(+ JUMBE) Rayvanny atemwa na mkewe, jumbe zavujishwa Insta

Staa wa ngoma ya Tetema kwa sasa anazongwa fikra baada ya kutemwa na mkewe Fahy Vanny.

Kwa mujibu wa posti aliyoichapisha Insta, jumbe za mkewe za kutotaka tena mahusiano ni ishara tosha kuwa ndoa yao imeingia shubiri.

Fahy Vanny anasema kuwa maisha ya ndoa na RayVanny yamemfika mwisho.

(+ Video) Mama akatisha hotuba ya William Samoei Ruto, asimulia masaibu

Katika ujumbe uliojaa machungu,mkewe anampa msomo Rayvanny kumkoma na kumsahau mtoto wao Jaydan.

Screenshot from 2019-11-25 16:49:02

“Hesabu mimi na Jay amefariki kwenye maisha yako. Nitapigana na nitashinda. Sitakosa pesa ya kula. Ila mimi na Jay hesabu kuwa tumekufa kwenye maisha yako,” aliandika Fahy katika mtandao wa Insta.

Rayvanny alimjibu kuwa mkewe amekuwa akitamani maisha yasiyo na tija yoyote.

Huku akionyesha ishara ya kukubali matokeo, staa huyu alimtakia mkewe mema na kudokeza kuwa bado anaipenda familia yae.

Magix Enga ataja sababu ya kumsamehe Harmonize, aachilia UNO YouTube

“Nimekuwa Nakuheshimu miaka tuliokuwa pamoja. Kuna mengi tumekoseana na tumesameheana na kila mara umekuwa ukitamani maisha ambayo kila siku nakwambia hayatakusaidia,”

“Nakuheshimu na naiheshimu sana familia yangu. Ikiwa umeamua mwenyewe kuondoka, siwezi kulaumu. Bado napenda familia yangu. Nakutakia Maisha Mema,” aliandika Rayvanny.

 

“Yaani Tanzania tumesha wai kabisa,” Willy Paul

Staa wa muziki wa injili nchini Willy Paul ametangaza kuwa sasa ameiteka soko la muziki la nchi jirani ya Tanzania. Kupitia nyimbo alizowashirikisha wasanii Nandy na mkali Rayvany kutoka lebo ya WCB inayomilikiwa na staa mkubwa afrika Diamond Platnumz, sanaa yake imepenyeza kwa urahisi na kueleweka freshi na watanzania.

Tazama nyimbo yake hapa na Rayvanny;

Kwa utafsiri wa haraka, michambo ya wakenya katika mitandao ya kijamii huenda ilimpa nguvu staa huyu kuzidi kupambana na kujitafutia nafasi nzuri ya muziki afrika mashariki.

Pata uhondo hapa:

“Amekula matofali mbili na mimba ikona mwezi mmoja”- Mulamwah

Willy M Tuva katika kipande kifupi cha video alichokiposti Pozze anaonekana akimpa shavu kubwa katika shoo iliyofanyika Dar Tanzania.

Tazama hapa:

Willy Paul ni kati ya wasanii wanaopevuka kwa kasi nchini akiwemo staa wa kike Nadia Mukami, Masauti na kundi la muziki la Ochungulo. Wasanii wengi wamezungumza swala la pozze kuonekana kuasi dini na kufanya muziki wa kidunia.

Soma hapa:

Je, Willy Paul kamkosea mungu? Wakenya watoa maoni

“Willy paul kama anataka kufanya muziki wa kidunia yupo huru. Ni uamuzi wake.” alisema HopeKid.

Staa wa muziki kutoka nchi ya Jamaica Alaine alimtetea Willy paul juzi kati kipindi na ambapo wakenya walikuwa  wanatokwa na povu katika mitandao ya kijamii kumhusu msanii huyu wa injili kuwa na tabia na mienendo inayokinzana na neno la mungu.

“Watu wamkosoe Willy paul kwa upole na kwa upendo. Jamani tusimkosoe kwa chuki na kwa ukali.” alisema Alaine.

Diamond Platnumz na babake wakutana na kuzima tofauti zao

Msanii na staa mkubwa Afrika Diamond Platinumz ameweza kukutana katika redio ya Wasafi FM na babake na kuonekana kuzima tofauti zao za awali.

Mzee Abdul alimtaliki mkewe miaka ya awali kijana huyu akiwa kidato cha kwanza. Naseeb alitangulia kwa kusema kuwa ubaridi unaonekana kati yao na baba mzazi umechochewa na kutokua pamoja kwa kipindi kirefu.

“Kiukweli siwezi kusema nina ukaribu na mzee. Hatujakuwa na bond kubwa naye ila mimi sina matatizo naye…tukiwa kuna issue tutakutana naye tuongee” Diamond alisema katika mahojiano.

diamodn and his parents
Diamond Platnumz na wazazi

Ukaribu wa Naseeb na mamake umeonekana kwa muda mrefu kunoga huku babake akionekana kusahaulika na msanii huyu.

Katika kitengo cha Block 89 cha shoo ya redio ya Wasafi, babake Platnumz anaonekana kutokea ghafla katika mahojiano  ya mtoto wake na kituo hiki.

Mwanae anamiliki chumba hiki cha habari pamoja na runinga bila kusahau lebo ya Wasafi (WCB)  inayojivunia kusimamia wasanii wakubwa Afrika mashariki na Afrika ya kati kama Rayvany,  Harmonize, Lavalava, Mbosso na Queen Darleen.

Baada ya kuugua kwa muda mrefu, babake Chibu alipata ufadhili kutoka kwa mtendawema aliyeguswa na hali yake ya ugonjwa.

diamondplatnumzinyellow
Diamond

Yule sio mtoto wangu kunizaa ila niseme kuna watu hawana wazazi na wana hela.Aliniangalia katika mitandao ya kijamii katika hali sio nzuri na akatokea kutoa usaidizi”

Diamond anadai kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinamtumia babake kupata ufuasi mkubwa wanapokwenda kumhoji kuhusu tofauti zao.

“Naamini vyombo vya habari vinakuzakuza na kutengeneza matatizo kati yangu na baba.”

diamond platnumz madale
Bongo singer Diamond Platnumz

Kwa upande mwingine anaona kuwa babake anamweka katika kicheko kwa watu wengi hususan wapinzani wake anapoonekana kama hamsaidii mzazi.

Babake alimwomba msamaha na wote kuonekana wameridhiana katika mazungumzo yao

Kama nimekukosea naomba unisamehe na ujaribu kuangalia utanisaidia vipi mimi babako.”

Diamond alionya kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vinavyomtumia babake kwa maslahi yao na hawamsaidii. Mkali huyu wa kibao kipya The one  alimaliza kwa kuomba msamaha.

“Well mimi siwezi kusema nina  matatizo na babangu. Naamini utofauti wake na mama unafanya tuwe hatuna ukaribu…Naomba anisamehe pia kwa sababu sijui akiwa na mama walikosana kwa misingi gani.”

Also read more here