Toboa Siri: Nilikuwa napepeta mke wa rafiki ya babangu

Jamaa kwa jina kingman alijitolea kutoboa siri ambayo imekuwa ikimsumbua kwa miaka kadhaa sasa.

Huku akiwa hadithia watangazaji Mbusii na Lion katika kitengo cha toboa siri jamaa huyo alifichua kuwa alikuwa na uhusiano na mke wa rafiki ya babake.

Toboa Siri: Nimezalisha bibi ya bro yangu na hajui juu yuko Somalia

Alidai kuwa mke wa rafiki ya babake alikuwa na mtindo wa kuwatembelea nyumbani na wawili hao wakatengeneza urafiki ambao ulizaa matunda ya uhusiano wa siri ambao hamna yeyote aliyejua.

Uhusiano huo ulipepetwa na kuwa babake Kingman na mume wa mpenziwe walikuwa wakisafiri mara kwa mara na wawili hao kubakia upweke kwa zaidi ya wiki nne.

Nilimaliza form four last year na nilikuwa na kaa na mzae wa mine sides za Thika. Budangu alikuwa anaenda na ma lorry na sasa kuna msee alikuwa anaenda naye job.” Alisimulia Kingman.

So wife ya beste yake alikuwa anakam kejani time buda yuko wanaongea, sasa time mob buda alikuwa anaenda kwa wiki tatu au nne ivi so huyo wife alikuwa anakam keja tuna tulia tulia.

Sasa siku mob akanishow huwa amenitambua na alikuwa ameiva juu bado alikuwa myoung. Sasa nilijipata nimepita na yeye mara ka nne nikiwa chuo bado.” Aliongeza akidai kuwa wawili hao bado huzungumza ispokuwa ni vile yeye anaishi mbali sahii.

Toboa siri: Nataka bro yangu ajue huwa napiga bibi yake kuni

Pata uhondo kamili.

Toboa Siri: Nimezalisha bibi ya bro yangu na hajui juu yuko Somalia

Jamaa aliamua kutoboa siri kali akidai kuwa alimzalisha bibi ya ndugu yake baada ya wawili hao kuanzisha uhusiano pindi tu nduguye aliondoka na kwenda shughuli ya kulinda amani, Somalia.

Toboa siri: Nataka bro yangu ajue huwa napiga bibi yake kuni

Alisimulia kuwa nduguye mkuu alimuarifu amuangalilie mkewe lakini alianzisha uhusiano ambao ulizalisha mtoto. Cha kushtua ni kuwa hamna anayejua kinacho endelea hata baada ya jamaa kuondoka kwa miaka mitatu.

Alisimulia, Niko na siri kubwa, mimi nina bibi na nina penda bibi ya ndugu yangu kuliko wangu, ndugu yangu mkuu ni jeshi wa KDF na yuko Somalia na aliniambia niwe nikimuangalilia.

Unajua yeye alichagua ile material minji minji wife material lakini huyu wangu ako chini kidogo. Tumeendelea na hata tumezaa pamoja mtoto mmoja wa mwaka mmoja na tunafanana kabisa.

Akaongeza, ndugu yangu alizaa naye watoto wawili na akaenda nami nikaongeza wa tatu. Ndugu yangu anajua ana watoto wawili na hata sijui akirudi itakuwa aje kwani amekuwa huko kwa miaka mitatu na nashuku alioa mke mwingine.

Yeye huniambia nimuangalilie mke na sasa naona nilimuangalilia vizuri.

Toboa Siri: Bwanangu Huniita Jina La Mamangu, Sikujua Anampiga Kuni Pia

Pata uhondo kamili.

Toboa siri: Nataka bro yangu ajue huwa napiga bibi yake kuni

Jamaa alituma ujumbe akidai anataka kumtobolea nduguye siri ili ajue kuwa amekuwa akimnyemelea mkewe.

Alidai kuwa shemejiye ni mrembo kupindukia na kuwa hawezi kataa majaribu hayo.

Sa unajua bro akiwa siendangi mchana ni bibi yake tu natembelea. Unajua kitu ukiitiwa huwezi acha halafu tena ukiangalia bibi ni mrembo kabisa. Wale wenye mimi hupata huwa tunaachana.

Nina miaka 21 na mke wa bro ana miaka 23 lakini bro yangu ni wa miaka 32. Alisimulia.

Pata uhondo kamili.

Toboa Siri: Bwanangu Huniita Jina La Mamangu, Sikujua Anampiga Kuni Pia

Mrembo mmoja aliwashangaza watangazaji Mbusii na Lion katika kitengo cha ‘Toboa Siri’ alipofichua kuwa mumewe amempachika mamake mimba.

Mwanadada huyo alikiri kuwa shida ilianza wakati mmoja mumewe alirudi nyumbani akiwa mlevi chakari na badala amuite jina lake alikuwa anamuita jina la mamake.

Toboa Siri: My wife has no idea I have been sleeping with her younger sister

Hapo alianzisha uchunguzi na ndipo aligundua kuwa wawili hao wana uhusiano. Isitoshe amempachika mimba.

“Mimi nimeolewa na nina mtoto moja. Nimekaa kwa ndoa kwa miaka miwili sasa tulikuwa tunakaa vizuri na mume wangu na ilifika mahali akaanza kubadilika, mara hali kwa nyumba na nikimuongelesha anajibu na hasira.” Alisimulia mwanadada huyo.

Siku moja kwenye harakati zake za ulevi alianza kuniita jina la mama yangu. Sasa nikashindwa nini inaendelea na aliendelea kuniita ivo siku kadhaa. Naishi na yeye lakini mamangu yuaishi kivyake kwani ni single mother.

Toboa Siri: Nina Sugar Mummy Na Bibi Yangu Hana Shida

Nikakuja nikachunguza nikapata wana uhusiano pamoja na hata sahii mamangu (mwenye umri wa miaka 40) ana mimba na nashuku ni yake. Niliangalia message zenye hutumiana na hata mamangu humuita sweetheart.” Aliongeza akidai kuwa hajui kama mamake mzazi anajua uhusiano wao.

Skiza uhondo wote.

Toboa Siri: Nina Sugar Mummy Na Bibi Yangu Hana Shida

Jamaa fulani aliwashtua wengi katika kipindi cha Mbusii na Lion Teketeke katika kitengo cha ‘Toboa Siri’ alipofichua kuwa ana sugar mummy Nairobi huku mkewe akiwa mashambani.

Isitoshe, mkewe anajua kuwa jamaa ana Sugar mummy lakini hana shida kwani amefanya kila juhudi ili kumpa maisha bora.

Kuna huyu mama tulipatana naye huku tao, tukaanza urafiki kidogo kidogo mwishowe ikawa mapenzi.

Sasa unajua huyu mama ni tajiri sana. Mimi niliacha bibi ocha na huyu mama anadai nimpeleke nyumbani kwetu na sijawahi mwambia nina bibi. Tumekuwa na uhusiano na huyu mama kwa miaka mitano na huyu mama tumekuwa kwa uhusiano wa miaka mitatu.

Mimi huenda nyumbani lakini inabidi nimemdangaya kuwa naenda kumsalimia mama mzazi. Huyu mama tunaishi naye kwake na ni mzee kiasi kwani ameniwacha na miaka kumi na miwili.

Kazi yangu na yeye ni kumpeleka kazini na gari halafu narudi baadaye akimaliza kazi. Kuni nayo naitembeza vibaya sana. Aliongeza akidai kuwa mkewe anajua hayo yote lakini hana shida kwani namfanyia mazuri nyumbani kama kujenga nyumba.

Skiza uhondo kamili.

 

Toboa Siri: Niliua mtoto kuficha aibu kwani alikuwa wa baba wa kambo

Katika kitengo cha ‘Toboa Siri’ juma hili, watangazaji Mbusii na Lion walipigwa na mshtuko baada ya mwanadada mmoja kusimulia kisa kilichomkumba akiwa angali mtoto mdogo.

Alisimulia kuwa mamake aliolewa na mwanaume mwingine akiwa mdogo na kuwa hakujua kuwa yule baba wa kambo angegeuka kuwa mnyama kwake.

Kulingana na mwanadada yule, siku moja yule jamaa alimnajisi na kumtishia kuwa atamuua kama angemweleza yeyote kuhusu unyama huo, Isitoshe aliendeleza unyama ule kwa siku kadhaa na mambo yaliharibika baada yake kupata mimba.

Hapo alingoja hadi mtoto azaliwe na akaamua kuchukua sheria mkononi mwake na kumuua yule mtoto kwa kumnyonga ili kuficha ile aibu ya baba wa kambo. Cha kushtua ni kuwa hajawahi eleza yeyote kuhusu kisa kile na alingoja hadi kutoboa siri yake hewani.

Soma usimulizi wake na kisha uskize kanda yake.

Sasa mamangu aliolewa akiwa na mimi na mzee wake ambaye ni baba wa kambo wangu, aliniita siku moja na kuniambia nimpelekee simu kutoka kwa bedroom.

Sasa kwa ajili nilikuwa mtoto mdogo wa darasa la saba akanibaka na akaniambia nisimueleze yeyote kwani atanimaliza. Wawili hao bado wameoana.

Alinibaka karibu mara tatu hadi nikashika mimba yake na mamangu alidhani kwamba nimepata ile mimba huko nje, na nilishindwa kumwambia mamangu lakini ile siri ilikuwa inaniumiza moyoni.

Baada ya miezi tisa nikazaa kama kawaida na ilibidi nilimmaliza yule mtoto kwani singeishi naye. Nilimnyonga tu ivo na hata hawakujua chenye kilikuwa kinaendelea. Walimzika na hiyo kitu ikaishi lakini naangalianga huyu mzee nahisi kumfanyia kitu kibaya lakini sijawahi ambia mtu yeyote.

Alisimulia mwanadada ambaye alitoka kule na kusafiri hadi Nairobi.

Skiza kanda ifuatayo.