaanza kazi yangu.” Alieleza Magoha.

DCI kuchunguza waziri Kiunjuri na Wamalwa juu ya kashfa ya mabwawa

Aliweza kujipiga kifua na kujigamba kuwa na mali ya millioni 250, na kujitambulisha kama mkristo kamilifu wa kanisa la katoleki.

Profesa huyo aliwaambia maafisa wa wizara ambao wana shuguli za rushwa waweze kabadilisha mienendo yao kabla hajawatambua, aliwaonya pia ambao wanawaomba wasichana wa shule wafanye ngono na wao huku akisistiza kuwa siku zao zimehesabiwa.

Pia aliingia katika mjadala wa mitandao ya filamu za ponografia na kupendekeza iweze kufungwa.

“Kama bunge hili itakubali uteuzi wangu, basi ombeni Mungu sana nisiweze kuwapata mkiwaambia wasichana washule wapanue miguu yao.” Magoha alisema.

Aliweza kusema kuwa na uwazi na ushiriki katika elimu ya ngono. Magoha alionyesha nia yake kuweka sura katika mtaala mpya, aliitisha fedha za kutosha ili kuhakikisha mafanikio ya utekelezaji.

Wazazi wape watoto fursa ya kukuza vipaji! – Sauti Sol

“Ukweli ni kuwa tuko nyuma sana katika mtaala huo mpya, Rwanda wamefanya na pia Sudan kusini wamefanya, na maanisha kuwa nchi yetu ya Kenya inapaswa kuwa ishaanza mtaala huo na kisha nchi zingine zifuatie,

“Nitaenda kuamsha mtaala mpya.” Alisema Magoha.

Aliweza kuunga mkono kuongezwa kwa karo ya vyuo vikuu mpango ambao ulikuwa umeanzisha lakini si zaidi ya vile ilikuwa imeongezwa.

Alisema kuwa ni lazima karo iongezwe ili iweze kuwa sawa na nyakati hizi za kiuchumi, Magoha alihaidi wanafunzi ambao usajili wao uliweza kukataliwa kwa kutumia vyeti vya kazaliwa visivyo halali kukalia mtihani wa kitaifa.

Mwezi jana (Kenya National Examinations Council) walikataa usajili wa wanafunzi 370,000, baadaye iliweza kusema kuwa wanafunzi hao watapewa nafasi ya pili kurekebisha makosa yao na kisha kukalia mtihani.

 

 

 

Shida zangu zinatokana na kusaidia watu – Bahati alizungumzia utata

Akihudhuria Malaika Tribute Awards Jumatano, msanii Bahati aliweza kuongea mwishowe na kuzungumzia utata ambao unamkumba kwa sasa.

Msanii ameweza kutuhumiwa kwa kumuitiapolisi  bibi ya msanii Seed Nimo Gachui, na kisha kukataa kulipa Mr Seed pesa zake.

Sababu za kutomueka baba wa mtoto wangu kwenye mitandao – Awinja

Bahati alikataa kuguzia kisa cha msanii Mr Seed kutoka katika kampuni ya EMB, lakini katika mahojiano alisema,

Bahati
Bahati

“Shida yangu kubwa ambayo nimekuwa nayo kutoka Disemba ni kutokana na ukweli kuwa huwa nawasaidia watu,

“Lakini mwisho mwa siku utaweza kusaidia, kwa sababu baraka za mtu huwa zinatokana na kusaidia.” Alisema.

Akiongeza alisema kuwa hajawahi kujibu mambo kama hayo, “mambo yangu mingi huwa tu inaendelea kama kawaida”.

Aliendelea na kusema…

Ilikuaje: Niliwachana na baba wa mtoto wangu kabla ya kujua nina uja uzito – Pierra Makena

“Unavyo itwa na Mungu huwa unamgonja ili akupe maneno yanayofaa, unapoanza kuongea bila usaidizi wake ama mwongozo wake,

“Utashtukia tu umeharibu kila kitu na kuongea kando na ambacho ungefaa kuongea, mungu huwa anaongea kwa wakati wake, anaweza kawia lakini itakuja kupita.” Alizungumza.

Alieleza kwanini hajawahi jibu madai hayo ambayo wasanii wengi wameweza kusema na pia mwingine kujitokeza na kusema kuwa amemdai Bahati.

Raila Odinga Junior reveals Lamba Lolo hit makers are his favorite artists

“Biblia inasema katika kitabu cha James 1:9 Wapenzi ndugu zangu, kumbukeni haya, kila mtu anapaswa kuwa na haraka ya kusikiza, mpole kwa kukasirika na mpole pia kwa kuongea,

“Ndio maana huwa sikasiriki haraka.” Bahati alieleza.

Aliweza kuongea na kupunguza sauti yake na kuuliza waandishi “kama singewahi kuwa simgefunga duka zenu?

Exclusive: Dj Mo addresses rumours that he cheated on Size 8

Akiongeza..” Nyinyi watu mmeandika zaidi ya mada 19 kunihusu.” Aliongeza Bahati.

Mke wa aliyekuwa maneja wake Mutua aliweza kuandika ujumbe mkali kwa Bahati akimuita atoke katika biashara yake sugu.

Ufuatao ni ujumbe ambao mwanamke huyo aliweza kuandika..