Senate yapiga marufuku mikutano ya kamati kuzuia maambukizi ya Covid 19

Hakuna seneta atakayekubaliwa kwenda bungeni kwa mikutao ya kamati ya senate kuanzia wiki ijayo kama njia moja ya kuzuia usambaaji wa virusi vya corona .

Tangazo hilo linajiri siku  chache tu baada ya bunge la taifa kupunguza shughuli zake kwa hofu ya wafanyikazi na wbaunge kuambukizwa ugonjwa huo. Spika wa senate Ken Lusaka  amesema mikutano yote inayowalazimu maseneta kukutana ana kwa ana imefutiliwa mbal kwa mwezi mmoja ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo .

Tanzia:Mhadhiri wa UoN Ken Ouko afariki dunia kwa ajili ya Covid 19

Spika  amesema hali itatathminiwa baada  ya mwezi mmoja  na kamati ya senate kuhusu uhasibu ndio inayoweza kuandaa mikutano  kila baada ya muda Fulani  inapohitajika .

Wiki jana spika wa bunge la taifa Justin Muturi alipiga marufuku mikutano yote ya kamati na kushauri dhidi ya mikutano yote ya ana kwa ana katika majengo ya bunge . Agizo hilo lilitolewa baada ya kuibuka ripoti kwamba huenda wabunge kadhaa na wafanyikazi wa bunge wameambukizwa ugonjwa wa corona .

Jumanne iliyopita  kiongozi wa wachache bungeni John Mbadi alifichua kwamba wafanyikazi 36 wa bunge wamepatikana na Covid 19

 

 

Maseneta wakosa kukubaliana kuhusu ugavi wa pesa

Pendekezo la kutaka  mfumo wa tatu wa kugawa pesa kwa kaunti kuahirishwa  kwa miaka miwili limekataliwa na maseneta  katika kura iliyopigwa siku ya Jumanne.

Ugatuzi unaporomoka magavana waonya huku ukosefu wa pesa ukizua mgogoro

Hatua hiyo imejiri huku seneta wa Siaya James Orengo akimshtumu rais kwa ‘kutoweza kufikiwa ‘ kwa urahisi ili kuweza kushughulikia utata huo ambao umezua mgawanyiko katika seneti.

Ripoti hiyo ya kamati ya fedha na  bajeti  ilikuwa imeunga mkono mapendekezo ya tume ya ugavi wa mapato CRA   ambayo yangezifanya kaunti zenye idadi ya juu ya watu kupata mgao mkubwa na zenye idadi ndogo ya watu kupata kiasi kidogo  yalitaka mfumo huo kuanza kutekelezwa katika mwaka wa kifedha wa 2021/2022.

Hata hivyo  mapendekezo hayo ya seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata yalikataliwa na maseneta wenzake waliopiga kura kupinga hatua hiyo.

Jaribio hilo la senate siku ya Jumanne lilikuwa la sita kwa masenate kujaribu kupitisha mfumo huo mpya kuhusu jinsi pesa za kaunti zitakavyogawanywa.

Raila awataka maseneta kuunga mkono mfumo wa CRA wa ugavi wa mapato

Maseneta walionekana kuunda mirengo yao ndani ya unge ili kukaidi ushauri wa viongozi  wa vyama  vyao rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga waliotaka mfumo huo kupitishwa.

Hakuna pesa! Lusaka aahirisha vikao maalum vya kujadili ugavi wa pesa kwa kaunti

Maseneta walimfokea spika wa senate Ken Lusaka  baada ya Lusaka kuahirisha kikao maalum kilichofaa kujadili mfumo utakaotumiwa kugawa pesa kwa kaunti zote 47.

Ni mara ya nne kwa spika kuahirisha mjadala kuhusu suala hilo   baada ya kundi aliloliteua kupata mwafaka kukosa  kukubaliana.

Papa Shirandula alikuwa akinisaidia kusuluhisha migogoro na mke wangu asema Njoro

Kila kambi imekuwa  na msimamo mkali na kuzuia uwezekano wa kuafikia  mfumo wa pamoja unaoweza kutumiwa kugawa raslimali kwa kaunti  kwani wale ambao kaunti zao zingepata mgao wa juu wameutetea vikali mfumo mpya ilhali  wale kutoka kaunti zilizotengwa wanataka hali ya sasa isalie .

Chini ya mfumo uliopendekezwa  kaunti za  Garissa, Wajir, Marsabit, Isiolo, Samburu, Turkana, Tana River, West Pokot, Lamu  na  Mandera  zitapokea jumla  ya shilingi bilioniu 17.

Mudavadi ataka mikutano yote ya kisiasa kupigwa marufuku

Wajir  itapoteza  shilingi bilioni 2  billion, Marsabit  na Mandera  bilioni 1.9  kila moja ilhali  Garissa  itasalimisha  shilingi bilioni  1.6 billion  nayo Tana River  itapoteza Sh1.5 billion.

Uasin Gishu, Nakuru, Kiambu, Nandi  na Kakamega c zitapata mgao wa juu .

 

 

Kasuku nje ndani kimya: Sudi, Wako hakusema neno hata moja bungeni mwaka wa 2019 – Mzalendo

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi  hakusema lolote   bungeni mwaka wa 2019,  imeonyesha  ripoti iliyotolewa na shirika la mzalendo.

Uhuru azindua baluni za internet za loon ili kutumia vyema mtandao wa 4G

Kulingana na tathmini ya  ripoti  za hapo awali, Sudi amedumisha sifa yake hiyo ya kutosema lolote bungeni tangu mwaka wa 2017. Mbunge huyo ni mtetezi mkubwa wa naibu wa rais William Ruto  na amekuwa  akitoa maoni kuhusu masuala ya kisiasa

bunge 2

Ripoti hiyo imeonyesha kwamba  seneta wa  Busia Amos Wako  hakuzungumza  katika seneti  mwaka jana  pamoja na viongozi  wengine walioteuliwa

Shhh! Mwanamke ashtakiwa kwa kuwaita polisi ‘wafisadi’ Riruta

Viongozi hao ni  miongoni mwa wajumbe 25  katika seneti na bunge la  taifa  ambao wametajwa kwa  utendakazi mbovu  katika kipindi hicho. Seneta wa Kajiado Philip Mpaayei,  wenzake  wateule  Christine Zawadi  na  Mercy Chebeni  walitajwa kwa utendakazi adimu.

Seneta  Ledama Ole Kina (Narok)  alitajwa kama mchapakazi zaidi katika seneti.

bunge 3

Alifuatwa na Moses Wetangula (Bungoma), Aaron Cheruiyot (Kericho), Ochilo Ayako (Migori)  na  Getrude Musuruve (Mteule).

Katika bunge la taifa mbunge wa Mumias Mumias West John Naicca; Samuel Arama (Nakuru West); James Gakuya (Embakasi North); George Aladwa (Makadara); Abdi Shurie (Balambala)  ni miongoni mwa waliotajwa kwa utendakazi mbovu  katika bunge na mijadala

Miongoni mwa waliotambuliwa kwa uchapakazi mzuri katika bunge ni  Millie Odhiambo (Suba North), David Ole Sankok

( Mteule ), Wilberforce Oundo (Funyula)  na Robert Pukose (Endebess).

Waiguru kujua hatima yake siku ya Ijumaa

Spika wa senate  ameatangaza kwamba bunge hilo litafanya kikao siku ya Ijumaa ili kuijadili ripoti ya kamati ya wanachama 11 inayochunguza hoja ya kuondolewa afisini Anne Waiguru kama gavana wa Kirinyaga.

senate

Katika arifa ya gazeti rasmi la serikali iliyochapishwa Juni tarehe 23  maseneta wametakiwa kuwa katika bunge la senate  saa nane unusu mchana siku ya Ijumaa.

Gavana huyo ameshtumiwa na wawakilishi wa kaunti waliomuondoa afisini kwa kutumia vibaya  afisi yake, kukiuka katiba  na kukiuka sheria za uagizaji wa bidhaa.

Pia anashtumiwa kwa kujitengea shilingi milioni 10 kama marupurupu  yake ya usafiri.

Waiguru ameyataja madai hayo kama wongo na njama ya kuhujumu uongozi wake. Akijitetea mbele ya kamati ya wanachama 11 siku ya Jumatano, Waiguru amesema anapigwa vita kwa sababu ya kuunga mkono  mchakato wa BBI.

Kama Bosi![Picha] Waiguru aonekana akicheza ‘solitaire’ wakati wa kikao cha kumfurusha afisini

Endapo   kamati hiyo itapata uhalali wa mojawapo ya madai yanayotolewa na wawakilishi hao huenda wakaidhinisha uamuzi wao wa kumfurusha Waiguru afisini. Uamuzi huo hata hivyo utafanywa kupitia kura ya maseneta.

Endapo  madai hayo yatapuuzwa na  wanachama wengi basi hoja hiyo itashindwa.

Waiguru  Kukutana na waliomfurusha  leo wakati vikao vya kamati ya senate vinapoanza

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru leo  atakabiliana na wawakilishi wa kaunti waliopitisha hoja ya kumuondoa afisini mbele ya kamati ya seneti  inayoskiza madai ya kuondoewa kwake afisini.

Baada ya kumtimua Duale ,Uhuru sasa anajitayarisha kulirekebisha baraza la mawaziri na ripoti ya BBI

Watafika mbele ya kamati hiyo ya wanachama 11  kuanzia saa nne asubuhi. Kulingana na mwenyekiti wa kamati hiyo, seneta wa Kakamega Cleophas Malala, pande zote mbili zitaanza kikao chao leo kwa  kutoa mawasilisho ya mwanzo.

Muda mfupi baadaye  spika wa bunge la kaunti ya kirinyaga   Anthony Gathumbi,   mwenyewe au kupitia mwakilishi atawasilisha madai yote dhidi ya Waiguru. Kamati hiyo wiki jana ilimuagiza spika huyo kufika mbele yake na kutoa majina ya wawakilishi watatu wa kaunti watakaoandaman naye. Gathumbi pia alitakiwa kutoa nakala  20 zilizochapishwa za   stakabadhi zizilizotegemewa katika hoja ya kumuondoa Waiguru afisini. Pia alitakiwa kutoa majina ya mashahidi.

Trouble ni Amani: Mudavadi sio kinara wa chama cha ANC Osotsi

Wawakilishi hao wa kaunti Juni tarehe 9 walijadili na kupitisha hoja ya kumuondoa Waiguru mamlakani wakimshtumu kwa kukiuka katiba  na kutumia vibaya mamlaka ya afisi yake.  Jumatano, gavana huyo na mawakili wake  – Kamotho Waiganjo  na  Paul Nyamodi watakuwa kizimbani kukabiliana na madai dhidi ya mteja wao.

 

 

Wololo! Tazama ushahidi wa gavana Waiguru atakaotumia kujitetea mbele ya senate

Gavana  wa kirinyaga Anne Waiguru   ambaye waakilishi wa kauti walipiga kura ya kumtimua afisini amejitayarisha na  maboksi chungu nzima ya ushahidi ili kujitetea na madai yote ambayo waakilishi hao walitegemea kumuondoa afisini .

waiguru

Waiguru  aliwasilisha majibu yake hayo kupitia mabunda ya stakabadhi yaliyopakiwa katika maboksi mengi  yanayotarajiwa kuwasilishwa mbele ya kamati ya senate iliyopewa jukumu la kuamua hatma yake .

Ameandika ujumbe ufuatao

Today(Jumamosi) at about 4.20pm I filed responses to the impeachment motion with substantive responses to each of the allegations leveled against me. I have full confidence in my legal team and believe my response is sound. Let’s allow senate to do its work. I have confidence in the rule of law and believe that Truth & Justice will be our shield and defender.

waiguru 1

waiguru 2

waiguru 3

 

Urithi wa Kindiki! Maseneta 2 kumenyana kubaini atakayechukua wadhifa wa naibu spika

Wadhifa wa kurithi nafasi ya naibu spika wa bunge la seneti na iliyoachwa na Kindiki Kithure sasa imesalia na wagombezi wawili baada ya seneta mteule Isaach Mwaura na Stewart Madzayo wa Kilifi kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Katika taarifa aliyoitumwa kwenye vyomba vya habari, seneta Mwaura amesema ameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na uamuzi wa chama cha Jubilee wa kumpendekeza Seneta wa Uasin Gishu Margaret Kamar kurithi nafasi hiyo.

Je shule na makanisa nchini zitafunguliwa? Rais Kenyatta ataka wizara ya Elimu na Usalama kushirikiana

“Now that the Jubilee Party has endorsed Prof Margaret Kamar as its candidate for Deputy Speaker, I have come to a very difficult decision to withdraw my candidature. My bid to run for the second most important position in the Senate was inspired by the desire to ensure that the youth and persons with disabilities get represented in the top leadership of parliament. That I was the youngest of the 5 aspirants, and being a second term member, having served both in the National Assembly and Senate, I believed that I had what it takes to preside over the house of Senate, independently, impartially and with sobriety,” amesema Mwaura.

Isaac-Mwaura

Hiyo jana, seneta Madzayo wa Kaunti ya Kilifi alitangaza kujiondoa kwa harakati za kutaka nafasi hiyo kwa kile alisema ni ushauri kutoka kwa marafiki wake wa karibu na baadhi ya viongozi.

Yaliyomo kwenye kapu la hotuba ya rais katika maadhimisho ya Madaraka day- Soma

Mwaura aidha amesema kuwa eneo la Mlima Kenya limepoteza nyadhifa shupavu katika bunge la seneti na hivyo ni sharti na lazima serikali ijayo iangazie swala hilo.

“Mt. Kenya region has lost both the Deputy Speaker and the Deputy Majority Deputy Whip positions and it is my hope that this shall be put into consideration in future parliamentary leadership and other positions,” Mwaura amesema

Aluta Continua: Uhuru sasa kuwafurusha washirika wa Ruto Katika kamati za senate

Siku chache baada ya kuwaondoa  uongozini maseneta wanaomuunga mkono DP William Ruto katika senate , mpango wa kuwafurusha maseneta wa mrengo wa Rutro katika kamati za senate sasa umeanza kutekelezwa .

We Have Options:Mashambulizi dhidi ya DP Ruto yawahamakisha viongozi wa Kalenjin

uhuruto

Mtikisiko mkubwa wa uongozi wa kamati hizo unatarajiwa kufanywa kufikia siku ya jumanne . Kiranja  wa upande wa walio wengi Irungu Kang’ata  amesema wanakamilisha mabadiliko hayo na wanatumai kwamba yatakuwa tayari kufikia siku ya jumanne .

Miongoni mwa wale wanaolengwa  ni maseneta saba  waliopinga hoja ya kumuondoa Kindiki Kithure kam naibu wa spika  wa senate .

Maseneta hao ni  Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet), John Kinyua (Nyandarua), Samson Cherargei (Nandi), Susan Kihika (Nakuru), Aaron Cheruiyot (Kericho), Benjamin Langat (Bomet)  na  Kindiki mwenyewe .

Green light: Wana taaluma kutoka Ukambani waunga mkono Kalonzo kushirikiana na Jubilee

Ruto 2

Siku ya ijumaa  maseneta wote wa Jubilee  isipokuwa saba  hao  walipiga kura ya kumfurusha  Kindiki kama  naibu wa spika wa senate  baada ya jumla ya maseneta 54 kuidhinisha hoja hiyo .

Kindiki  alifurushwa  kwa kutokuwa muaminifu kwa rais Uhuru Kenyatta ambaye ndiye kiongozi wa chama cha Jubilee .

Kang’ata hata hivyo amesema  hapatakuwa na hila dhidi ya jamii yoyote katika kupendekeza mageuzi  hayo katika senate  lakini akaongeza kwamba baadhi ya waliopinga hoja hiyo watakiona cha mtema kuni.Cheruiyot  yupo katika kamati ya PSC ,ambayo ni muhimu kwani huta maamuzi  bungeni .pia ni mwanachama wa  kamati za ICT, Kawi na Bajeti

Kinyua, Cherargei  na  Langat  ni wenyeviti wa kamati za senate  na huenda wakapoteza nafasi hizo .Kinyua  ni mwenyekiti wa kamati ya ugatuzi  na uhusiano kati ya serikali kuu na za kaunti   na pia ni mwanachama wa kamati ya afya.

Tyranny of jokers?Ruto aachwa mataani baada ya Maseneta wake kushindwa kumuokoa Kindiki

Charargei  ni mwenyekiti wa  kamati ya haki  ,masuala ya kisheria na haki za binadamu  ambayo wanachama wake ni pamoja na   James Orengo  na  Okong’o Mogeni (Nyamira). Cherargei  pia ni mwanachama wa kamati za ugatuzi na leba .

Langat ni mwenyekiti wa kamati ya elimu  .seneta huyo wa Bomet pia ni mwanachama wa  kamati ya shughuli za bunge   na kamati ya kanuni na utaratibu . Pia yupo katika kamati ya  Utalii na viwanda .

 

 

No Targets:Mageuzi katika Senate hayalengi jamii yoyote asema Munya

Waziri wa kilimo  Peter Munya amewakemea viongozi wanaomuunga mkono DP Ruto  wanaodai kwamba mageuzi katika senate yanalenga  jamii Fulani . Amesema mageuzi hayo  katika chama cha Jubilee  yanalenga kukiboresha chama hicho na usimamizi wa serikali bali hakuna jamii inayolengwa .

Uhuru:Yaliyomo katika kapu la Shilingi Bilioni 53.7 za kuchochea ukuaji wa uchumi

Munya amesema Ruto amekuwa kikwazo   kwa ajenda ya serikali kwani amekuwa akiwachochea maseneta na wabunge  kusababisha vurugu serikalini na kufanya kuwa vigumu wa rais Uhuru Kenyatta kutekeleza majukumu yake ya utawala . Mirengo miwili ya kisiasa imeibuka ndani ya chama tawala cha Jubilee kati ya wanaomuunga mkono rais Kenyatta na walio katika upande wa naibu wake William  Ruto na kuunda makundi ya  Tangatanga  na  Kieleweke.

Akizungumza katika mkutano na wakulima wa kahawa huko Meru siku ya jumamosi Munya amesema  rais Kenyatta hajakiuka sheria au katiba kwani anatumia maamlaka yake kufanikisha demokrasia .Munya  amesema kuondolewa kwa Kindiki Kithure kama naibu spika wa senate ni jambo linalokubalika kwani seneta huyo alikuwa amemkaidi kiongozi wa chama chake .siku ya ijumaa maseneta 54 kati ya 67 walipiga kura kumuondoa Kindiki kutoka wadhifa huo .

Tyranny of jokers?Ruto aachwa mataani baada ya Maseneta wake kushindwa kumuokoa Kindiki

Wale waliopiga kura kumuokoa Kindiki ni   Kipchumba Murkomen wa  Elgeyo Marakwet, Susan Kihika wa  Nakuru, Samson Cherargei wa Nandi, Aaron Cheruiyot wa  Kericho, Christopher Lang’at wa  Bomet na Mithika Linturi wa Meru.Kindiki  wakati mmoja alikuwa ametajwa kama anayeweza kuwa mgombea mwenza wa naibu wa rais William Ruto wakati wa uchaguzi mkuu wa 2022 na kuondolewa kwake kama naibu spika wa senate ni pigo kwa mrengo wa DP

Munya amesema hatua ya kuondolewa kwa  Murkomen na susan Kihika katika uongozi wa senate ni dhihirisho kwamba rais Kenyatta  analenga kukinadhifisha chama cha Jubilee ili kuboresha ajenda yake ya maendeleo na usimamizi ufaao  wa shughuli za serikali .

Nafasi zao zilichukuliwa na Samuel Poghisio wa West Pokot  na seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata,

Munya  amesema kila mtu anafaa kuubeba msalaba wake  na kufuata mkondo anaotaka kinara wa chama cha Jubilee na  Mkuu wa serikali ,Uhuru Kenyatta