‘Wacha ajue nilifunzwa kunukuu bibilia tangu utotoni,’Ruto amjibu Raila

Vita vya maneno vimeshuhudiwa mara kwa mara kati ya naibu rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga huku vikizidi endapo wawili hao wanazungumza kwenye mkutano wowote.

Ruto mnamo Jumanne alimpa jibu kinara huyo baada ya kusema kuwa Ruto amekuwa akinukuu biblia hata kushinda maaskofu.

Ruto apuuzilia mbali uvumi kuwa Uhuru atasalia mamlakani

Ruto 1

“Wiki iliyopita aliambia watu wa Taita Taveta kuwa DP ananukuu Biblia kuliko hata maaskofu na anapenda kuenda kanisa. Mimi nilifunzwa kuhusu neno

Kama kuna kurasa zimeandikwa kuhusu uganga, basi hiyo mimi sijui. Yeye anaweza kuongea kuhusu hilo. Huyo wachaneni na yeye

Wacha ajue nilifunzwa kunukuu biblia tangu utotoni.” Alizungumza Ruto.

Raila amewaonya viongozi vya kanisa dhidi ya kuchukua msaada wa pesa kutoka kwa naibu rais kwa maana hiyo ni moja wapo ya njia ya ufisadi.

Eliud Owalo ajiunga na kambi ya DP Ruto kabla ya kipute cha 2022

Raila Odinga
Raila Odinga

Kwenye ziara yake ya ukanda wa Pwani, Raila alimfananisha Ruto na mtu mnafiki anayetumia kanisa na mali yake kuwateka wananchi kisiasa.

Hata hivyo, wafuasi wa Ruto wametupilia mbali mishale ya maneno kutoka kwa wakosoaji wake wakisema wanachomwa roho kwa kuwa anaelewa masaibu ya raia.

Raila awarai wawakilishi wa Taita Taveta kutotekeleza mageuzi katika uongozi wa bunge hilo

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewaraia wawakilishi wa bunge la kaunti ya  Taita taveta ambao ni wanachama wa ODM kutofanya mageuzi ya uongozi wa bunge hilo ili kukiboresha chama cha ODM katika eneo hilo.

Mkuu wa NMS Badi Kuhudhuria mikutano ya baraza la mawazi baada ya kula kiapo cha kuweka siri

Raila  alifanya mkutano wa faragha na waakilishi hao akiwa ameandamana na gavana wa taita taveta Granton Samboja, mwenzake wa Mombasa Hassan Joho na katibu mkuu wa ODM  Edwin Sifuna. Wengine waliokuwepo katika mkutano huo ni  seneta  Jones Mwaruma  na wabunge  Johnes Mlolwa wa Voi na  Danson Mwashako wa Wundanyi.

Raila alianza  ziara yake ya siku mbili kulivutia eneo hilo upande wake  siku ya Jumatano. Kumekuwa na mgogoro wa uongozi katika bunge la taita  taveta. Juni mwaka huu wawakilishi wa kaunti walimfurusha  kiongozi wa wengi Jason Tuya na kumpa kazi hiyo  Harris Keke wa  wadi ya Rong’e.

EACC yawaonya magavana kuhusu azimio la kuvinyima vyombo vya habari pesa za matangazo

Ziara ya Odinga katika eneo hilo inajiri wiki moja tu baada ya naibu wa rais William Ruto kuzuru eneo hilo  na kufanya mkutano na viongozi wa kidini katika eneo la Taveta. Raila anaendelea na kampeni zake kuipigia debe  Ripoti ambayo haijatolewa ya BBI na mchakato mzima wa ‘Handshake’ kati yake na rais Uhuru Kenyatta

 

Gavana Wycliffe Oparanya aachana na azma yake ya urais

Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya ameachana na azma yake ya uaniaji kiti cha urais mnamo mwaka wa 2022 ili kumuunga mkono kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.

Akizungumza gavana huyo alisema kwamba angependa sana kupata uongozi wa chini na wala si gavana mwaka huo.

Pia alimwambia Raila kuwa endapo kuwa kiongozi amtafutia kiti huko wakati muhula na muda wake utakwisha.

Acheni mchezo! Wabunge wa Tanga Tanga waambia Wamalwa na Oparanya kwa kumtembelea Gideon Moi

oparanya

“Naachia wengine siasa za kaunti baada ya muda wangu kukamilika, nataka kuangazia siasa za nchi na kumuuliza Raila kunitafutia kiti huko juu.” Aliongea Oparanya.

Usemi wake unajiri siku chache baada ya gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua kuzindua zabuni yake ya urais, pia gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana alidai kuwa atawania kiti cha urais ifikapo mwaka wa 2022.

Oparanya,Wamalwa wamewarai MCAs kutupilia mbali miswada ya kuwatimua magavana

Je nani atakayeshinda katika kinyang’anyiro cha uwaniaji kiti cha urais, na je kinara wa ODM atawania kiti hicho?

Cleophas Malala atembelea jumba la Capitol Hill baada ya Raila Odinga kumsuta

Siku chache baada ya kinara wa ODM Raila Odinga kumsuta seneta Cleophas Malala, Jumapili kwa kupinga mfumo mpya wa ugavi wa mapato hatimaye ameweza kumtembelea kinara huyo afisini mwake Capitol Hill.

Raila alishangazwa endapo Malala alichaguliwa kuwakilisha watu wa Kakamega baada ya kupinga mfumo huo, huku akimsuta Seneta huyo Raila alikuwa na haya ya kusema,

‘Wengi wanasema kuna siri kati yangu na Uhuru ya kumtapeli Raila,’Ruto ajibu

“Endapo umechaguliwa kama mbunge ama seneta, unatakiwa kuwakilisha watu. Mfumo umewasilishwa seneti lakini unasema hautaki kuwanyima watu wa kaunti zingine pesa, umechaguliwa kweli na watu wa Kakamega?

Endapo kuna seneta ambaye kaunti yake inapokea pesa nyingi lakini anapinga mfumo huo sio eti anawapenda watu wa kaunti zingine, kuna shaka.” Alizungumza Raila.

Ni ugavi wa mapato ambao unaungwa mkono na baadhi ya maseneta huku wengi wakiupinga, baada ya kuwa na mkutano na kinara huyo Malala alisema kwamba,

“Nimechangamka kwa kuwa na mazungumzo na mheshimiwa Raila Odinga kuhusu mkazo unakabili ugavi wa mapato katika seneti, tulipata kuwa ugavi wa mapato ya shilingi moja mwananchi mmoja inasaidia kaunti zote ili kuweka utulivu wa nchi yetu

Raila akejeli maseneta wanaokataa pesa katika mfumo mpya wa ugavi wa mapato

Nilimhakikishia kinara Raila Odinga kuwa mimi na wenzangu tutajadili kuhusu ugavi huo kwenye seneti.”

Seneta imeahirisha kikao chao cha ugavi wa mapato zaidi ya mara tatu kwa kutoskizana kwa maseneta.

‘Endeleeni kumuunga baba na Uhuru Kenyatta mkono,’ Sonko awaambia wananchi wa Kisumu

Hku akihudhuria mazishi ya mwendazake mwanakandanda Kevin Oliech ambaye alikuwa nduguye kiranja ya timu ya Harambee Stars Dennis Oliech ambaye aliaga dunia akiwa ujerumani akipokea matibabu ya saratani, hii leo Sonko aliwashukuru wakazi wa Kisumu kwa kumkaribisha na heshima kubwa.

Sonko kugharamia mazishi ya Kevin Oliech

Huku walinzi wake wakijaribu kutafuta njia katika ukumbi wa vijana wa eneo hilo, nguvu zao zilifua dafu baada ya vijana hao kusema gavana Mike Sonko awahotubia mwanzo ili aweze kuhudhuria mkutano wa mazishi ya mchezaji huo.

Sonko 1

Hakuwa na jambo la kufanya alifungua gari lake na kuwahotubia vijana hao, alipokuwa anazungumza aliwashauri wenyeji waweze kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta na Raila kwa umoja wa taifa.

“Watu wa Kisumu nina furaha kwa maana mmenikaribisha vyema humu, nataka kuwashauri na kuwaambia mwendelee kumuunga baba na rais Uhuru Kenyatta mkono

Kwa ajili ya umoja wa taifa letu.” Alisema Sonko.

Usikubali hawa ministers wakuharibie jina-Gavana Sonko amwambia Uhuru

Pia alizungumzia kutokuwa na kazi kwa vijana huku akisema handisheki ijayo itashughulikia shida hiyo.

“Najua vijana wengi huku kisumu hawana kazi, nawahakikishia kuwa serikali na hendisheki ijayo itashughulikia jambo hilo.”

Raila akutana na Robert Njura jamaa aliyemvusha kwa boti hadi Uganda mafichoni

Aliyekuwa waziri mKuu Raila Odinga amekutana na    Robert Njura ambaye aliokoa maisha yake mwaka wa 1991 alipokuwa akikimbia kwenda mafichoni nchini Norway akitoroka utawala wa rais Daniel Moi .

rao 2

Raila asema atatangaza mipango ya 2022 baada ya mchakato wa BBI

Njura aliyekuwa kijana wa maka 19 wakati huo alimvusha Raila katika ziwa Victoria kuingia nchini Uganda  wakati Bwana Odinga alipokuwa akisakwa na maafisa wa polisi . Njura wakati huo alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu na kwa kazi yake ya kumvusha Odinga hakujua  mteja wake alikuwa nani na baada ya kulipwa shilingi 2000 kwa kazi yake ndipo alpojulishwa kuhusu ‘mteja’ aliyevushwa kuingia Uganda .

rao 3

Kulingana naye ,baadhi ya vijana katika eneo hilo walikataa kumvusha bwana Odinga kwenda Uganda kutumia boti lakini yeye alijitolea . Odinga amesema mchango wa  Njura  katika kubadilisha mkondo wa siasa nchini kupitia hatua hiyo yake ni mkubwa na hauwezi kusahaulika .

rao 4

 

Kenya ni Yetu:Raila na Kagwe kufungua tamasha kubwa ya muziki inayolenga kuwapa wakenya matumaini

Odinga  ameandika ujumbe katika mitandao  ya kijamii akimsifu Njura kwa hatua hiyo yake akisema ;

‘ Ni  heshima kubwa kukutana  na Robert Njura aliyenivisha kwa boti nchini Uganda nikienda mafichoni Norway .Njura ni dhihirisho kwamba ukakamavu ,kujitolea  na nguvu za vijana kunaweza kuafikia mengi. Mungu ambariki pamoja na vijana wetu katika maadhimisho haya yam waka wa kumi  tangu tuipate katiba mpya’ Odinga ameandika

rao 5

 

Kenya ni Yetu:Raila na Kagwe kufungua tamasha kubwa ya muziki inayolenga kuwapa wakenya matumaini

Kiongozi wa upinzani Raila na waziri wa Afya Mutahi Kagwe wanatarajiwa kufungua tamasha kubwa ya muziki  ya  waathiriwa a Covid 19 jumamosi kuanzia saa mbili usiku .

‘Kenya imekuwa nyumba ya pili kwangu,’Gramps Morgan azungumzia tamasha la Kenya Ni Yetu

Odinga  atawapa himizo wakenya kuungana  wakati huu wa janga la corona  ilhali Kagwe atazidisha wito wake wa wakenya kujikinga dhidi ya virusi hivyo kwua kuvalia maski ,kuosha mikono na kutorundikana  katika sehemu moja .

Kagwe

Tamasha hiyo imewaleta pamoja wasanii wazito na majina tajika katika muziki wa humu nchini wakiwemo  Sauti Sol. H_Art The Band, Eric Wainaina, Sammidoh, Suzanna Owiyo, Redfourth Chorus, Elizabeth Njoroge, na  Nairobi String Quartet  pamoja na msanii  wa rege  Morgan Heritage.

Tamasha hiyo muziki imepigwa jeki na muungano wa wamiliki wa vyombo vya habari  na litatapeperushwa mubashara kutoka  All Saints Cathedral , Nairobi.

Raila odinga
Raila odinga

“ Janga la Covid 19 limewaathiri wanahabari,wahudumu wa afya ,watangazaji na wananchi . Wakati huu wa  simanzi na uchungu  tunasimama na waknya tukiamini kwamb tutafaulu katika  vita dhidi ya janga hili’ Amesema mwenyekiti wa MOA Wachira Waruru

Kenya ni Yetu Live! Concert, bonge la show kudhihirisha ustahimilivu wa wakenya

Tamasha hiyo inadhaminiwa na  Stanbic Bank  na itapeperushwa kwa njia ya kidijitali  kupitia   www.yetulive.com  na  Kiss TV, Citizen TV, NTV, K24, KTN, Switch TV, Family TV, 3 Stones TV, Kass TV, TV47, KBC  na vituo vikubwa vya redio

 

 

 

 

 

 

 

Raila asema atatangaza mipango ya 2022 baada ya mchakato wa BBI

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amesema atatangaza mipango yake ya uchaguzi wa 2022 baada ya kutamatika kwa mchakato wa BBI . Odinga amesema anazingatia hatua kadhaa lakini uamuzi wake utakuwa wazi baada ya kukamilishwa kabisa kwa  utaratibu mzima wa BBI.Odinga amesema kwa sasa yeye na rais Uhuru Kenyatta wataangazia mwafaka wao wa handshake na  atasalia kimya kuhusu siasa za urithi wa 2022.

Ruto aanza mikutano ya mashinani, Ijumaa atakuwa Mombasa

Raila  ameongeza kwamba makubalaino yake na Uhuru kusitisha uhasama yalilenga kudumisha Amani nyakati za uchaguzi .

“  Rais hatazoungumzia uchaguzi wa 2022,mimi pia Sitazungumzia uchaguzi huo . Nitazungumza kuhusu 2022 baada ya kutamatika kwa mchakato wa BBI, Raila amesema katika mahojiano na Runinga ya Citizen jumanne usiku .

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa bwana Odinga kuzungumza kuhusu anavyopanga kushughulikia uchaguzi wa 2022 ingawaje kuna ishara kutoka kwa washirika wake kwamba huenda analenga kugombea kiti cha urais kwa mara ya tano .

Wakati wa kurekebisha katiba iwe bora ni sasa-Uhuru

Naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe na  katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi Cotu ,Francis Atwoli  wamedokezea kwamba Raila  ndiye atakayemrithi rais Kenyatta .

Lakini katika mahojiano hayo ,Raila alisema wanaotoa pendekezo hilo wana haki yao ya kidemokrasia kutoa maoni yao.

 

 

Pesa sabuni: Tazama picha za sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama Ida Odinga

Mkewe kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, Mama Ida Odinga alifikisha miaka 70 wikendi iliyopita familia yake na marafiki walimwekea sherehe ya kifahari na ya kipekee ili kusherehekea siku hiyo ya kipekee.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu tofauti. Hata hivyo wengi walifuata kanuni za wizara ya afya ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Huku wengi wakikaidi kanuni hizo kwa maana baadhi ya viongozi wa humu nchini hawakuwa wamevalia maski.

EgC2RuhXsAE7DJt

Baadhi ya viongozi na waliohudhuria sherehe hiyo ni naibu mwenyekiti wa chama cha jubilee David Murathe, aliyekuwa mbunge wa Gatanga Peter Kenneth, gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru na kiongozi wa wanawake wa Homa bay Gladys Wanga.

Wengine ni mwanachama wa EALA Oburu Oginga, mbunge wa Wajir Fatuma Gedi na kamishina wa NGEC Priscilla Nyokabi.

Kupitia kwenye mitando ya kijamii ya twitter Raila alikuwa na haya ya kusema siku hiyo.

“Happy birthday kwa mke wangi Ida muhimu na uchambuzi wa urahisi, mtangulizi wa furaha na nguvu kwa familia yetu kutoka mara ya kwanza nilipokuona maisha yangu yalibadilika

EgGZKFOXoAE7R0B

Tunashukuru kwa ajili ya nguvu yako, Mungu aendelee kulinda na kubariki maisha yako.”Raila Aliandika.

Sherehe ilifanyika nyumbani kwao Karen. Hizi hapa baadhi yya picha za sherehe hiyo;

EgGZKFPX0AM76Ur

EgGZk6DXkAEsqY6

FB_IMG_1598245335971

FB_IMG_1598245333050

FB_IMG_1598245329945

FB_IMG_1598245326519

FB_IMG_1598245323572


Polisi wanatumiwa kuwanyanyasa na kuwatishia maseneta-William Ruto

Naibu Rais William Ruto ameunga mkono hatua ya kuunda kamati ya seneti ili kusuluhisha mjadala wa ugavi wa fedha ambao unaonekana kukumbwa na utata si haba.

Ruto alisema itakuwa jukumu la kamati hiyo kutumia busara ya hali ya juu katika kuamua njia mwafaka itakayotumika baada ya maseneta kufeli kuafikiana katika vikao walivyofanya mara tisa.

Wakati uo huo alikashifu vikali dhuluma dhidi ya viongozi wenye maoni kinzani akisema kuwa wananchi hawakuipigia kura serikali ya Jubilee ili kunyanyaswa.

Ruto

“Hatua ya kuwatishia wananchi, kuwanyanyasa na kuwadhulumu viongozi ni makosa, na hiyo sio sababu iliyowafanya mamilioni ya wananchi kurauka kutupigia kura.” Ruto Alisema.

Watatu hao walikamatwa wakiwa maeneo tofauti kaunti za Nairobi na Kajiado katika njia isiyoeleweka. Watatu hao walikuwa miongoni mwa viongozi waliopinga pendekezo la serikali kwamba fedha za baadhi za kaunti zipunguzwe.

Aidha kinara wa Upinzani Raila Odinga pia alikashifu kukamatwa kwa maseneta hao na kudokeza kwamba hatua hiyo ilidhihirisha Kenya ingali katika enzi za ukoloni.

Raila Odinga
Raila Odinga

“Kukamatwa kwa maseneta hao jana, kama vile mzozo wa kuhusu mswada wa ugavi mapato, ni dhihirisho kuwa hatujaafikia demokrasia.”