Raila Junior aomba msamaha kuhusu matamshi yake ya ‘ODM slay queen’

Mwanawe kiongozi wa ODM Raila Odinga  ,Raila Junioe ameomba radhi kuhusu  ujumbe wake wa twitter ulioonekana  kuwakashifu viongozi wa ODM Kuhusu ajenda zao  . Raila Junior   jumanne alisema chama hicho kinafaa kurejelea mkono wake  wa hapo awali

“…  Chama chetu sio tu kuhusu ndege za kibinafssi na  Slay queens  na kuwatukana viongozi wengine ,tuna ajenda ya maendeleo  ambayo ipo katika manifesti yetu’ Raila Jr alisema

Mbunge Alice Wahome aishtaki Serikali kuhusu kuruhusiwa kwa Mohammed Badi katika baraza la mawaziri

Lakini jumatano Junior alibadilisha msimamo wake akisema huenda ujumbe wake huo ulichukuliwa vibaya akisema ;

” Ufafanuzi …kama mwanachama wa kawaida wa ODM Maoni yangu  sio ya chama . Nakishukuru chama cha ODM  kwa kuruhusu demokrasia na kumpa kila mtu fursa ya kutoa maoni yake’ alisema

” Maoni yangu hayamlengi kiongoi yeyote  na naomba radhi  kwa  kutafsiriwa vibaya kwa ujumbe wangu’

Msamaha wake hata hivyo hakuchukuliwa kwa wepesi kwani watu wengi walionekana kuendelea kumkosoa wakimtaka akome kuzungumzia masuala ya chama cha ODM .

Mbona Uganda ilikimbilia Tanzania na kuiacha Kenya katika mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta?+Podi ya Yusuf Juma

” Wewe na mjombako Oburu  mnafaa kujifiche sehemu Fulani hadi mikakati yote ianze kutekelezwa .. hamwezi kufunga midomo yenu’ @RealOmbatiEdwin said.

@patroba said ” Ulisema ukweli . kwa kweli chama cha ODM  kinadidimia .huwezi kulinganisha ODM  ya mwaka wa 2007 na ODM YA 2020  mtu Kama Sifuna runs ODM like his pit latrine.”

 

 

Murkomen na Raila Junior warushiana cheche za maneno kwenye Twitter

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na mwanawe kinara wa ODM Raila Odinga Jumatano, Juni 24 walirushiana makonde kwenye  mitandao ya kijamii ya twitter.

Wawili hao walijibizana kuhusu ujumbe aliokuwa ameuchapisha Murkomen 2017 wakati Raila alikuwa akiapishwa kama rais wa wananchi.

Junior alizungumza kuhusu masaibu anayopitia Murkomen baada ya kutimuliwa na Jubilee kutoka wadhifa wake.

Raila Junior
Raila Junior

Kijana huyo wa Raila alimkumbusha seneta huyo aliyokuwa ameambiwa hapo awali alipokuwa akimcheka Baba na masaibu yake.

“Kuwa mamlakani ni utamu. Maneno haya yamekuja kumpata Murkomen.”Aliandika Raila Junior.

Hata hivyo, Murkomen alikerwa na maneno hayo na kumtaka Raila Junior kumwandikia babake hayo au Ikulu. Alijigamba kuwa ameweza kuafikia makubwa kuliko aliyokuwa ameafikia Raila katika umri alio nao seneta huyo.

Ni majibizano ambayo yalizua hisia mseto kutoka kwa Wakenya wengine kwenye mtandao.

Majibu Nayo! Tazama jinsi Raila Odinga Junior alivyorusha ‘kombora’ twitter

Mwanawe kiongozi wa ODM Raila Odinga Junior  jana amempiga mmoja wa watumizi wa twitter  kumbo kali sana pale twitter alipojaribu kutilia doa kiwango cha masomo yake . Jamaa huyo Joseph Omondi alijutia mbona alianzisha vita hivyo na Junior kwani jibu lake sio lililotarajiwa .

Dennis Okari na mkewe Naomi washerehekea mwaka mmoja tangu wafunge ndoa 

Wengi wa wanaotumia twitter wanbafahamu kwamba mfalame wa majibu makali huwa   wakili Miguna Miguna lakini huenda anapata ushindani kutoka kwa Raila Junior . Hata hivyo wengi wa waliofuatilia majibizano hayo kati ya Omondi na Raila Junior walionekana kughadhabishwa na jibu ambalo Junior alilitoa wakisema kama mtoto wa  Raila Odinga ,alifaa kuonyesha  ustaarabu kidogo mtandaoni .

 

Katika majibizano hayo Omondi alikuwa akieleza kwamba mwanawe Naibu wa rais  June Ruto ana kisomo zaidi ya Raila Junior na hivyo basi anastahili kushikilia nafasi  anayohudumu  kama mwakilishi wa balozi huko Poland .Hata hivyo majibu ya RailaJunior yalimuacha kila mtu kinywa wazi .

 

 

 

Ilikuaje: Tulikaa na mke wangu kwa miaka 5 bila kupata mtoto – Raila Junior

Raila Junior ni mtoto wa kinara wa ODM Raila Odinga, ni mwana biashara ambaye ana kampuni zake ambaye ni mzalishaji wa kampuni zake.

Akiwa katika mahojiano na Massawe Japanni, alisema kuwa watu wengi huwa wanampa kazi si kwa ajili yeye ni mtoto wa Raila bali kwa sababu wanajua utaalamu wake uko katika kiwango cha juu.

Ilikuaje: Rahab Nyawira asimulia vile alikuwa mwizi wa mabavu

“Watu wanapotupa kazi ili tuwafanyie huwa wanatarajia kazi mzuri si kwa ajili wanajua mimi ni mtoto ama mtu ambaye ametoka kwa familia kubwa,

“Huwa nafanya kazi na kampuni kubwa kwa ajili ya utaalamu wangu na wanajua kuwa uko katika hali ya juu.” Alisema Raila Junior.

Raila Junior akiwa katika miaka kumi ndipo aliweza kumuona baba yake mzazi ambaye ni Raila kinara wa chama cha ODM.

“Niliona watu wakiwa wamejaa nyumbani kwa mama yangu hapo ndipo niliweza kumuona babayangu,

“Nilikuwa mtoto mdogo kwa hivyo sikujua ni nini kilichokuwa kinaendelea, huwa napingana au natofautiana na baba yangu kwa mambo ambayo huwa anasema,

“Si kwa sababu simpendi lakini huwa na msimamo wangu, hilo ni jambo la kawaida katika familia.” Raila Junior aliongea.

Kwa mara nyingi katika mitandao ya kijamii Raila Junior huwa anatofautiana na babayake, alisema kuwa Raila ni mwanadamu wa kawaida.

“Baba huwa anakasirika wakati jambo linaenda vile halistahili.” Aliongea.

Ilikuaje: Niliimba nyimbo lakini hazikuwa zinanipendeza – Kush Tracey

Mwanabiashara huyo alisema kuwa wakati walipompoteza ndugu yao wa kwanza Fidel Odinga, lilikuwa pigo kubwa kwa familia  kwa sababu alikuwa anawalinda mzuri kama kifungua mimba.

Akiongea katika mahojiano hayo, alisema kuwa waliweza kukaa miaka mitano na mke wake bila kupata mtoto lakini kisha baadaye aliweza kubarikiwa na mtoto mvulana.

“Tulikaa kwa miaka mitano bila kupata mtoto, sikuweza kumsukuma bibi yangu kwa maana kila mtu alikuwa anasukumwa nje na marafiki,

“Baadaye na mshukuru Mungu kwa sababu aliweza kutubariki na mtoto mvulana,” Alisimulia Raila Jumior.

Alisema kuwa hana nia yeyote ya kisiasa kwa sasa labda katika maisha ya baadaye kwa maana kwa sasa anakuza biashara na kampuni zake.

Raila Junior alisema kuwa yeye huwa anakula mahali popote yaani hoteli zozote, na kutozungumzia ama huwa na walinzi.

“Mimi huwa nakula mahali popote hotelini Mombasa hata hapa mjini Nairobi, kwa sasa siwezi ongelelea ama niko na alinzi kwa sababu ya usalama wangu,” Raila Junior alisema.