Proverbs 14:3: Aya ya bibilia ambayo Saphan alimtaka Eunice asome

Leo katika kitengo cha patanisho, Gidi na Ghost walikuwa na kibarua kigumu walipojaribu kuwapatanisha, Saphan na bi Eunice.

Kulingana na Saphan, mpenziwe wa miaka mitatu aliondoka kwa nyumbani baada ya kuzomewa na babake Saphan wakti ambapo alikosa kurudi nyumbani.

Kulingana na Eunice, babake Saphan hakutaka alale nje ya nyumba yake na wakti aliporudi alimfurusha kwa boma lake baada ya kumpa nauli.

PATANISHO: Hata akini block sitamsahau kwani nampenda – Saphan

Alimlaumu Saphan kwa kutomtetea mbele ya babake na alipopigiwa simu aliapa kutorudi nyumbani huku akimrai Saphan aendelee na maisha yake.

Kwa upande wake, Saphan hakuamini alichoskia na kusononeka. Aliapa kutomsahau mpenziwe hata kama itamchukua miaka kumi.

Wakti alipojua kuwa maji yamezidi unga alimuacha Eunice na aya mbili za biblia ambazo angependa azisome.

Hata hivyo aya iliyowafurahisha Gidi na Ghost ilikuwa ya mithali 14 mstari wa 3.

Aya hiyo inasema;

3. The proud speech of a fool brings a rod to his back, but the lips of the wise protect them.

Kiswahili:

Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi

 

Je wadhani baada ya kusoma mithali hii Eunice atamrudia Saphan?

PATANISHO: Hata akini block sitamsahau kwani nampenda – Saphan

Saphan, 31, kutoka Utawala alituma ujumbe akidai kuwa angependa kupatanishwa na mkewe bi Eunice, 24,  na kusema kuwa shida ni kuwa siku moja alimuachilia akatembee na kurudi nyumbani akiwa amechelewa, ambalo halikufurahisha wazazi wake.

Anasema mkewe aliondoka na kwenda Kisumu ambapo sasa anaishi na dadake.

Ataponea? Mo Farah atuhumiwa upya na swala la madawa ya kusisimua misuli

“Nampenda sana na sitaki kumuachilia hivyo. Wakati wa holiday alisema anataka kwenda kumuona dadake na badala ya kurudi siku hiyo akarudi siku iliyofuata jioni jambo ambalo halikumfurahisha babangu.” Alisimulia Saphan.

Alikasirika na kuondoka na kwenda kwa dadake, sasa hivi najaribu kumpigia lakini ameni block pia kwa Whatsapp. Niko tayari kumpokea na tuishi kwa maisha yetu mazuri.” Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na bado hawajajaliwa na watoto.

“Mwambie awe mwanaume awache mambo ya kuskiza wazazi wake, wakati nilikuwa nafukuzwa alikuwa hapo mbona alikuwa amesimama tu hapo?.” Aliuliza Eunice.

‘Niliacha ukahaba baada ya babangu kuja lodging’

Eunice aliongeza,

Mume wangu nilimwambia naondoka na nitalala kwa dadangu na babake ndiye aliniuliza kwenye niliko na kuuliza mbona nimelala nje. Isitoshe aliniambia narandaranda nje na niliporudi akaniamrisha nifunge virago niondoke.”

Kwa upande wake, Saphan anasema kuwa mkewe alimrushia maneno kwa gate na kumuamrisha asimtete mbele ya wazazi wake.

“Sirudi! Nishaamua, yeye aishi maisha yake na wazazi wake!”