Doktari! Karibu nyumbani, Vera ni ‘wife material’ usiwe na hofu. Wasema wakenya

NA NICKSON TOSI

Mwanasosholaiti Vera Sidika ni kama amepata mtu wa kumdekeza vyema raundi hii akiwa daktari kutoka Nigeria, miezi michache tu baada ya kuwachana na Jimmy Chansa kutoka Tanzania.

Amekuwa akitundika picha kwenye mitandao ya kijamii na jamaa huwa wa asili ya Nigeria kwa jina Tommy Daniel , nyingi ya picha hizo akiwa anazitundika kwenye Instagram na kumuita majina ya kumsifia kama cute.

Vera Sidika and Tommy

Tommy ni mwanagainagolojia na mwanamitindo wa zamani aliyekuwa anafanyia kazi hiyo Dubai.

Tommy alituma ujumbe huu kwenye Instagram yake, ujumbe uliokuwa unamwelekea Vera.

 Kuwa salama huko uliko, aliandika Tommy
 Vera kwa upande wake alijibu kwa madaha akaandika hivi.
Asanti hun🥰❤️😘.
52_vera-sidika-2-640x426-640x426

Baada ya wakenya kuona jumbe hizo walikuwa na haya ya kuandika katika mitandao mbailmbali.

 

gw374580 @queenveebosset soo mliachana na bwanako wa tanzania?

shishythemodel Wueeehh ninani anayeona hiihahah @timmytdat ujaluo shuma ni doshi🤣🤣😆😆

 

 catekaddy @queenveebosset doctari mwingine?no, jaribu a shamba boy Vee.

 

Mimi siwezi kustahimili mahaba ya taabu! Vera Sidika Afunguka

NA NICKSON TOSI

Mwanasosholaiti Vera Sidika ameamua kubwaga manyanga siku chache to baada ya ripoti kujiri kuwa amewachana na mpenziwe kutoka Tanzania Jimmy Chansa miezi sita baada ya kuwa kwa uhusiano.

Kutokana na kisa hicho, pamekuwepo mabishano baina ya Vera na mfuasi wake kwa jina Halima kwa kile shabiki huyo amesema ni mwanadada huyo kuranda randa bila ya kukaa kwa uhusiano na mwanamume mmoja.

Halima aliandika hivi katika ukurasa wake;

“Twafahamu kuwa wewe ndio shida, si wanaume,”aliandika Halima.

Baada ya Vera kuona ujumbe huo, alionekana mwenye hamaki na kumjibu kwa kusema haya.

“Halima mimi siwezi kustahimili uhusiano ambao ni kama sumu eti ninajaribu kumfurahisha mtu, unaweza fikiri yale unayodhani lakini mwisho wa siku ni kuwa ni mimi nitafanya uamuzi wa maisha yangu. Kama unafurahishwa na hayo sema kwa sababu watu wamejaa kwenye mitandao kusema ya wengine ilhali yao imewashinda, sitawahi kuvumilia ujinga maishani mwangu mimi, nitachagua kilichokizuri kwangu na kibaya kukiachilia,” alimjibu Vera.

52_vera-sidika-2-640x426-640x426

Vera aidha hakuweza kufafanua iwapo mapenzi yake na Chansa na Otile Brown yalikuwa na shida zipi kwani alionekana  kana kwamba alikuwa kuzungumzia mahusiano hayo. Uhusiano wake na wawili hao ulidumu kwa takriban miezi 6 kila mmoja.

vera

Mwaka 2017 Vera alitengana na mpenzi wake kutoka Nigeria kwa jina Yomi ambaye alikuwa amejongea kisima cha asali cha Vera kwa miaka 2 wengi wakadhani ya kwamba labda wangeoana lakini wakatengana .

 

 

 

 

 

Aliyefanya kitendo hiki hatawahi ona mlango wa Mbinguni,Asema Vera Sidika

NA NICKSON TOSI

Vera Sidika amejikuta katika njia panda baada ya wanannchi kutumia picha zake akiwa nusu uchi kueneza jumbe za kutaka watu wazingatie usafi kama njia ya kukabili virusi Vya Corona.

Alhamisi mwanasosholaiti huyo alituma picha katika mitandao ya kijamii akijiuliza maswali ni kwanini watu waliamua kutumia picha yake  visivyo, anasema picha hiyo ilikuwa imeandikwa onyo kuhusiana na hatari ya kushika usoni kwa mikono chafu.

Kuna hii picha inayozagaa katika mitandao ya kijamii ,aliyefanya hivyo hatawai ona mlango wa kuingia mbinguni kamwe 😂🤣😂 ❤️  🤣”aliandika Vera.

Vera-Sidika

Picha hiyo ilikuwa na maandishi usijishike macho,mapua namdomo kama hujaosha mikono, kaa nyumbani kama uko na dalili zozote za Corona, maandishi hayo yalimfanya Vera kuwa na hamaki kwani anahisi kuwa picha yake ilitumiwa visivyo.

vera-sidika-thirst-trap1-480x600

Wakenya walikuwa na haya ya kusema kuhusiana na picha hiyo katika mitandao ya kijamii.

romyjons “Tungetengeneza picha kama za GIG alafu ttuewaambie wananchi wanawe mikono mara hiyo.”

willisraburu “🤣🤣🤣🤣”

naughty_bree “🤣🤣🤣🤣🤣”

brandprintkenya “Chukua io COAT of arms apo upelekee watoto wako nyumbani 😂😂😂”

martinkihia “Wacha tunyonge nyani  na hii🙊🙊”

nyaikafrank370 “Ona sasa umenitobolea [email protected]

Mnapayuka nini?wacheni kulaumu rais Kenyatta! asema Vera Sidika

NA NICKSON TOSI

Mfanyabiashara maarufu kutoka Kenya Vera Sidika sasa amejitokeza na kuwashtumu wakenya kwa kile anasema haikuwa makosa ya raids Kenyatta kuruhusu ndege ya kutoka Uchina kutua nchini.

Kwa mujibu wa Vera ,kupigwa marufuku ndege kutoka eneo moja si suluhisho kwa kuzuiya virusi vya Corona bali taifa lilifaa lipige marufuku kuwasili nchini kwa ndege kutoka mataifa ya kigeni,hatua ambayo labda ingesaidia kuzuiya mkurupuko wa virusi hivyo nchini.

“sasa watu wengi wamekuwa wakimlaumu Rais Kenyatta kwa kuruhusu ndege kutoka uchina kutua nchini,nimekuwa nikijadili na watu ambao wamekuwa wakionelea eti ndege hiyo ndiyo iliyochangia Corona kutua nchini,maoni ambayo ni upuzi kwangu,kwa kweli iwapo kuna kitu ambacho kilistahili kufanyika ni kupigwa marufuku kwa ndege zote kutua nchini.Maoni ya Vera Sidika

VERA

Its dumb to blame the president for letting the China plane into the country – Vera Sidika

Yanajiri haya baada ya Vera kutuma ujumbe wa jumbe alizokuwa ametumiwa na rafikiye zilizokuwa zinadai kuwa iwapo ndege hiyo ingekatazwa kutua nchini basi tungekuwepo na mgogoro wa kidiplomasia baina ya Kenya Uchina.

Vera aidha alimfahamisha jama huyo kuwa Corana haikuwasilishwa na ndege wala kutoka katika taifa la Uchina na kuongeza kuwa iwapo hata serikali ingezuiya kutua nchini kwa ndege hiyo basi mtu kutoka Uchina angesafiri kutoka Uchina hadi Uingereza na kutua nchini akiwa na virusi hivyo.

Its dumb to blame the president for letting the China plane into the country – Vera Sidika

Kwa sasa ndege za Uchina zimezuiya kutua Kenya lakini hiyo iliyotoka Uingereza ilikubaliwa na kuwabeba waliokuwa wameathiriwa na virusi hivyo,huwezi kabiliana na tatizo hilo kwa sasa,na watu waache kulaumu serikali.alidai Vera

Vera-Sidika

Penzi la Pesa tu ,Vera na ‘mpenziwe’ waachana

NA NICKSON TOSI

Mwanasosholaiti na mfanyabiashara Vera Sidika ametia kikomo katika mapenzi yake baina ya mchumba aliyekuwa amemtambulisha kwa umma wiki mbili zilizopita.

Jimmy Chansa na Vera wamekuwa wakiibua hisia mseto haswa miongoni mwa wafwasiwao katika mitandao ya kijamii baada ya kufuta picha walizokuwa wamepiga wakiwa pamoaja.

Utafiti tulioufanywa katika mitandao ya kijammi yao ,tumebaini kuwa Jimmy amefuta picha zao zote walikuwa wamepiga wakiwa pamoja katika maeneo ya kujivinjari na Vera swala ambalo limeibua hisia mseto miongoni mwa wapenzi hao wawili.

Sidika vile vile aliamua kufuta picha hizo katika mtandao wake wa kijamii .

Vera Sidika with her new boyfriend Jimmy Chansa,

Siku chache baada ya wapenzi kusherehekea siku ya wapendanao ulimwenguni,Vera na Jimmy walionekana kama watu waliokuwa wametofautiana  kwani ,hakuna picha zozote walizoweka katika mitandao yao ya kijamii.

Vera kwa upande wake aliandika hivi kwa mtandao wake wa kijamii.

 “ Happy Valentines Day Sweethearts. I love y’all with all my heart ❤️

Mgeni njoo mwenyeji apone: Saumu Mbuvi ajiandaa kukaribishwa mtoto wa pili.

Septemba mwaka jana Vera aliyekuwa anaogelea katika dimbwi la mapenzi na Jimmy ,alimjuandikia jama huyo ujumbe wa kutoa nyoka pangoni wa penzi siku ya kuzaliwa kwake lakini jumbe huo ulifutwa saa kadhaa baada ya kuandikwa.

“Happy Birthday to the most handsome man in the World. My King My Dr. Bae On your special day I pray that the ground you walk upon will forever bring you blessing. The sky above will forever release favour on you. The breeze around you will forever blow peace. Happy birthday my love @iamjimmychansa I love you” AlisemaVera Sidika

Vera Sidika and Jimmy Chansa

sVera baada ya kudhiniishia umma kuwa alikuwa na uhusiano wa kimahaba na Jimmy ,aliwaonya paparasi wanaopenda udaku kukimia na kuangazia maisha yao mbali na yake.

‘The same people claiming they are waiting for break up drama are the same who said they are waiting for break up with Senegalese guy… but they never saw it. Just because it happened before doesn’t mean it’s a pattern. There’s reasons to why things happened that way, during that time and none of you all will ever understand. So keep waiting for break up drama that will never come,” aliandika  Vera.

Vera with her new boo (Instagram)

Shika mbele ya Umma: Vera Sidika amwambia mpenziwe

Kabla hata mawingu ya Siku ya kusherehekea Valentino hayajafunguka,mwanabloku na ‘mfanyabiashara’Vera Sidika aliandikia mpenziwe ujumbe akimwambia anaweza mpusu ,kumshika mahali anaitaji mbele ya watu ikiwa ni nia mojawapo ambayo anaipenda sana wakati anahisi hamu ya mapenzi.

Vera alisadiki kuwa lugha yake ya mapenzi ni kutaka mwanaume kumhisi kila siku,kila mahali,na popote pale anapohitaji.

Image result for vera photos

Vera na mpenzi wake huyo  Jimmy Chansa palikuwepo na uvumi mkuwa wameachana baada ya kujivinjari wakiwa Mombasa  na hata kukosa kutuma picha zao za mahaba katika mitandao yao.

Jimmy hata hivi alisema kuwa Vera alikuwa amemwacha bila ya ufahamu wake .

Image result for vera photos

Katika ujumbe wakati kabla ya siku ya kusherehekea Valentino,Vera anamweleza mpenziwe kuwa yeye anapenda kutunzwa kama malkia.

Huu hapa ujumbe wenyewe.

Love me an affectionate man. Always hold my hand, waist, give me forehead kisses, PDA. Just touch me anywhere and everywhere and I will be drowning in love,” Aliandika Vera

Image result for vera photos

Hata hivyo Vera amekuwa akiwachanganya wafwasi wake haswa baada ya kuonekana na mwanamziki wa Nigeria Burnaboy ambaye walionekana pamoja katika hafla moja USA .

Image result for VERA AND BURNA BOY PHOTOS

Sababu ya Vera kuibadilisha rangi yake

Vera Sidika amekuwa majadiliano ya mji sasa kwa wiki nzima baada ya kuibadilisha ngozi yake na kuwa nyeusi.

Vera alisema, “Kamwe usikubali kufafanuliwa na maisha yako ya hapo awali, kwani ilikuwa tu ni funzo si hukumu ya maisha.”

Alipata maoni mengi mazuri na, bila shaka ya, upinzani.

Mmoja alisema, “Mabadiliko ya Vera ni makubwa kuliko unavyoyafikiria! Unawahimiza wanawake wadogo kujipenda vile walivyo. Pongezi Vee.”

“Sonko ni mtanashati na ninampenda,” asema Zari

Hata hivyo, hivi ndivyo Vera alivyoibadilisha rangi ya ngozi yake. Alinunua bidhaa itwayo tan ambayo huenda kwa Sh4,000 hadi Sh13,200, moja ikiwemo Bondi.

Sands Self Tanning Mist, ambayo inapatikana kwa Sh 13,200.

Kulingana na wataalam, unapojipaka ‘tan’, indumu siku nne au tano na unapopokea matibabu ya ziada, inadumu siku saba au nane
kabla ya kufifia.

Vera alikuwa akiukuza wimbo wake mpya unaojulikana kama Mimi, ambao unasema dhidi ya ubaguzi kulingana na rangi ya ngozi.
Soma mengi hapa –> https://radiojambo.co.ke/

Willy Paul na mapya ! Sahau minenguo na Nandy sasa

Staa aliyejawa na utata kutoka hapa nchini Willy Pozze sasa amechapisha picha na kipusa freshi kwenye mtandao wake maridhawa wa instagram. Katika chapisho hili la kizazi, Pozee anaonekana kwenye mapozi hatari na mrembo kutoka hapa nchini Verasidika.

Soma hapa:

Baada ya Wema kufungwa jela, mamake Mondi atume ujumbe

Tazama Hapa:

View this post on Instagram

Goodnight from we!!!!

A post shared by W.I.L.L.Y.P.O.Z.Z.E (@willy.paul.msafi) on

Kulikuwepo na habari zilizoteka mitandao kuwa huenda staa huyu amehama kufanya muziki wa kidunia ila hajaweza kutangaza rasmi. Mwenzake Bahati katika mahojiano amenukuliwa kuhakikisha anamuombea muimbaji Willy Paul.

“Nitamuombea sana. Ni ndugu yangu. Ni imani atarudi.”  alisema Bahati.

Pata uhondo:

Je, unakubaliana na Bahati kumhusu Willy Paul?

Ikumbukwe kuwa Vera ni mwanamitindo na mwanadada mjasiriamali. Katika posti hiyo, Pozze anawatakia mashabiki wake usiku mwema.

View this post on Instagram

………. IN TOWN

A post shared by W.I.L.L.Y.P.O.Z.Z.E (@willy.paul.msafi) on

Kiki kama hizi za mapozi na wanamitindo zilikuwa naye staa Otile Brown kipindi anatoka kimapenzi na Vera. Huenda ikawa Willy Paul anapania kufanya kiki kama hizi?

Katika mahojiano na muimbaji wa muziki wa injili Hope Kid, staa huyu alikiri kuwa kiki zinasaidia kuukuza muziki sio ata nchini bali ata mataifa mengine