Hongera! Kenya 7s yafuzu kwa michuano ya Olimpiki Japan 2020

Timu ya raga ya wachezaji saba kila upande ilifuzu kwa mchuano ya Olimpiki Japan mwaka ujao, baada a kuilaza Uganda 31-0 katika fainali za Africa 7s jana, mjini in Jo Berg, Afrika kusini.

Oscar Dennis alifunga mara mbili huku , nahodha Andrew Amonde, Daniel Taabu, na Jeff Oluoch pia wakifunga. Shujaa wanarejea kwa mara ya pili baada ya kuwakilisha Afrika katika awamu ya Rio 2016.

Timu hio itarejea nyumbani kesho huku wakianza mazoezi ya mkondo kwanza wa IRB sevens, itakayochezwa Dubai mwezi ujao.

Hayo yakijiri, mabingwa KCB walilaza Top Fry Nakuru alama 50-13 huku Homeboyz, wakiwanyuka Menengai Oilers 25-20 katika michuano ya ligi ya raga ya Kenya cup.

Kabras nao waliwagwaruza Impala 25 -3 na kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa baada ya mechi ya tatu, sawia na KCB na Homeboyz. Kwingineko Mwamba waliwagwaruza Kisumu 65- 22, nao Nondes wakiwalima Blakblad 38- 23.

Tukielekea ulaya, Leicester ilipanda hadi nafasi ya pili kwenye jedwali ya EPL baada ya kuinyuka Arsenali 2-0. The foxes walipachika mabao yao kupitia mfungaji bora Jamie Vardy na James Maddison katika kipindi cha pili na kuhakikisha Arsenali wameshuka hadi nafasi ya sita.

kwingineko, Chelsea ililaza Crystal Palace 2-0 kupitia mabao ya Tammy Abraham na Christian Pulisic na kupanda hadi nafasi ya tatu. huku Sheffield United ikipanda hadi nafasi ya tano bada ya sare ya 1-1 na Tottenham.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ”hakuna nafasi kabisa ” ya klabu hiyo kumsajili Kylian Mbappe, ingawa kumekuwa na kampeni za mitandao ya kijamii kuhusu tetesi za kuwa mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain ,20 atatua kwenye klabu hiyo.

Barcelona walirejea kileleni mwa ligi ya Uhispania baada ya kuilaza Celta Vigo mabao 4-1, huku nahodha Lionel Messi akifunga magoli matatu naye Sergio Busquets akiongeza la nne.

Lucas Olaza alifungia Celta goli la kufuta machozi. Ushindi huo ulihakikisha Barca wamejizolea alama 25 sawia na mahasidi Real Madrid huku wakiwa na magoli mengi.

Real Madrid nao wailiwaadhibu Eibar 4-0 huku Karim Benzema akifunga mawili nao Sergio Ramos na Federico Valverde ’wakiongeza moja kila mmoja.

Katika ligi ya Ujerumani, mabingwa Bayern Munich waliwapiga Bourssia Dortmund 4-0, chini ya mkufunzi wa muda Hansi Flick.

Robert Lewandowski alifunga magoli mawili huku Serge Gnabry akiongeza la tatu naye mlinzi Matts Hummels akijifunga mwenyewe. Bayern walipanda hadi nafasi ya tatu na alama 21, alama moja nyuma ya Borussia Mönchengladbach ambao hawajacheza mechi moja.