Eric Omondi alinipa shavu kimuziki, Bahati hakuweza- Madini Classic

Staa wa muziki nchini Madini Classic amefunguka katika kikao cha Papa Na Mastaa kuwa mchekeshaji Eric Omondi alikuwa wa kwanza kumshika mkono na kumpa moyo wa kufanya muziki. Muimbaji huyu alimtaja Eric kama nguzo muhimu katika maisha yake ya sanaa. Madini Classic aliirithi jina lake kutoka kwa babu yake ambaye alikuwa mchimbaji migodi katika kitongojiduni cha Migori.

 

Soma hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Madini alimueleza Papa mwanzo mwisho jinsi alivyotoka kijijini na kuja Nairobi kujituma kwenye haso zake za kimziki.

“Kipindi natoka nyumbani kweli sikuwa na muziki. Nimekuja kuimba nikiwa hapa Nairobi . Muziki ulionitambulisha kwenye mainstream media unaitwa Nikaribishe. Kikawaida safari ya muziki huwa ndefu sana. Sio kitu unaweza ukabumburuka na ghafla utusue.” alisema Madini.

Madini aliweza kueleza ukaribu wake na Eric Omondi na jinsi alivyomhimiza afanye muziki mkubwa.

“Eric Omondi ni mtu na ambaye anapendana sana kipaji changu. Alimuuliza Bahati huyu Madini ni nani. Bahati akamwambia kuwa mimi ni rafiki yake. So akamwambia mbona usisaidie huyu jamaa atoke kimuziki kwa sababu bahati alikuwa ashatoka na akawa mkubwa lakini inaonekana mikakati za Bahati na shughuli zikawa nyingi mpaka akasahau.” Madini alimueleza Papa.

Pata uhondo hapa:

 

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Madini alisema kuwa anatamani sana angefanya muziki na mastaa kama Sauti Sol, Alikiba na Diamond Platnumz. Kupitia kuwashirikisha kwenye ngoma, staa huyu alisema anaweza jifunza mengi kimuziki.

 

 

 

Seru: Nazizi tumeongea na yeye kufanya kazi

Ni ndoto ya kila msanii kuona anapevuka kisanaa na muziki wake kukua. Msanii Chipukizi yeyote huwa na maazimio ya kufanya muziki utusue na kufikia mashabiki wake. Hali kadhalika hutaka sana kufanya nyimbo na kuwashirikisha mastaa wakubwa ili muziki wake unawiri.

Seru haachwi nyuma katika jitihada za kuhakikisha muziki wake unapevuka huku akiwaangalia mastaa wa hapa nchini kama Wyre na Nazizi. Mkali huyu wa nyimbo inayofanya vizuri ya Freedom anajivunia kufanya muziki wa Reggae kwa lugha ya Kiswahili tofauti na wasanii wenzake na kumfanya tofauti katika tasnia.

Msanii chipukizi Jah Ises Seru amefunguka kuwa yupo katika mazungumzo na staa wa reggae Nazizi katika kipindi cha Papa Na Mastaa. Seru alifungukia Papa kuwa angependa kuingia studioni na kufanya nyimbo hatari na mkali huyu wa reggae.

Soma hapa:

Morgan Heritage wajenge studio moja hapa nchini – Jah Ises Seru asema

“Kama Nazizi tumeongea na yeye kufanya kazi. Wasanii kama Wyre ningetamani kufanya nyimbo nao na naamini siku itakapotimia utaiskia.” Seru alimueleza Papa.

Pata uhondo kamili:

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Jah Ises katika kikao hiki amesimulia kuwa kando na muziki anafanya kazi tofauti kama uchoraji na kuchonga sanamu.

“Kuna ukurasa katika mtandao wa Facebook nimefungua wa kuchapisha kazi zangi za sanaa inayofahamika kama Seru Arts. Kuna kazi nimefanya  jiji la Nairobi karibu na round about ya parliament.”

 

Morgan Heritage wajenge studio moja hapa nchini – Jah Ises Seru asema

Wasanii wapo wanaofanya Reggae nchini ila katika kikao cha Papa Na Mastaa kukaja msanii chipukizi anayefanya mtindo huu wa muziki wa lugha ya Swahili.

Jah Ises Seru alifika katika kipindi hiki na kueleza Papa mwanzo mwisho jinsi anavyoutegemea muziki kujisetiri kimaisha.

Akieleza kuwa alianza muziki katika umri mdogo kanisani kwao, chipukizi huyu anafunguka sababu za kufanya mtindo huu wa nyimbo.

Soma uhondo hapa:

Gabu amsifia msanii Diamond Platnumz

“Okay muziki nilianza kitambo nikiwa mdogo nikiwa kwenye kwaya za kanisa. Nilipenda reggae kwa sababu ya ujumbe  wake. Muziki huu unaongea kuhusu jamii.”

Msanii chipukizi na mwimbaji wa muziki wa Reggae amewaomba wanasanii kwenye kikundi cha Morgan Heritage kusaidia kukuza talanta nchini.

“Morgan Heritage wajenge studio moja hapa nchini kuwasaidia wasanii wachanga kama sisi.” alisema Seru.

Soma hapa :

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Tofauti na wasanii wengine wanaofanya Reggae kwa kizungu, Seru anaufanya muziki huu kwa Swahili. Alieleza Papa sababu za kufanya hivi

“You know Kiswahili kitukuzwe. Naamini watu wengi hupata ninachokiimba nikifanya kwa lugha ya Kiswahili.”

Seru yupo na albamu moja ambayo ndani yake kuna nyimbo 12 moja ikifahamika kama Freedom na anapania kufanya nyimbo zingine katika albamu inayofuta itakayofahamika kama One Chance ambayo itakuwa na nyimbo 8.

“Niko na nyimbo kibao kwa sasa katika album ambayo iko na 12 tracks. Ninafanya album karibu kutoka itakuwa na nyimbo nane”

 

 

Gabu amsifia msanii Diamond Platnumz

Msanii mkubwa Afrika mashariki Gabu almaarufu kama Bugubugu alipata nafasi na kufika kwenye kikao cha Papa Na Mastaa kinachoruka kupitia mtandao wa youtube wa Redio Jambo.

Kikao hiki huongozwa na mtangazaji Rais Papa  na huwa ni kitengo maridhawa cha mazungumzo na mastaa wakubwa nchini.

Gabu ameweza kuzungumzia nyimbo yake na msanii Mbosso kutoka lebo ya WCB huku akimsifia msanii nguli Afrika na mmiliki wa Wasafi FM na Wasafi TV Diamond Platnumz.

“He’s a good businessman. Very sharp. Anajua chenye anafanya.”

Soma habari kemkem:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Staa Gabu ameweza kuzungumzia nyimbo inayotamba kwa sasa Koroga na sababu kubwa za kuichapisha katika mtandao wa Vevo.

“Vevo inalipa vizuri. Vevo ni ya mastaa. Na pia watu wengi wanatoka Youtube na kwenda kwa Vevo. Halafu ina rangi nzuri katika TV yako nyumbani. Nimependa tu vevo.”

Katika nyimbo hii inayofanya vizuri katika mtandao huo, Gabu alifunguka jinsi walivyoshirikiana na staa kutoka Uganda Addy Andre na Arrowboy.

Soma hadithi hapa:

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

“Niliita Arrowboy akakuja kwa studio nikampatia collabo nikamwita Addy andre kutoka Uganda ni producer na bado mi msanii amefanyia Jose Chameleone kwa hivyo akakuja Kenya tukafanya muziki. Tukasafiri Tanzania tukafanya video na Kenny kwa siku 3.  Kenny anafanya na Zoom Production Wasafi alafu video ikatoka.”

Mkali huyu wa Koroga pia alizungumzia kuhusu collabo yake na Mbosso kutoka lebo ya WCB, Mastory huku akionekana kubana kiwango cha hela alichomlipa.

Soma mengine hapa:

“Simama wakuone kijana mfupi round” – Mbusii amuita Uche

“Mambo ya hela sitataja. Chenye nitakwambia ni tuliclick vizuri mambo yakawa sawa ile siku alikuwa amekuja Nairobi. Tukaclick vizuri alikuja kwa studio yangu Kompakt Records tukarekodia audio hapo alafu tukaenda Tanzania kushoot video. Tuko na uhusiano kati ya Kompakt na Wasafi.”

Hali kadhalika Gabu alimzungumzia msanii Kristoff na jinsi anavyomwona kisanii

“Kristoff tumetoana mbali nimeweza kum_advise hapa na pale. Na Kristoff sasa ni one of the biggest artistes hapa Kenya. Sisi ni marafiki tu, family friends na business men.

Soma hapa:

Musician Vivian opens up on being in an abusive relationship

Msanii huyu alieleza kimya cha kundi la Punit ambayo wengi wamekuwa wakihisi kuwa kuna ubaridi ambao ni dalili ya kuvunjika kwa kikundi hiki.

“Timu tupo lakini tuko na bigger fish to fry. Mimi niko na studio yangu hapo nmeshikana na Steve Ongechi. Boneye na studio yake pale Decimal Records ameshikana na Musyoka. Frasha alikuwa ndani ya Pacho. Idea yetu ni kushikilia industry in various ways but tunakuja pamoja tunafanya kama Punit na kila mtu ni brand kivyake.”

Gabu amesema kuwa yupo na mpango imara wa kuhakikisha kuwa anawasaidia wasanii chipukizi kupitia studio yake

“Kwa studio kuna wasanii tunawabring up hapo Kompakt Records  in the few months hivi mtakuwa mnawaskia. Kuna nyimbo ya kimataifa nafuatilia ila chenye nafuatilia sai ni my new artiste anatoa ngoma”.

Soma hapa:

Gidi amkosoa rapa Khaligraph Jones

 

“Simama wakuone kijana mfupi round” – Mbusii amuita Uche

Katika shoo ya Papa Na Mastaa, Mbusi alifunguka kuhusu anavyofanya kazi na deejay wake Uche Adi Rasta. Uche ni kati ya madeejay wanaofanya na mtangazaji huyu katika shoo ya Mbusi Na Lion TekeTeke katika kituo cha Redio Jambo kuanzia saa tisa hadi saa moja jioni.

Katika mahojiano hayo ambayo hufanyika kwa mastaa wanaofanya sanaa nchini, Mbusi alimwambia Uche asimame aonekane na watazamaji.

“Simama wakuone kijana mfupi round. Uche namchukulia kama small brother.” alisema Mbusii

radiojambodj

Soma hapa:

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Uche pia alielezea anavyomfahamu bosi wake na kusema kuwa ni mtangazaji ambaye inakuwa rahisi kufanya kazi naye huku akisimulia kuwa hawajahi kuwa katika matatizo katika kazi zao.

“Mbusi ni mtu ambaye mwenye heshima. Anakubali chochote unamwambia.” alisema Uche.

Mbusi alieleza jinsi yupo katika mstari wa kwanza kuunga mkono muziki wa hapa nchini ili kuwainua wasanii.

mbusihnaliondehplayful

“Mbusi Na Lion TekeTeke supporting local content.”

Mbusi alionekana pia kuwakanya mabinti wanamitindo na kusema kuwa waende polepole katika kazi zao huku akisisitiza kuwa hawezi kuwabania katika mahusiano.

“Na hao unawaita watoto waambie waende polepole tafadhali.”

 

Soma hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Katika kikao cha Papa Na Mastaa wiki hii ilikuwa zamu ya mtangazaji Mbusii kufika na kujumuika katika shoo yake Rais Papa inayoruka kupitia mtandao wa Youtube wa Radio Jambo.

Papa hutumia fursa hii kuhoji mastaa kuhusu maisha yao ya muziki, mahusiano na mitindo. Mbusii ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Mbusii Na lion TekeTeke, alisimulia mwanzo mwisho kuhusu alivyoanzia utangazaji katika kituo cha utangazaji cha Ghetto.

Soma hapa mengine :

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

“Nilifanya miaka miwili kama office messenger na miaka tatu katika utangazaji.”

Mbusii alielezea Papa jinsi alivyokuwa muigizaji wa vitabu vya riwaya vya shule ya upili na baadaye kupata kazi katika Radio Jambo kituo kinachoendeshwa chini ya mwavuli wa kampuni ya Radio Africa Media Group.

Staa Mbusii ni miongoni mwa watangazaji hapa nchini ambao wamewekeza kwa kiwango kikubwa katika tasnia ya burudani kwa kuanzisha kampuni inayofahamika kama Hakuna Mbrrcha Entertainment. 

Katika kampuni hii, Mbusii ameweza kuajiri vijana wengi wakihudumu kama madeejay, wasanii wa kurekodi miziki kati ya maswala mengine tofauti.

Soma hapa:

Mercy Masika speaks about how song, ‘Mwema’ changed her life

Kuhusu mahusiano Mbusi alisema kuwa ingawaje ana mke na watoto hawezi kuwafungia nje mabinti warembo katika mahusiano.

“Watoto wa kike hiyo ni kiumombasani…nikiingia Mombasani nione Fatuma unadhani nitawabania kweli? Siwezi wabania lakini nikona bibi na watoto.”

Tazama mahojiano yetu naye.

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Msanii na rapa mkubwa Afrika mashariki King Kaka amefunguka sana kuhusu kufanya muziki na aliyekuwa mpenzi wake Sage.

Katika mahojiano na mtangazaji Rais Papa katika kipindi kinachoruka katika mtandao wa youtube ya Redio Jambo, mkali huyu ameweza kusema kuwa hana matatizo na mzazi mwenzake baada ya wao kutengana huku akisema nafasi ikitokea wanaweza ingia studio na kufanya ngoma.

“Tukikutana studio tunaweza fanya ngoma. Muziki inafanywa tu si ni muziki.” Alisema King Kaka.

Soma mengine:

Musician Vivian opens up on being in an abusive relationship

Papa Na Mastaa ni kipindi na ambacho kimetengwa kwa mahojiano ya kipekee na mastaa wa muziki, mkali huyu ambaye ni mjasiriamali, rapa na mwimbaji pia ameanzisha juhudi za kuwasaidia wasanii chipukizi inayofahamika kama Empires Gold na tayari wasanii watatu wapo katika mpango huo.

King Kaka pia ameweza kuweka wazi sababu iliyomfanya yeye kuacha kufunza masomo ya biashara katika chuo kikuu cha Zetech. Staa huyu aliweka pembeni kazi hii kwa misingi ya kazi nyingi zinazomwandama.

“Nilikuwa mhadhiri Zetech University. Nilikuwa nafunza business na kwa vile schedule yangu ilikuwa tight nkaacha. For almost 2 years sifunzi.”

Mkali huyu aliweza pia kuzungumzia safari yake ya Marekani inayofahamika kama Eastlando Royalty US Tour. Ziara hii ya marekani iliweza kumfanya aingie studio na kumshirikisha msanii wa kimataifa Cassidy katika nyimbo inayofanya vyema ya Far Away.

“The fact that nikona Cassidy kwa ngoma ni ushindi ukubwa,” King Kaka alieleza katika kikao cha Papa Na Mastaa.

Pata uhondo hapa:

My hubby pinned me down and shaved my hair – Cries Woman

Audio ya nyimbo hii ilifanywa hapa nchini na Musyoka na video ikihaririwa na mkenya anayeishi Marekani, Hussein Njoroge.

King Kaka alifunguka zaidi kuhusu mahusiano yake na msanii Sage na jinsi anavyotenga wakati kuongea na watoto.

“I think you’re talking about sage yeye akona my other daughter. Lazima niende kumwona mtoto wangu ambaye ni Ayana lakini naishi na Nana. You’ve to create time for your kid.”

King Kaka hali kadhalika alisema kuwa yupo freshi na Msanii Khaligraph na kumsifia sana.

“Ni jamaa anafanya vizuri tunashukuru mungu. Tukiona vijana wanatia bidii tunafurahia. Anatia bidii kwa kazi zake. Tunaongeaongea ikifika time tutaingia studio.”

Soma hapa:

‘Kijana fupi amenona..’ Compilation of the best quotes by lonyang’apuo