Oh No!Covid-19: Watu 5 wa kwaya maarufu ya Uganda Watoto Children’s choir wapatikana na virusi vya Corona

Wanachama watano wa  kwaya ya muziki ya Uganda ya  Watoto Children’s Choir  wamepatikana na virusi vya   Corona  baada ya kuzuru Marekani na Canada wiki mbili zilizopita .

Corona Movies/Series: Filamu zenye maudhui yanayofanana na zimwi la Coronavirus unazoweza kutazama (Part 1)

museveni

 

Siku ya Jumanne tarehe 31, rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza visa 11 vipya vya ugonjwa huo na kufikisha jumla ya watu 44 walioambukizwa COVID 19 nchini Uganda. 11 hao ni pamoja na watoto 5 wa kwaya hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na kwaya hiyo, makundi yao mawili yalirejea kutoka Marekani na Canada wiki mbili zilizopita. Kwaya  zote mbili kisha ziliwekwa chini ya karantini baada ya kuwasili Uganda  tangu machi tarehe 20 .

Habari za Hivi Punde! Prince Charles apona Corona

“ Mtu mmoja mzima alipatikana na virusi hivyo wakati huo na mara moja akatengwa’ sehemu ya taarifa hiyo inasema .

Baada ya wengine kupimwa,  watu watatu  wazima  na mtoto mmoja walipatikana na virusi hivyo  na kulazimisha vipimo kufanywa kwa wanachama wote waliosafiri. Kwaya hiyo imekuwa ikifanya ziara za matiafa ya nje   imezuru Marekani, Canada na Uingereza. Uganda imetangaza  marufuku ya kutotoka nje  kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo na kufunga mipaka yake .

 

 

 

 

 

Mhubiri Uganda akamatwa kwa kusema hakuna coronavirus Afrika

 
Polisi jijini Kampala, Uganda wamemkamata kasisi mmoja kwa kutamka matamshi yasiyo ya kweli na kueneza propaganda kuhusu ugonjwa wa Coronavirus.

Mhubiri huyo anadaiwa kutumia stesheni yake ya runinga kuwaambia umma kuwa ugonjwa huo haupo barani humu huku akidai kuwa hakuna kifo hata kimoja kimeripotiwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika.

Hayo yakijiri, idadi ya watu ambao wamegunduliwa kuwa na virusi vya Corona nchini Uganda imeongezeka kutoka wagonjwa kumi na 18 hadi 25 baada ya watano kupimwa siku ya Ijumaa.

Serikali sasa imewataka waganda kuzingatia kwa kina mikakati iliyowekwa ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Tukirejea nchini, serikali inahimizwa kubadili marufuku ya kutotoka nje ili iwe ya kuanzia saa tatu usiku ili kuwaruhusu wanaotekeleza huduma muhimu kufika nyumbani kutoka wanapoondoka kazini.

Mwenyekiti wa muungano wa wamiliki matatu Simon Kimutai anasema washikadau katika sekta ya usafiri wa umma wako tayari kuafikiana makubaliano ili tatizo la kuongezwa ka nauli lisuluhishwe.

 

Hot Momma! Zari Hassan afichua umri wake

 Zari Hassan  amekuwa akipokea shutuma kwamba ameficha umri wake na kwamba amekuwa akidanganya kuhusu  miaka yake halisi .

Not Me! Kipusa katika video ya wimbo wa Diamond ‘Jeje’ Akanusha kuwa katika uhusiani na staa huyo .

Zari hajakuwa akiwajibu wale wambao wametlia shaka ukweli wake kuhusu umri wake halisi  akisema yungali hajatimu umri wa miaka 40 .   mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz na mama ya watoto watano  ndio sasa anakaribia umri wa miaka 40 kwani kwa sasa ana umri wa miaka 39.

Je,Diamond na Malaika ni wapenzi? Simba aandika jumbe kwa Kipusa huyo wa video ya ‘Jeje’

Amefichua hilo katika ujumbe wa picha aliopiga kiwa nchini Uganda  kwa kuandika;

“What 39 going 40 looks like.”

Wengi wamekuwa wakisema kwamba huenda Zari  ana umri wa juu kuliko muonekano wake .  Katika tukio moja  picha za  pasipoti  yake zilivuja mtandaoni na kuonyesha kwamba  alikuwa ameshatimu umri wa miaka 40  na alikuwa akidanganya kuhusu miaka yake .

Oh No! Mkunga mashakani baada ya ‘kukata’ kichwa cha mtoto

Maafisa wa polisi nchini Uganda wanachunguza kisa kimoja ambapo mkunga mmoja aliripotiwa kumuhudumia visivyo mama mjamzito aliyekuwa katika uchungu wa kujifungua ambapo kichwa cha mwanawe kilikatika.

Inadaiwa kwamba muuguzi huyo alimvuta mtoto huyo kwa kutumia nguvu nyingi mtoto huyo ambaye tayari alikuwa amefariki na kuishia akibeba kiwiliwili chake wakati mama huyo alipokuwa akijifungua.

Tanasha hakuwa na mapenzi dhabiti kwa Diamond asema Tunda

Wakati mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoingia katika chumba cha kujifungua , familia yake inasema kwamba alisubiri kwa muda mrefu kabla ya kuhudumiwa.

Kwa siku nne mfululizo alikuwa amelazwa katika kituo cha Afya cha Bulumbi 111 akisubiri wakati mwafaka wa kujifungua mwanawe.

Kulingana na gazeti la Daily Monitor, wakati mmoja wa familia yake iliwasilisha ombi la kuitaka hospitali hiyo kumhamisha hadi katika kituo cha msalaba mwekundu iwapo hospitali hiyo ilikuwa imeshindwa kumsaidia ajifungue.

Kulingana na gazeti hilo babake mtoto huyo alisema: Tulienda hospitalini siku ya Alhamisi, iwapo walikuwa wameona tatizo lolote wangekuwa wametuarifu tumhamishe hadi kwenye kituo cha msalaba mwekundu , lakini wakalazimika kutumia nguvu.

Wakati mkunga huyo alipokuwa akimhudumia muda wa saa sita mchana , miguu ya mtoto ilikuwa ya kwanza kutoka lakini mtoto akakwama kuanzia mabegani kwenda juu.

Inasemekana kwamba Mkunga aliyekuwa anamsaidia mama huyo kujifungua alimvuta mtoto huyo na baadaye kwenda kuketi chini. Baadaye alirudi akamvuta mtoto na kuanza kumgeuza geuza. Muuguzi huyo hatahivyo anadaiwa kuomba usaidizi kutoka kwa muuguzi mwenzake.

Muuguzi huyo alimvuta mtoto huyo huku akimgeuzageuza na baadaye mtoto akatoka lakini bila kichwa.

Babake mtoto huyo alisema: Wakati mtoto alipotoka , muuguzi aliendelea kumvuta mtoto na kumrudisha ndani . Mtoto alikufa kifo kibaya .Serikali inahitaji kuwafunza hawa watu.

‘Mume wangu mwoga hajui kufanya mapenzi!’Mwanamke apasua mbarika

Bi Musazi anasema kwamba mwanawe alikuwa mzima kutokana na ushahidi wa miguu yake iliokuwa ikicheza.

Kisa hicho kimezua hisia kali nchini Uganda huku wakaazi wakitoa wito kwa serikali kuwafunza wakunga jinsi ya kusaidia katika kujifungua.

Bwana Ibrahim Okelo ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho alisema: Tunaitaka serikali kuwabadilisha wakunga hao na msimamizi wa hospitali,

Mwili wa mtoto huyo ulipelekwa kituo cha Afya cha Busia kwa uchunguzi kabla ya kupelekwa nyumbani kwa mazishi.

Maafisa wa polisi wamesema kwamba wanachunguza kesi hiyo wanayodai kuwa kisa cha uzembe dhidi ya mkunga huyo.

Wakaazi wanadai kwamba katika kipindi cha miezi mitatau , wanawake wawili na watoto wawili wamefariki wakati wa kujifungua katika kituo hicho.

Maafisa wa polisi wanadaiwa kuwa walipelekwa ili kuweka usalama katika kituo hicho cha Afya baada ya wakaazi kujaribu kukivamia kutokana na masuala hayohayo.

Jaribio la gazeti la Daily Monitor kuzungumza na msimamizi wa kituo hicho cha Bulumbi 111 pamoja na afisa wa afya wilayani hazikufua dafu kwa kuwa hawakushika simu zao.

Wale walioshika simu walisema kwamba hawajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

-BBC

Beauty and brains: Wajue wanamuziki hawa warembo kutoka Uganda

Mara nyingi, tunapoangazia wanawake warembo, waliobobea na wanaong’aa katika upande huu wa Afrika Mashariki, sisi huangazia sana wanawake kutoka humu nchini na sana sana Tanzania.
Hata hivyo, chenye wengi wamesahau ni kuwa Uganda kwa Museveni, sanaa ya muziki imepamba moto huku wanawake wakiwa katika mstari wa mbele kupeperusha bendera hiyo.
Leo tunaangazia warembo nane ambao wamebarikiwa na sauti na talanta ya usanii,
1.Spice Diana
spice diana

2.Juliana kanyamozi

Juliana.Kanyomozi1


3. Sheebah

Image result for sheebah karungi


4.Winnie Nwagi

winnie nwagi

5.Desire Luzinda

desire

6.Irene Ntale

Irene Ntale

7. Fille

fille


8. Kemi sera

Kemi sera

Nililala nikaamka na lafudhi ya Marekani – Mwanadada kutoka Uganda asema

Mwanadada mmoja kutoka nchi jirani ya Uganda ambaye anaiga wamarekani anapozungumza, amewashtua wengi baada ya kudai kuwa sio kupenda kwake ila aliamka siku moja na kujipata na lafudhi hiyo.

Kwa wale wasiojua maana ya neno lafudhi ni; Lafudhi ni namna ya pekee ya kutamka lugha kutokana na lugha ya mwanzo/awali ya mzungumzaji au eneo alipojifunza lugha.

Ilikuaje: Pesa zangu za kwanza niliwasaidia wazazi wangu-DJ Shiti

uganda

Akizungumza na runinga ya Urban TV, mwanadada huyo ambaye ni mwanabiashara kwa jina Victoria Akao, alisema kuwa lafudhi yake ni kama zawadi kutoka kwa maulana na kwa kweli hajawahi tembelea nchi ya Marekani.

“God does extraordinary stuff, right? So I just woke up one morning and the accent just came on and I was like ‘okay’ and people started saying ‘Hey what’s up with it?’ And I was like ‘I don’t know!’ because I did not even realise I was speaking like this, so its God,” Victoria alisema.

Don’t disappoint our ancestors,’ Mashabiki wamuomba Larry baada ya kurejelea runinga kaa takataka

Mwanadada huyu amenikumbusha slay queens wetu humu nchini ambao hujipatia lafufhi feki kila wanapowaona wazungu kwa minajili ya kuwavutia.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na mungu wake, Victoria alisema kuwa ameokoka.

Tizama kanda ifuatato na utueleze iwapo Victoria anajifanya ama ni ukweli lafudhi yake ni kipawa kutoka kwa mwenyezi mungu.

Tazama kanda hii HAPA

 

 

Uganda: David Obala apeleka nzige bungeni ili kuangazia janga hilo

Video ya mbunge mmoja wa Uganda aliyebeba na kupeleka nzige bungeni imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

David Obala ambaye anaiwakilisha kaunti ya Ngora Mashariki mwa Uganda , aliwapeleka nzige hao bungeni siku ya Jumanne ili kupinga hatua ya serikali ya kuchelewa kuliangazia janga la kukabiliana na mlipuko wa wadudu hao ambao wameharibu mimea katika eneo la Afrika mashariki hatua inayozua hofu ya kusababisha baa la njaa.

Baada ya mbunge mwingine kulalamika, bwana Obala alilazimika kuikabidhi chupa iliojaa nzige kwa afisa wa bunge anayesaidia katika kuweka amani bungeni.

Spika alitaka kuelezewa kila wiki kutoka kwa wizara kuhusu hatua ya serikali ya kuwanyunyuzia dawa wadudu hao.

Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda lilituma ujumbe wa twitter wa video hiyo ambapo mbunge huyo alionekana akiwabeba nzige hao.

Kulingana na Daily Monitor, tayari serikali imenunua lita 10,000 ya dawa ya wadudu hao ambayo hutumika kote duniani kwa unyunyizaji wa angani.

Dawa hiyo inatarajiwa kuwasili nchini humo siku ya Ijumaa kutoka nchini japan , kulingana na maafia katika wizaRa ya kilimo.

Wadudu hao wamedaiwa kusambaa katika wilaya 17 nchini Uganda ikiwemo Acholi, karamoja, Teso na maeneo yaliopo Magharibi mwa mto Nile.

Wilaya hizo ni Abim, Kaabong, Nakapiripirit, Amudat, Agago, Katakwi, Nabilatuk, Moroto, Kitgun, Soroti na Kole miongoni mwa maeneo mengine.

 -BBC

(+Picha)Spice &Sauce! Tazama Ujumbe ambao Msanii wa UG Spice Diana kwa dadake Brenda akisherehekea Birthday yake .

Msanii nyota wa Uganda Spice Diana  jana aliwasha mitandao ya kijamii kwa kuweka picha za dadake na ujumbe maalum wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa . Diana aliandika-

 Happy birthday to my baby sister @brenda_darlingz . You the most annoying creature in my world , but I love you. Enjoy your new age . May God grant you healthy life, n make all your wishes come true.
I like the good girl in you lately 
😉😍

(+PICHA) Bridget Achieng amuekea mwanawe sherehe ya siku ya kuzaliwa

Wengi   walioziona picha za Brenda katika ukurasa wa facebook wa dadake Spice Diana  hata hivyo walizungumzia mnato na urembo wake .  Brenda alipiga pozi kadhaa  ambazo dadake aliweka mtandaoni . Hata hivyo  Diana hakueleza Brenda alikuwa akitimu umri wake .

“We hope this one lasts,”Mashabiki wamwambia Lilian Muli baada ya picha akimpa busu mpenziwe

Tazama picha za Brenda ambazo zimewatoa wanaume Kijasho

Picha za Brenda,dadake msanii Spice Diana
Picha za Brenda,dadake msanii Spice Diana

 

 

Mzee wa miaka 94, wake 19 na watoto 100 aoa tena, kunani ?

Mzee Nulu Ssemakula, raia wa Uganda mwenye miaka ya zaidi 94 na wanawake zaidi ya 19 amezua gumzo kwa kuongeza familia yake kwa kuoa wake wanne tena.

Hata ingawa baadhi ya watoto wake wana wajukuu, mzee huyu anasema bado ana matumaini ya kuwa na watoto zaidi na hata wake wengi zaidi.

Mzee huyu ambaye  alianzisha shule yake binafsi kwa madhumuni ya watoto ambao ni  zaidi za 100.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Ssemakula alielezea kuwa matamanio yake ya maisha ni kuwa na wake  na watoto  wengi kwanikama familia yake kubwa ikitafsiriwa kwa utajiri.

Mwanahabari Aliyekejeli Ushindi Wa Kipchoge Akemewa Mtandaoni

“Kwa bahati mbaya, nimepoteza wake wangu wanne na wengine ambao wanahitaji zaidi ya uwezo wangu, niliwaacha waende. Lakini waliniachia watoto; Bado nitaoa zaidi ikiwa bado nina miaka zaidi na hata nina watoto zaidi. Katika watoto na wake, ndipo ninapopata raha yangu. Huo ni utajiri wangu wa kweli, “alisema.

Kwa sasa, Ssemakula anaishi na watoto wake 66, mdogo zaidi akiwa na miezi 10. Mkewe wa mwisho ana miaka 24 na anatazamia kuongeza familia yake zaidi.

Ssemakula alianzisha shule iitwayo Kiyombero Shule ya Msingi ili kuwakidhi watoto wake wote wanaoenda shule na wajukuu.

Rais Mtaafu Moi alazwa katika Nairobi Hospital

Shadiah Tumuheirwe, mkewe ambaye ni mdogo kwa wote, ni kiongozi. Yeye hupeana maagizo na masharti katika familia.

Mbali na kujenga shule, Ssemakula anamiliki mashine ya kusaga kahawa na nyinginr ya kuhifadhi maziwa kama kitega uchumi na kuleta mapato kwa ajili ya kuimudu familia yake.