Viongozi wa Pokot wapinga hatua ya serikali kufunga shule

Viongozi kutoka Pokot magharibi wamepinga hatua ya serikali kuu ya kufungwa kwa shule zisizo salama kwa kuwa na miundo mbinu.

Akizungumza na gazeti la The Star, Samuel Phogisio ambaye ni seneta katika kaunti hiyo alisema kuwa hatua hiyo itazuia watoto wengi kupata elimu. Alitaka serikali kutenga kando fedha ili kuboresha miundo mbinu za shule hizo.

Aliyepata alama 428 KCPE afanya kazi ya ‘walking scarecrow’ kwa shamba ya ngano

Aidha aliongeza kuwa shule za umma zinasimamiwa na serikali ya kitaifa na hivyo basi ni jukumu lao kuhakikisha kuwa shule hizo ziko katika viwango vinavyotakikana kuwa.

Phogisio alitaka serikali iongeze mgao wa fedha wa kujenga shule katika kaunti mbali mbali ili watoto wapate elimu kwa mazingira yaliyo bora.

Vile vile seneta huyo aliwaomba wale wanaoweza kujitolea kufadhili kutengenezea miundo mbinu ya shule hizo wajitokeze kwa wingi ili watoto katika kaunti hiyo wazidi kupata elimu bora.

Phogisio alisema kuwa katika kaunti hiyo wanafunzi wengi hawajui kusoma na kuandika hivo basi shule zikifungwa hali hiyo itazidi kuwa duni.

Wanaume waongoza kwa idadi ya vifo kupitia ajali za barabarani