Ratiba ya miji atakayozuru sonko wa masonko wiki hii. Mji wako ni upi?

Ratiba kamili ya miji atakayotembelea sonko wa masonko wa Redio Jambo imewekwa wazi kama mlango wa kanisa ili mashabiki wajue kwa kiuhalisia wanapaswa wamsubiri maeneo gani na wakati upi katika wiki hii.

Leo jumatatu sonko ashamwaga hela lukuki tayari katika kaunti ya Kiambu na kuzamia kaunti ya Nyeri. Kupitia swali mboga sana la kuitambua “The Phrase That Pays”, msikilizaji anatuzwa shilingi elfu moja.
Kwa kutengeneza bango na kuandika Redio Jambo Ongea Usikike, mshindi anatuzwa elfu 5 pesa taslimu.

Soma hapa pia:

Dah! Mapokezi makubwa Kiambu. Sonko wa masonko amwaga pesa kibao

Kesho sonko huyu ataanza ziara yake mji wa Nyeri na baadaye alasiri kukita kambi maeneo ya Mwea. Msururu huu wa kutembelea miji mbalimbali utafikia maeneo ya Kirinyaga , Embu ,Meru na hatimaye Murang’a ijumaa.

Pata uhondo:

Rais Kenyatta awaambia viongozi waige mfano wa marehemu Laboso

Sio mara ya kwanza kituo hiki kufika vijijini na mjini wanakosikiliza mashabiki wao. Nia na azma kuu ni kuwatuza mashabiki wake kwa kuwa balozi wazuri kokote nchini.

“Lets go Kenya…,” mtoto wa Gidi aishabikia timu ya raga ya kitaifa

Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Patanisho, Gidi Ogidi jana alichapisha kwenye mtandao wake maridhawa wa insta kipande cha video wakizungumza na mtoto wake Marie Rose kupitia mfumo wa mawasiliano wa Skype.

Soma hapa:

Harmonize awanunulia wazazi gari mpya

Katika video hiyo, Marie anamulezea babake jinsi alivyoshabikia timu ya kitaifa ya raga katika msururu wa mwisho wa michuano hiyo mwaka huu.

18424266_1660842310890804_1746066059842251100_n

Gidi husafiri mara kwa mara kuenda nchini Ufaransa kuwaona bibi yake Ziva Elijah na mtoto wake. Mtoto huyu alikuwa akiimba kwa furaha. Tazama hapa:

“Lets go Kenya, Lets go Kenya.”

Soma hapa:

“Huddah na Vera nawatamani…”, asema Willy Paul

Gidi anaendesha kipindi kikubwa na hapa nchini. Kulingana na utafiti wa kundi la  Geo Poll Survey, Kipindi cha hiki kinasikilizwa na idadi kubwa ya wakenya hivi kumweka Gidi na mwenzake Ghost katika ramani ya watangazaji nguli nchini.

18403735_1660842244224144_3414620974359658254_n

 

Eric Omondi alinipa shavu kimuziki, Bahati hakuweza- Madini Classic

Staa wa muziki nchini Madini Classic amefunguka katika kikao cha Papa Na Mastaa kuwa mchekeshaji Eric Omondi alikuwa wa kwanza kumshika mkono na kumpa moyo wa kufanya muziki. Muimbaji huyu alimtaja Eric kama nguzo muhimu katika maisha yake ya sanaa. Madini Classic aliirithi jina lake kutoka kwa babu yake ambaye alikuwa mchimbaji migodi katika kitongojiduni cha Migori.

 

Soma hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Madini alimueleza Papa mwanzo mwisho jinsi alivyotoka kijijini na kuja Nairobi kujituma kwenye haso zake za kimziki.

“Kipindi natoka nyumbani kweli sikuwa na muziki. Nimekuja kuimba nikiwa hapa Nairobi . Muziki ulionitambulisha kwenye mainstream media unaitwa Nikaribishe. Kikawaida safari ya muziki huwa ndefu sana. Sio kitu unaweza ukabumburuka na ghafla utusue.” alisema Madini.

Madini aliweza kueleza ukaribu wake na Eric Omondi na jinsi alivyomhimiza afanye muziki mkubwa.

“Eric Omondi ni mtu na ambaye anapendana sana kipaji changu. Alimuuliza Bahati huyu Madini ni nani. Bahati akamwambia kuwa mimi ni rafiki yake. So akamwambia mbona usisaidie huyu jamaa atoke kimuziki kwa sababu bahati alikuwa ashatoka na akawa mkubwa lakini inaonekana mikakati za Bahati na shughuli zikawa nyingi mpaka akasahau.” Madini alimueleza Papa.

Pata uhondo hapa:

 

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Madini alisema kuwa anatamani sana angefanya muziki na mastaa kama Sauti Sol, Alikiba na Diamond Platnumz. Kupitia kuwashirikisha kwenye ngoma, staa huyu alisema anaweza jifunza mengi kimuziki.

 

 

 

Massawe atarudi kuwapasha polisi Industrial

Baada ya ajali ya jumatano iliyofanyika kati ya gari ya staa wa redio Massawe na basi ya sacco ya Orokise, mtangazaji huyu ameapa kufika kituo cha polisi Industrial na kuwapasha.

Akizungumza jana katika kipindi anachopeperusha kuanzia saa nne hadi saa nane alasiri, mtangazaji huyu alionekana kutopendezwa na wanapolisi hao.

“Am still going for my abstract and I think I will give them peace of my mind.” afoka Massawe.

Soma hapa:

Baadhi ya maneno Massawe huyatumia hewani na maana yake

Massawe akionekana kukerwa na tabia ya wanapolisi hao, amefunguka walivyomnyamazisha na kumtaka asiongee. Alikuwa ameandamana na maafisa wa polisi hadi kituo hicho baada ya tukio hilo.

Massawe aligongwa na gari kutoka nyuma na kuvunja kioo cha gari lake. Kulingana naye gari hiyo ya sacco ya Orokise ndio walivunja sheria za barabarani.

“Unajua wakati mwingine unaweza ukawa careful barabarani lakini mwenzako hafuati sheria.”

Baada ya kupatikana na bima pana ya gari lake, afisa mmoja alimueleza kuwa asiwe na hofu.

Pata uhondo hapa:

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

“Madam insurance yako ni comprehensive wacha insurance isort.” amesema Massawe.

Hali kadhalika Massawe amedokeza alivyotaka kukimbia na kutoweka baada ya kisa hicho lakini msamaria mwema akamsihi asifanye hivyo.

“Nilitoka mbio. Nilikuwa nataka kutoroka. Msamaria mwema akaniambia nisifanye hivyo.”

Massawe ameongeza kusema kuwa wanapolisi hawafai kuwadhulumu wananchi na kuwa uwepo wao ni kuhakikisha usalama kwa watu wote.

 

Baadhi ya maneno Massawe huyatumia hewani na maana yake

Utangazaji wa redio ni mojawapo ya sanaa duniani zinazohitaji ubunifu mkubwa na ukakamavu wa kuwashika na kuwagandisha wasikilizaji katika spika za redio zao.

Sanaa yoyote lazima msanii achombeze maneno matamu yanayofanya kazi yake ionekane bora na ya kuvutia zaidi.

Soma hapa:

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

Mwimbaji wa nyimbo za mapenzi atapenda sana kuchonga mistari inayokwenda freshi na maudhui na lengo anayokusudia kwa mashabiki wa jinsia tofauti. Hali kadhalika anapofanya maonyesho jukwaani atakuwa na baadhi ya maneno kinywani ambayo wafuasi wake humtambua nayo.

Mtangazaji Massawe hajaachwa nyuma katika mtindo huu na kuna baadhi ya maneno anayoyatumia katika kipindi chake cha Bustani la massawe ili kuvutia mashabiki.

Pata uhondo hapa:

Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

Tumekusogezea hapa baadhi ya tungo virai (phrases) anazopenda kutumia:

  1. “Nafurahi kuwa tupo pamoja nawe”

Baada ya nyimbo inayocheza hewani kumalizika, mtangazaji huyu anapenda sana kuanza na maneno haya kama kitambulisho cha kufungua shoo.

     2. “Ngwenee”

Hili ni tamko ambalo lina asili ya lugha ya Kikamba na huwa na maana ya ‘Nakuona’. Kwa haraka haraka unaweza toa ubashiri wako na kusema kuwa Massawe husema hivi labda kwa sababu anatoka maeneo ya ukambani au labda ni mbinu ya kugeuza ndimi na kuwavuta wasikilizaji kutoka jamii hiyo.

    3 .” Uko hii town? Au niko hii town au labda hii ni town”

Massawe hutumia maneno haya mara kwa mara. Staa huyu huwa anataka kujua mashabiki wake wanategea kipindi wakiwa maeneo gani.

 

Soma pia:

‘Safiri salama dadangu’ Massawe Japanni mourns her best friend

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

Mtangazaji wa kipindi cha majira ya mchana – Bustani la Massawe  na kinachopeperushwa kuanzia saa nne hadi saa nane alasiri katika mawimbikasi ya Redio Jambo amechapisha ujumbe  kwa mashabiki wake katika mtandao  maridhawa wa Instagram.

Staa huyu amezamia insta story yake na kutoa ushauri wake kwa mashabiki wake kuwa wakae ange muda wowote wanaposafiri.

“Siku iliyoje! Ndo nafika chumbani baada ya kuhusika katika ajali ndogo ! Mafunzo nimeyasoma muda wowote chochote kinaweza kufanyika. Funga mkanda wa usalama kila wakati.”

 

 

massawe

Tumekusogezea hapa:

Massawe Japanni anusurika baada ya kuhusika katika ajali mbaya (PICHA)

Mtangazaji Massawe alipigwa na butwaa na kuingiwa na kibuhuti baada ya tukio la jana. Wasikilizaji walimkosa Jumatano ila leo (Alhamisi) yupo yupo kuwakonga nafsi wasikilizaji wake.

Zamia uhondo hapa:

Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

Kipindi chake huangazia sana matatizo yanakumba familia katika jamii hususan wanaume wanaopachika mabinti mimba na kuwazimia data ghafla. Massawe huwapigia simu na kuwasaidia kwa kuwaelekeza katika kituo cha kusaidia kina mama.

Jilie utamu hapa:

Video of the day: Massawe Japanni’s dancing skills are top notch!

 

“Simama wakuone kijana mfupi round” – Mbusii amuita Uche

Katika shoo ya Papa Na Mastaa, Mbusi alifunguka kuhusu anavyofanya kazi na deejay wake Uche Adi Rasta. Uche ni kati ya madeejay wanaofanya na mtangazaji huyu katika shoo ya Mbusi Na Lion TekeTeke katika kituo cha Redio Jambo kuanzia saa tisa hadi saa moja jioni.

Katika mahojiano hayo ambayo hufanyika kwa mastaa wanaofanya sanaa nchini, Mbusi alimwambia Uche asimame aonekane na watazamaji.

“Simama wakuone kijana mfupi round. Uche namchukulia kama small brother.” alisema Mbusii

radiojambodj

Soma hapa:

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Uche pia alielezea anavyomfahamu bosi wake na kusema kuwa ni mtangazaji ambaye inakuwa rahisi kufanya kazi naye huku akisimulia kuwa hawajahi kuwa katika matatizo katika kazi zao.

“Mbusi ni mtu ambaye mwenye heshima. Anakubali chochote unamwambia.” alisema Uche.

Mbusi alieleza jinsi yupo katika mstari wa kwanza kuunga mkono muziki wa hapa nchini ili kuwainua wasanii.

mbusihnaliondehplayful

“Mbusi Na Lion TekeTeke supporting local content.”

Mbusi alionekana pia kuwakanya mabinti wanamitindo na kusema kuwa waende polepole katika kazi zao huku akisisitiza kuwa hawezi kuwabania katika mahusiano.

“Na hao unawaita watoto waambie waende polepole tafadhali.”

 

Soma hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage