I’m Negative,’ Meneja wa Diamond afichua hana corona

Ni habari  njema kwa mashabiki wa meneja wa staa wa Bongo Diamond, Sallam SK Mendez baada ya jamaa huyo kutangaza kuwa amepata nafuu baada ya kuwa chini ya uangalizi kutokana na virusi vya Corona.

Sallam ambaye alionekana mchangamfu alipokuwa anatoa taarifa hiyo kwa wafuasi wake, alifichua kuwa amekuwa chini ya karantini kwa wiki mbili na sasa amepata nafuu.

Diamond Platnumz ajiweka katika ‘karantini’ baada ya maneja wake SK Mendez kupatwa na virusi vya Corona

sallam-696x696

AFTER 14 DAYS GOT TESTED TWICE AND BOTH RESULTS CAME BACK NEGATIVE AND NOW AM OUT OF ISOLATION CENTRE. THANKS TO ALLAH, THANKS TO DOCTORS, NURSES AND THE GOVERNMENT. Sallam Aliandika.

Sallam ndio mwathiriwa wa  pili wa  Tanzania kupona corona, katika posti zingine alimshukuru Mungu kwa kwa kupata nafuu.

“NIMSHUKURU ALLAH 🙏🏽 NA PIA NIWASHUKURU WOTE MLIONITUMIA MSG, COMMENTS, DM NA DUA ZENU. BILA KUWASAHAU TEMEKE ISOLATION CENTRE KWA KUWA BEGA NA BEGA PAMOJA NA MIE BILA KUNICHOKA PALE NILIPOKUWA NIMEZIDIWA, NA SHUKURANI ZANGU ZINGINE ZIENDE KWA MADAKTARI BINGWA KUJUA MAENDELEO YANGU MARA KWA MARA NA PIA SERIKALI YANGU NA VIONGOZI WAKE HUSIKA WIZARA NA MKOA WALIKUWA HAWANA UBAGUZI KUTUJULIA HALI NA KUTUPA MOYO NA KUTUPA MAHITAJI TUTAKAYO.” Aliandika.

Aliwapa wananchi na hata mashabiki wa ushauri .

“NAOMBA NIWAPE TAARIFA NDUGU YENU, KIJANA WENU NIMECHUKULIWA VIPIMO MARA MBILI NA NIMEKUTWA NEGATIVE NA KWA SASA NIPO HURU. ILA NAOMBA TUENDELEE KUJIKINGA NA KUFATA USHAURI WA VIONGOZI WETU NA KUACHA MAELEKEZO YA UTASHI YASIYOKUWA NA UHAKIKA. ALLAH IS GREAT 🙏🏽🙏🏽🙏🏽”

Lebo ya WCB kutumia uganga kuzuia mvua Dar Es Salaam, Babu Tale

 

Boss Tale amefungukia Bongo 5 kuwa wanafanya wawezalo ili kuzuia mvua isinyeshe.

WCB ina fiesta kubwa sana Dar Es Salaam ambayo itakuja mastaa kama Wizkid, Tiwa Savage kati ya wengineo.

‘Nikwambie hapa tulipo tunahangaika sana kupigia waganga simu.”

“Unawaza nani anakuzuilia mvua so tunatoka nje ya box…”

“Its normal we are African, ata wewe unafanya usininyoshee kidole…” Alisema Boss Tale.

Unajua yepi kumhusu mbunge mteule Imran Okoth? Soma hapa

Tale alikuwa anazungumzia harakati wanazofanya ili kuhakikisha fiesta ya Wasafi katika uwanja wa posta imekuwa shwari.

Aidha, Tale amefunguka jinsi muziki unavyolipa hela kibao huku akimtaja Diamond Platnumz kama mtu anayependa kuwekeza.

“Diamond anaweza kuwekeza hela kwa msanii bila kuogopa lolote …”

Tale ni mojawapo wa mameneja wa lebo ya WCB akiwemo Sallam SK na Mkubwa Fella.

Tale amesema kuwa anamwangalia Fella kama ndugu yake.

Ametaja mchango mkubwa zaidi wa Fella katika muziki wa Bongo Fleva.

Haya yanajiri huku Mondi akiangusha ngoma kubwa ya Baba Lao itakayokonga nafsi mashabiki wao fiesta la Kijitonyama.

Ngoma hii ilileta utata na kufanana na Soapy ya Naira ila S2Kizzy akaweka wazi.

(+Video ) Boni Khalwale shujaa wa kurusha mawe, achangamsha Twitter

Producer huyu wa mkwaju wa ‘Baba Lao’ ya Mondi ametokezea na kufunguka kuhusu midundo ya ‘Baba Lao’ na ‘Soapy’ ya Naira kufanana.

Akihojiwa na kituo cha Wasafi FM nchini Tanzania, S2Kizzy amesema kuwa waliomba ruksa ya kuimba na mdundo huo.

Producer huyu ameeleza kuwa alivutiwa zaidi na mdundo wa Naira katika ngoma ya Soapy.