‘Alinipiga matiti pasi ndio wanaume wasiniangalie’ Asimulia ‘utamaduni’ wa Cameroun aliofanyiwa na shangazi yake

Utamaduni au mtindo wa kupiga matiti pasi ili kuyazuia yasiwe makubwa umekithiri afrika magharibi na hasa nchini Cameroon . Wanaotekeleza  hilo hudai kwamba hatua ya kuzuia kukua kwa matiti ya wasichana wanaoanza kubaleghe huwazuia kuwavutia wanaume na hivyo basi kuepuka dhulma za kimapenzi lakini  jambo hilo limetajwa na wanaharakati kama ukiukaji wa haki za wasichana na dhulma kwa waathiriwa.

Ni kama torture! Harusi na honeymoon zilizoishia katika quarantine

Kabla ya masimulizi ya  Jane  Mbithi mwenye umri wa miaka 32 sasa kuibuka, wengi nchini  hawana ufahamu iwapo kuna utamaduni kama huo. Jiwe hutiwa motoni kama kaaa kisha kupitishwa juu ya matiti kwa lango la kuyapunguza. Jane alifanyiwa  utataribu huo  miaka 18 iliyopita  na shangazi yake ambaye alikuwa Mtawa(Nun) na alikuwa akiishi Cameroun wakati huo . Alipokuja nyumbani kwa likizo alimpata Jane akiwa ameanza kubaleghe na matiti yake yameanza kujitokeza, yakionekana kupitia nguo yake. Shangazi yake hakufurahia hilo na mara moja akamuambia mamake jane kuhusu  hatari ya mwanawe kubakwa na wanaume na hivyo basi kuliwa na haja ya kuyapunguza matiti yake. Mamake alishangaa  hilo litafanywaje lakini shangazi yake kwa ajili ya kuwa mtawa aliheshimiwa sana pale bomani na kila alichosema kilikuwa sheria. Alieleza jinsi utaratibu huo utakavyofanywa na muda sio mrefu, kila jane alikuwa akivumilia takriban dakika 20 za uchungu wakati jiwe la moto lilipokuwa likiwekwa kifuani mwake ili kupunguza kiasi cha matiti yake .

PESTLE

Wenzake shuleni walishangaa mbona alikuwa akilia wakati wote na kushika kifua chacke kwa uchungu. Wengine kama  rafiki yake wa karibu Stella alishangaa mbona  hawakuwa wakioga pamoja kama awali bila kujua kwamba Jane alikuwa akificha  alama katika kifua chake na kupungua kwa matiti yake kwa ajili ya uovu aliokuwa akifanyiwa na shangazi yake kutumia mila aliotoa Cameroun .

Visa 4 vipya vya COVID-19 vimeripotiwa, idadi yafika 42- Mutahi Kagwe

Alipokuwa msichana  mkubwa kujiunga na  chuo kikuu, Jane alijipata na matatizo ya kujiamini kwa sababu alijiona na kujihisi tofauti kama wasichana wenzake. Wengine walikuwa wakimfanyia mzaha kwa kumuita ‘mvulana’ kwa sababu ya kukosa matiti bila kujua masaibu aliyopitia . Jane hakuweza kumchukulia hatua yoyote shangazi yake kwa sababu uamuzi huo pia ungemuingiza taabani mamake ambaye alikuwa  amekubali  afanyiwe utaratibu huo . Walimuambia wakati huo kwamba kila wanachofanya ni kwa manufaa yake bila kujua athari za kitendo  hicho katika maisha yake  ya baadaye .

PESSTLE 2

Nchini Cameroun ambako utamaduni huo umekithiri, serikali na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yanapambana na  uovu huo ili kuzuia mateso kwa maelfu ya wasichana. Kupiga matiti pasi ni zimwi kama utamaduni wa kuwakeketa wasichana katika baadhi ya jamii za humu nchini. Athari za kitendo hicho kwa Jane hazitaisha hivi karibuni na zinamuathiri hadi wakati huu katika maisha yake ya utu uzima .

 

 

Shock!Siku niliyotakiwa ‘kulala’na maiti ya mume wangu kabla hajazikwa

Nduku  Nzilani hakuweza kutabiri yatakayomfika wakati penzi lake tamu ambalo lilianza kunawiri katika chuo kikuu  akiwa nje ya taifa na mkenya mwenzake  kutumbukia kuwa tukio la kumpa huzuni na majonzi tele .

‘Niliacha ukahaba baada ya babangu kuja lodging’

Akiwa na umri wa miaka 24 wakati huo nchini Australia  akisomea  Sheria ,Nduku alikutana chuoni na mkenya mwenzake ,kijana mtanashati sana na mpole kutoka Ukwala ,Siaya . Iwapo umewahi kuishi nje ya Kenya unaweza kufahamu hisia hii ya kuwa mbali na nyumbani kasha ukutane na mtu ambaye yuatoka Kenya .Ni  jambo zuri san aka sababu mnaweza kuzungumza mengi kwa wakati mmoja ikaonekana ni kana kwamba mmejuana maisha yenu yote .Hivyo ndivyo ilivyokuwa kati ya Nduku na   Derick Ochola.‘Kila kitu kilikuwa sawa tulipokutana  na nilijua kuanzia mwanzo kwamba huyu diye ninayemtaka kama  mpenzi wa muda mrefu’. Anasema Nduku . Ochola  naye hakuchelewa kwani  baada ya kukutana hapa na pale  chuoni alimtaka waweze kupatana pia nje ya chuo ,na ikawa rasmi kwamba walikuwa wanapendana hivyo basi shughuli zao nyingi wakawa wanazifanya pamoja . Alipowajulisha jamaa zake wakati wa likizo kwamba amekutana na  mkenya mwenzake ambaye wamependana na wanapanga kufunga ndoa baada ya masomo yao ,familia nzima ilijawa furaha  na kweli wakati huo kila kizuri cha maisha kilionekana!

Mwanamme Kamili? Jamaa akiri kuwa na bibi WATATU huku wawili kati yao wakilala pamoja naye katika kitanda kimoja!

Baada ya miaka miwili ambapo wote sasa walikuwa wamemaliza kusoma na kupata kazi ,walikubaliana kurejea Kenya ingawa kwa muda kidogo Nduku alibaki Australia . walifunga ndoa ya kanisani wakiwa ng’ambo nan i jamaa zao wachache  ndio walioweza kuishuhudia ndoa hiyo ingawaka walituma picha na kanda za video kwa wengi wa waliokuwa Kenya wakati huo . Ilikubaliana kwamba wangefanya harusi nyingine wakiwa Kenya na pia kufuatilizia na hafla ya kitamaduni ili kuashiria sasa kwamba wamekuwa mke na mume na hayo yakafanyika wakati wote walipokuja Kenya .

Uchawi?‘Niliambiwa nitayarishe uji wageni wanakuja,Kumbe ni Nyoka aliyefaa kunywa uji!’

Kwa bahati mbaya miezi   sita  tangu waje Kenya kuishi na kuanza familia yao nyumbani ,Ocholla alihusika katika ajali ya barabarani wakati gari alilokuwa  akiendesha  kugongana na  trela  kwenye barabara kuu ya Nairobi kwenda nakuru na ilikuwa kipindi cha pasaka 2016. Nduku hakujua kuhusu kifo cha mumewe hadi alipoona kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watu waliofariki kwenye ajali iliyotokea  eneo la kabati .Kilichomshika jicho ni rangi ya mojawapo ya magari yaliyohusika kwenye ajali hiyo-gari  dogo jekundu..na kwa hofu yake akaiangalia picha ile kwa karibu ili kuona nambari ya usajili na hapo ndipi ulimwengu wake ulizima kwa dakika kama tano.Hakuweza kupumua waka kuzungumza na akasalia kama bubu asijue cha kufanya . Alipopata ujasiri kitu cha kwanza alichofanya ni kmpigia mume wake simu lakini haikukereza kwani alikuwa mteja.

Nusura nijitie kitanzi,Asema Maureen Waititu

Hakuhitaji tena ufafanuzi kwamba alikuwa mjane .mume wake alikuwa ashafariki  na  hilo likathibitishwa na shemeji yake ,kakake mumewe ambaye alimpigiasimu akimueleza anakuja kumchukua hadi Nakuru wautambue mwili kasha matayarisho ya kumzika yaanze.Safari ya huzini ,simanzi na mshangao ilikuwa ndio imeanza kwa Nduku.  Kwa ufupi ,kando na kuomboleza kifo cha mumewe  kabla ya maazishi Nduku aliarifiwa kuhusu  mila za watu wa akina mumewe na hakuelewa kilichokuwa kikifanyika  hadi   mkesha wa kuzikwa kwa Ocholla. Nduku aliambiwa kwamba atalala katika chumba kimoja na mwili wa mume wake  na wakati wa mchakato huo ,anafaa kupata ndoto ya kushiriki tendo la ndoa naye.Maskini mtoto  kutoka Matuu ,alishangaa ,akashindwa la kufanya lakini kaambiwa huo ni utamaduni wa jamii ya  Waluo . Siku za jadi wajane katika jamii hiyo walitakiwa kufanya hivyo  kabla ya waume zao kuzikwa  ili ‘wasafishwe’ kwa matayarisho ya kurithiwa.

Mume wangu alishiriki ngono na mamangu mzazi ,mwanamke asema

 ‘Niliambiwa kwamba  endapo ningepata ndoto  ya kushiriki tendo la ndoa na mume wangu kabla hajazikwa basi ningekuwa huru  na tayari kuolewa tena’ anasena Nduku .

Anaongeza ‘ Iwapo ndoto haingekuja  basi njia nyingine ya tambiko ingetumiwa  ili kunifanya niwe ‘msafi’ kabla ya maazishi’

Ili kufupisha masimulizi yake ,hakuna aliyemtayarisha Nduku kwa yote yaliomfika kuanzia kifo cha mume wake na utamaduni wa watu wake.Alipokuwa hai alikuwa akimdokezea baadhi ya mila hizo lakini kwa sababu alikuwa msomi ,Ocholla hakuwa akizipa uzito sana mila za watu wa jamii yake lakini palipo na wazee ,utamaduni hausahaulikwi hivi hivi .Je,ni zipi mila  za jamii nyingine ambazo kwako umeziona kuwa na kushangaza? Ungefanya nini iwapo unhejipata katika hali ya Nduku?