Ronaldo afunga mabao 4 huku Ureno wakiwanyuka Lithuania 1-5

Cristiano Ronaldo alifunga mabao manne Ureno walipowanyuka Lithuania 5-1 katika mechi ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020.

Kiungo huyo wa Juventus sasa amefunga mabao 93 ya kimataifa, 16 nyuma ya rekodi ya dunia ya raia wa Iran gwiji Ali Daei. Matokeo haya yanaiweka Ureno katika nafasi ya kufuzu moja kwa moja, wakiwa alama tano nyuma ya viongozi wa kundi B Ukraine.

Serbia wamepanda hadi katika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo baada ya kuwanyuka Luxemborg 3-1.

PATANISHO: Mke wangu akirudi lazima tuongeze watoto wawili

Kwingineko, Henrikh Mkhitaryan anasema ilimlazimu kuondoka Arsenal ili kupata furaha ya kucheza soka tena, alipojiunga na Roma kwa mkopo msimu huu wa joto.

Alijiunga na Gunners kutoka Manchester United mwaka wa 2018, na kufunga mabao 8 tu kati ya mechi 39 za ligi. Raia huyo wa Armenia, ambaye alifungia nchi yake mabao mawili walipochuana na Bosnia jumapili, anahisi ni kama alikua lazima kwake kuondoka Uingereza ili kupata tena upendo wake kwa soka.

Matumaini ya Somalia ya kushinda awamu ya makundi ya kufuzu kwa kombe la dunia kwa mara ya kwanza yalifikia kikomo baada ya kunyukwa na Zimbabwe jijini Harare.

Tobiko hacheki na mtu hata samaki wakubwa watavuliwa Mau

Ocean Stars walikua na nafasi nzuri baada ya kushinda mechi ya awali 1-0 na kushinda mechi hio kwa mara ya kwanza katika michuano hio. Zimbabwe walianza kufunga baada ya dakika 77 kabla ya Somalia kusawazisha kupitia kwa Omar Abdullahi.

Tukirejea nchini, nahodha wa Gor Mahia Kenneth Muguna ametoa changamoto kwa wachezaji wenzake kuimarisha fomu yao barani Afrika.

Mabingwa hao wanajitayarisha kusafiri hadi Algeria kuchuana na USM Algers katika mkondo wa kwanza ya ligi ya Caf Champions siku ya Jumapili.

Safari za K’Ogalo za dakika ya mwisho, zimekua zikiathiri matayarisho yao.

Kauli ya Siku 11th September 2019

 

Uholanzi kumenyana na Ureno katika fainali ya kombe la ligi ya mataifa

Uholanzi ilitoka nyuma na kuinyuka Uingereza mabao 3-1 katika nusu fainali ya kombe la Ligi ya Mataifa na kufuzu kwa fainali ambako watakutana na Ureno, ambao pia waliwanyuka Uswizi 3-1 katika nusu fainali ya kwanza, mabao ambayo yalifungwa na staa wa Juventus, Cristiano Ronaldo.

Real Madrid imekubali kumnunua Eden Hazard kwa pauni milioni 88

Uingereza walichukua uongozi kupitia kwa mkwaju wa penalty wa Marcus Rashford katika kipindi cha kwanza, kabla ya mlinzi Matthijs de Ligt kusawazisha.

Masihara ya safu ya ulinzi ya Uingereza yalipelekea Kyle Walker kujifunga mwenyewe, kabla ya kosa la Ross Barkley kumpa Quincy Promes fursa ya kufunga bao la tatu.

Fainali hio itachezwa Ureno siku ya jumapili hii katika mji wa Guimaraes.

PATANISHO: Unikome! Utapata mke mwingine anayependwa na mamako

 

Mpira Ukipita Dakika 90 Basi Ni Bahati Nasibu, Alalamika Gidi Shabiki Wa Ufaransa

Siku ya Jumapili, Ureno ilistaimili kumpoteza nahodha wao Cristiano Ronaldo mapema katika mchuano wa fainali ya kombe la euro ili kushinda taji hilo kwa bao moja la dakika za muda wa ziada kwa hisani ya mchezaji Eder, taji la kwanza la kimataifa la taifa hilo.

Baada ya taifa hilo kuandikisha historia dhidi ya wenyeji ambao walikuwa wamepigiwa upato mkuu kutwaa taji hilo, mtangazaji Gidi Gidi alikuwa mwingoni mwa mashabiki waliohuzunika zaidi.

Gidi shabiki sugu wa ufaransa alikerwa na matokeo haya siku chache tu baada ya kujivunia ushindi wao dhidi ya Ujerumani katika nusu finali za michuano hayo akidai kuwa hatopoteza gari lake la Mercedes Benz, laiti angalijua kuwa kichapo chamngoja.

“Ni Monday freshi kabisa, ingawa sio freshi kwa watu wengine kama mimi kwa sababu timu yangu ya Ufaransa ilipoteza fursa ya kunyakua kombe la Uropa”. Alisema Gidi huku akifungua kipindi cha Gidi na GHost asubuhi.

“Lakini mimi huwa nasema ya kwamba, mpira ukipita dakika 90 hiyo nyingine ni bahati nasibu.” Aliongeza Gidi huku akiwapongeza wareno kwa ushindi wao mkuu licha ya kuwa na uchungu mwingi.

Skiza kanda ifuatayo.