PATANISHO: Mke wangu hanipii furaha kwani mimi mnyama?

Lucy kutoka Malindi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Mohammad Ali, akisema ni makosa kidogo yaliyotoke kwa nyumba.

PATANISHO: Mume wangu hata nguo za ndani hanishughulikii

“Naomba tu apigiwe simu nipatane naye niweze kuomba msamaha. Ndio aende tuliwachana asubuhi nikienda kazini na kurudi nyumbani kuandaa chakula cha jioni.

Mzee aliingia na mzigo na kuuweka kwa kiti na nikaupeleka kwa nyumba, kutoka jikoni kurudi nikapata ameuchukua ule mzigo na kuondoka. Sasa sielewi shida ni gani.” Alieleza Lucy.

Kisa hicho kilitokea wiki iliyopita na mwanadada hajui cha kufanya.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na miwili.

PATANISHO: Ndugu yangu alinipeleka kwa polisi nikatwangwa twangwa

“Mipaka umenipitishia kabisa, mimi hutoka na furaha kwenda kusherehekea na bibi yangu kurudi umenuna huzungumzi nami hatuna furaha kwani mimi ni mnyama?” Alisema Ali.

Hatuna furaha yoyote, miaka miwili mimi nawe hatujuani haya basi, mimi sina neno lakini unayoyafanya sina neno.” Aliongeza akiwa na wingi wa msononeko.

Kulingana na Ali, miaka miwili hajapata raha ndani ya ndoa kwani yeye hupakuliwa tu chakula na ndio hivo, hapo aliamua kuondoka.

Mimi mwenyewe nina pressure nina sukari na anaye nituliza ni wewe na sasa nikiona hunishughulikii naenda kutafuta mapumziko kwani maudhiko siyawezi.” Aliongeza mzee.

PATANISHO: Babangu alitutoroka tukiwa wadogo kwa miaka 11