‘Samahani kwa kutukana jenerali Badi,’Sonko aomba msamaha baada ya onyo la Uhuru

Vuta ni kuvute imekuwa ikishuhudiwa mara kwa mara kati ya gavana wa kaunti ya Nairobi na jenerali wa  Nairobi Metropolitan Services (NMS) Mohammed Badi.

Sonko aliomba msamaha na kusema maneno haya saa chache baada ya kukutana na rais Uhuru Kenyatta katika mtaa wa KICC.

“Nataka kusema kuwa nimemsikia rais Uhuru Kenyatta na nimekubali kuwa mahitaji na kaunti ya Nairobi ndio muhimu kuliko wanasiasa

Nataka kuomba msamaha kwa ndugu yangu Badi kwa mambo mabaya ambayo nimesema kumuhusu na naahidi tutafanya kazi pamoja ili tuweze kuleta maendelea kwa wakazi wa Nairobi.” Alisema Sonko.

Badi alisema kuwa hakuwa na kinyongo dhidi ya gavana Sonko na kwamba alikuwa afanye kazi naye ili kuwasaidia na kuleta maendeleo kwa ajili ya wakazi wa Nairobi na kaunti hiyo.

LVrk9kpTURBXy81MTc4YjkzNTA4NGM3ZDg2MjE5YTk3ZmU2ZDJjMDllMS5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB

“Nataka kumshukuru Gavana kwa maana kwa maana tumefutilia mballi ugomvi wetu na baina ya NMS na timu ya gavana, tutafanya kazi na kuhakikisha kuwa wakazi wa Nairobi wamepata mahitaji yao na maendeleo.” Badi Aliongea.

Katika hotuba ya Uhuru alimuonya gavana na wanasiasa ambao wanaleta siasa katika sekta hiyo, pia lipongeza timu ya Badi kwa maendeleo ambayo wanazidi kutenda hasa katika maeneo duni jijini Nairobi.

“Nataka kupongeza timu ya NMS kwa maana kwa miezi hiyo mbili wamechimba visima zaidi ya 200 katika maeneo duni hapa Nairobi

Sonko uwache masiasa mingi, Jenerali Badi hataki kiti ya gavana, hataki kiti hata ya MCA hapa Nairobi. Huyu ni jenerali wangu na akimaliza kazi ya Nairobi atarudi katika kambi ya jeshi 

Mfanye kazi pamoja ili wakazi wanufaike. Mimi sina haja na siasa na wale wanataka kufanya siasa lazima wakae kando,” aliongeza Rais. 

‘ Mheshi Umechoma,’ Khaligraph Jones na mashabiki watoa hisia kuhusu mavazi haya ya Sonko

Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko anajulikana kwa mavazi yake ya kifahari na kipekee. Wikendi iliyopita Sonko alimtembelea mbunge wa Starehe Charles Jaguar na kuposti picha akiwa na wanawe Jaguar na kuandika ujumbe mfupi uliosoma,

“KIDS GROW VERY FAST. AKI HUYU @JAGUARKENYA NI SHARP SHOOTER NAONA HAPA NI COPYRIGHT HAJACHEZWA. AMA?”

Lakini mashabiki wake waliona tu nguo alizokuwa amevalia jaguar ‘Louis Yutton’ miongoni mwa waliotoa maoni ya kicheshi na rappa Khaligraph.

sonko-2

“NAONA MHESH AMEANZISHA BRAND YAKE NOMA SANA LOUIS YUTON @JAGUARKENYA 🔥🔥🔥 GOTEA SONKORE” Khaligraph Jones Aliandika.

Jaguar naye alijibu na kumwambia;

“😂HATA SIKUWA NIMEONA”

Haya hapa maoni ya mashabiki wake;

boydis777
@mike.sonko hio outfit ulichezwa come I hook u up with something legit

elceyjonnes
@sham.abass 047 anavaa Louis yutton 😂😂😂…waaah sultan yuko wapi jameni

iamkamaa
Pia Governor anavaa Yutton…enyewe hali sio rahisi

andrewndambuki
LMAO…Loius what?

ras.star_getyouinshape
Hapa mhesh ule mtu amechezwa ni wewe 😂😂 designer wako!!

amfaizhusseyn
Mhesh Leo uko Kwa Louis YuTon 😂

fadedkara.ni
Louis yu Ton sonko ulichezwa😂

Kamanda wa polisi aliyemshutumu Sonko kwa kumshambulia aletwa Nairobi kuwa mkuu wa Polisi

Rashid Yakub amehamishwa hadi  Nairobu kuwa mkuu wa polisi kutoka kwa Philip Ndolo.

Mabadiliko hayo yameangazwa siku ya jumamosi  na Ndolo ataelekea Nyeri kuwa naibu kamanda wa chuo cha mafunzo ya polisi Kiganjo .

Yakub alikuwa kamanda wa polisi wa pwani na  disemba mwaka jana alimshtumu gavana wa Nairobi Mike Sonko kwa kumshambulia wakati Sonko alipokuwa akikamatwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Voi  kuhusiana na kesi ya utoaji  zabuni  ya shilingi  Milioni 357 .

Baadaye Yakub aliamua kuondoa kesi hiyo dhidi ya Sonko

 

 

‘Nilikuwa mlevi,’Sonko azungumzia kutia sahihi mkataba wa jiji la Nairobi

Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko alidai kuwa alikuwa mlevi alipokuwa anatia saini kwenye mkataba wa kumpa rais Uhru Kenyatta mamlaka ya kaunti hiyo.

“Nilikuwa mlevi, hawa watu walinichanganya na pombe kwanza, wakati wa kukutana na rais Uhuru Kenyatta nilikuwa naona Zigizagi.” Aliandika Sonko.

Mto wa vifo!Gavana Mike Sonko azungumza na akina mama

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Sonko Alhamisi jioni alidai kuwa alitia mkataba huo saini kwa ajili ya heshima aliokuwa nayo kwa rais Uhuru.

” Na pia tulikuwa tunawatakia wakazi wa Nairobu mema.”

unnamed

Sonko alisema kuwa hatokubali vitisho kutoka kwa bosi wa NMS Mohamed Badi.

“Huyu jeshi akiendelea kutofuata sheria afadhali wanitimue kama Waititu, sitakubali vitisho zake tena anasahau kuwa huu ni mkataba na unaweza kufutiliwa mbali wakati wowote.”

Patashika yazuka baada ya maafisa wa EACC kuvamia afisi ya Sonko

Miradi minne ya kaunti ya Nairobi ilipewa serikali kuu, waziri Eugene Wamalwa na gavana Mike Sonko walitia saini makubaliano hayo.

Tangu Mike apeane mamlaka yake Machi 18 kwa Badi, kumekuwa na mgogoro mkubwa kati ya viongozi hao wawili.

Major General Mohamed Abdalla Badi

Hata hivyo Badi alisema kuwa hana nia yoyote ya kisiasa.

“Mimi si mwanasiasa na sina usemi wowote wa kisiasa na wala sitatami kuwa katika siasa, yangu tu ni utoaji wa huduma niko hapa kama mfanyakazi, na nitafanya kazi yangu ili kuhakikisha wadi zote,85 zimepata maendeleo.” Alisema Mwezi jana.

Wiki jana, Sonko alikuwa mbele ya mahakama kujibu maswali kadhaa, bali aliitokeza bila hati zozote na kumlaumu Badi kwa kutofuata sheria.

Patashika yazuka baada ya maafisa wa EACC kuvamia afisi ya Sonko

Kumezuka patashika  siku ya Jumanne wakati maafisa kutoka tume ya Eacc  walipovamia  afisi ya kibinafsi ya gavana wa Nairobi Mike Sonko katika eneo la Upper Hill .

Maafisa kadhaa wa polisi walikuwa wamendamana na makachero kutoka Eacc  katika afisi ya gavana huyo  iliyojengwa kwenye kipande cha ardhi yenye thamani ya shilingi milioni 500 ya wafanyikazi wastaafu wa  Kenya.

Polisi walikuwa wamekuja kukadiria thamani ya kipande hicho cha ardhi, thamani yake inakadiriwa kuwa shilingi  milioni 500.

Hata hivyo maafisa hao walipofika walizuiwa kuingia na wafuasi wa Sonko  na wakalazimika kukwea lango kuu ili kuingia ndani ya jengo hilo.

Baada ya takriban saa tatu za mshikeshike, maafisa hao waliondoka bila kutekeleza walicholenga . EACC inachunguza jinsi Sonko alivyopata ardhi hiyo .

 

 

Ndoa ya Sonko yamfanya Akothee kuwa na hamu ya kuolewa

Mwimbaji maarufu Akothee, sasa anasema yuko tayari kuingia katika ndoa.

Mama huyo msimbe mwenye miaka 40, alikiri kwamba kulea watoto peke yake haijakuwa safari rahisi kwake lakini kwa sasa anatamani kuwa na mwenzake wa maisha.

Katika ujumbe mrefu kwenye Instagram, mama huyo wa watoto watano alimsifu Gavana wa Nairobi, Mike Sonko na mke wake Primrose walipokuwa wakisherehekea miaka 21 katika ndoa.

Raia wa Amerika aliyenaswa akiwatusi wakenya atimuliwa nchini

Alitambua namna ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kwa sababu ya kutokuwa na subira.

“Mheshimiwa sisi tulipoteza subira, tunataka wanaume ambao wamepikwa tayari na wana magari makubwa, majumba na pesa, na pia tunawataka wale wenye six pac pia, ndio maana wengi wetu tunaekeza kwa mtindo wa maisha badala ya kuekeza cha maana,” “Mike Sonko, nitakuambia ukweli, natamani wanandoa wachanga wawe na subira na kuvumilia na kujengana sisi sote tunaweza kuwa katika ndoa na kuwa tajiri pamoja, na kulea watoto wetu kama familia,” alisime Akothee.

Akothee aliongezea kuwa vijana wengi hawatambui kuwalea watoto katika uhusiano uliovunjika hawajui maisha ya faraghani yanavyoambatanishwa na majonzi na masumbuko.

Umoja wa Magharibi! Viongozi kutoka Magharibi wasema wako imara

Kulingana na mwimbaji huyo, sasa ametambua maana ya kuwa na mwenzake wa kumsaidia katika ufanisi na pia kutafuta ushauri kutoka kwake.

“Natamani ningekuwa na mume ambaye anaweza angalau tu kunilipia gharama ya umeme, ama hata kuninunulia kemikali za dimbwi la kuogelea, ama hata bidhaa za jikoni yaani hata nyanya tuu,” “Maisha ya uhuni ni ngumu. Ni wewe tu kutoka asubuhi hadi jioni, hakuna mtu wa kukupa ushauri, wa kukumbatia usiku ama hata wa kukuamkua asubuhi. Tuko tu tunatamani uhusiano za watu kwenye mtandao ya kijamii. Mwambie mke wako Primrose rais wa akina mama wasimbe angependa wasia wa kuwa na subira. Nataka kuolewa na miaka 40 nimechelewa sana lakini nina imani,” aliongezea Akothee.

 

 

Ukarimu wa Sonko! Ajitokeza na kumsaidia kocha wa zamani wa Harambee Stars

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amejitokeza kumsaidia aliyekuwa kocha wa zamani wa Harambee Stars Marshall Mulwa.

Licha ya kuiletea Kenya sifa sufufu katika rubaa za kimataifa kupitia unahodha wake katika timu hiyo ya kitaifa, Mulwa alikuwa akiishi maisha ya kusikitisha.

Kocha huyo wa zamani ambaye ana umri wa miaka 75 alibaki upweke baada ya familia yake kuamua kuishi ughaibuni.

Kutokana na umri wake, Mulwa hakuwa na njia nyingine ila kuwategemea wahisani ili kupata lishe na kusukuma gurudumu la maisha.

Wakati kikosi cha Sonko kilimtembelea katika nyumba yake ya kukodisha, Mulwa alipokea chakula huku Sonko akiahidi kusaka njia zingine mwafaka zitakazomfaa ili kuboresha maisha yake.

mike.sonko

“Mpira wa miguu unachukua jukumu muhimu katika jamii yetu kwa kuunganisha nchi yetu na pia kwa kuwapa vijana fursa ya kupata riziki,” Sonko alibaini katika chapisho la Facebook.

“Kandanda imekuwa na umuhimu mkubwa mno katika kuleta umoja nchini mwetu na vile vile kuwapa ajira vijana,” Sonko alisema kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Komesha Ubaguzi! Wacheza wapiga magoti kukomesha ubaguzi wa rangi

“Tutazungumza naye ili kujua ni vipi tunaweza kumsaidia ili aboreshe maisha yake,” aliongeza.

Wakati akiwa nahodha wa kikosi cha Stars, timu hiyo ilipata ushindi mara tatu katika Cecafa Senior Challenge kati ya mwaka wa 1981 hadi 1983.

Sonko na mkewe watimiza miaka 21 ya ndoa

Japo yupo chini ya shinikizo haswa baada ya kutimuliwa kutoka kwa afisi zake City Hall, Mike Sonko anasalia kuwa na furaha na kuendeleza familia yake kwa furaha.

Sonko na mkewe Primerose wameadhimisha miaka 21 ya ndoa na akitumia fursa yake, mkewe Primerose aliandika katika mtandao wake kumshukuru mumewe kwa kuendelea kuijali familia yao kwa miaka hiyo yote ambayo wamekuwa pamoja kama mume na mke.

Alimtakia mumewe Sonko maadhimisho mema ya ndoa saa chache tu baada ya Sonko kuwashauri wanaume kuwajibikia majukumu yao kama wazazi.

Muigizaji Luwi amsherehekea mpenziwe kwa kusimama naye

Primerose alitundika picha yao wakiwa pamoja na akiwa amekalia karibu na Sonko, picha ikiashiria penzi lao halisi.

Miongoni mwa watu wanaomfuatilia walimpongeza kwa kuishi kwa ndoa miaka hiyo yote na kumtakia kila heri.

Katika ujumbe huo, Sonko alifunguka na kusema kuwa japo hakuna mwanadamu aliyemkamilifu duniani, mafanikio yake kwenye ndao yao ni kusema neno Sorry anapokuwa amekosea.

Ramsy Nouh matatani! Mwanamke amkashifu kwa kukosa kumlipa

Amewahimiza wanaume kuomba msamaha iwapo wamekosea katika uhusiano na wakati wanapotofautana na wake wao.

 “If your wife catches you with a side chick say sorry, If you return home late say sorry. If you are wrong always say sorry,” Sonko.

 

Sonko ahaidi kulipa laki 300 kwa minajili ya kusaidia watoto wa afisa aliyemtia mbaroni Voi

Jaribio la kutia mbaroni gavana wa Nairobi Mike Sonko katika eneo la Voi litasalia kama kumbukumbu kwa wengi kufuatia namna afisa wa polisi alivyokabiliana naye mbele ya umma.

Kama njia ya kuonyesha upenda,Sonko ameamua kumlipia afisa huyo ambaye hii leo amekipata cha mtema kuni baada ya mwanamke mmoja kumshika mzima mzima mbele ya umma akisema afisa huyo aliyestaafu amekataa kutoa laki 300 za kukithi nmahitaji ya wanawe.

Sonko hata hivyo ,amesema atatoa kima hicho cha pesa ili zisaidie kukimu maisha ya afisa huyo aliyejulikana kama Mureithi.

Mureithi ni miongoni mwa maafisa wa polisi waliokabiliana na Sonko katika eneo la Voi alipokuwa anajaribu kukimbia kutiwa mbaroni na maafisa kutoka DCI.

Embedded video

Akitumia muda wake kupitia ukurasa wa Facebook,Sonko amesema amemsamehe Mureithi na atashughulikia maslahi ya wanawae.

“The Voi Base Commander who handcuffed me becomes a dead beat dad. I do not support domestic violence. I condemn the use of violence in any relationship but pole sana my friend Mr. Mureithi the recently retired Voi Base commander who forcefully handcuffed me with two pairs of handcuffs just to board a police chopper during my arrest at Voi,” aliandika Sonko..

Heka Heka! Mwanamke amshika kamanda wa polisi kimaso kwa kukosa kujukumikia majukumu yake

Amemtaka afisa huyo aliyestaafu kwa sasa kukubali iwapo watoto ni wake

 “My humble advice to you, if the baby the woman is alleging is really yours kindly accept the responsibility its just normal part of life and since you are now retired, I’m willing to pay for you the 300,000/= upkeep the woman has been awarded by the children’s court.”

Half Gavernor? Hatimaye Sonko atia saini kwa mswada wa ugavi wa fedha

Gavana aliye chini ya shinikizo Mike Sonko wa jimbo la Nairobi hatimaye ametia saini katika mswada wa ugavi wa fedha mwaka 2020 na ambazo zitapelekwea katika wasimamizi wa jiji kwa jina Nairobi Metropolitan Services NMS.

ImageImage

Serikali kufungua uchumi wa taifa- Kibicho asema

 

ImageImage

 

Mtafaidi nini mkiniua? Maisha yangu yamo hatarini, Moses Kuria asema

Taarifa za Sonko kutia saini katika mswada huo zinajiri miezi michache tu baada ya kudai kuwa hatatia saini katika nakala nyingine ili kuzuia baadhi ya majukumu yake makuu kutwaliwa na serikali kuu.

Katika mswada huo wa fedha ambao Sonko ametia saini hii leo, bilioni 1.25 zimetengwa kwa niaba ya maendelea jijini huku bilioni 2.25 zikitarajiwaa kugharamia mahitaji mengine.