PATANISHO: Mimi ndio hupigwa katika ndoa ya wake watatu

Taiti, 35, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Ernest, akidai kuwa wawili hao wanashinda wakikosana kila wakati akidai kuwa amefika mwisho na hajui la kufanya.

PATANISHO: Mke wangu hunidanganya kuwa mpango wa kando ni cousin yake

“Tulikosana Alhamisi wiki iliyopita kwani alienda kunywa pombe na wazee wenzake na akarudi na makelele, akanipiga karibu anichome na stove na hapo nikaondoka na kwenda nyumbani.” Alisimulia akisema kuwa mumewe ana wake watatu.

Stima ilikuwa imepotea na nikaondoka kwenda kununua mafuta ya taa, kurudi nikampata amesimama kwa mlango na kumuuliza mbona hajavalia nguo, akadai namuongelesha vibaya.

Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Hapo alichukua stove na kutupa na ikabaki nikizima moto.” Aliongeza akisema kuwa licha ya hayo yote bado anampenda na angependa kumrudia.

Isitshe Taiti alificchua kuwa mumewe huwa hapigi wake wengine ila yeye.

Bwana Ernest alisema kuwa wawili hao wanakosana tu kwa mambo ya ulevi na kuwa wawili hao ni walevi.

“Tulipokosana tulikuwa walevi pamoja na tulikuwa tunapiga story nikimwambia kuwa nitaongeza mke wa nne. Hapo akakasirika kwani hakujua ni mchezo.” Alijitetea.

PATANISHO: Ukibadilika nitajua tu kwani CCTV Ni mob