Maadhimisho ya miaka 10 ya Diamond Platnumz kwenye muziki, mchango wake

Msanii wa kizazi kipya na mkurugenzi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz anatazamiwa kufanya bonge la tamasha mjini Kigoma ili kuadhimisha miaka 10 ya uchapakazi katika tasnia ya muziki.

Sherehe hii itafanyika kwao Kigoma na ameweza kuwaalika wengi ili kuwapa burudani tele.

Lebo ya WCB yang’ara nyimbo 4 bora afrika mashariki 2019

Kama kawaida safari yoyote huwa imejaa milima na mabonde na wakati mwingine wengi hukatishwa tamaa.

Diamond ameweza kuipamba sherehe hii na kuita mastaa wengi Tanzania.

Aidha, staa huyu ameanzisha hashtegi kwa jina #Twezetu Kigoma ili kuwavuta wengi ukumbi wa Kigoma.

Wanaume mashuhuri wanaojivunia kuwa wazazi

Safari ya muziki ya nyota huyu wa bongo fleva ilianza mwaka wa 2009 na kufikia sasa amepiga hatua kubwa pamoja na kuupeleka muziki wa afrika mashariki katika upeo wa juu zaidi.

Diamond ameweza kutoa mchango mkubwa katika jamii huku akiwatoa kimuziki mastaa kama Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Mbosso pamoja na Lavalava.

Kando na mchango huo wa kupigiwa mfano , Diamond ametengeneza ajira kwa wanahabari kwa kuanzisha kituo cha redio na runinga Wasafi FM na Wasafi TV mtawalia.

 

Hatua kubwa alizozifanya Konde Boy baada ya kuitema Wasafi

Miezi imepita sasa tangu staa wa muziki nchini Tanzania aiteme lebo ya WCB.

Maendeleo na nyota katika kazi za staa huyu zinaonekana ziking’aa tofauti na wapinzani walivyodhania.

Harmonize ameweza kuoa Sarah mrembo mwitaliano na hakuwashirisha mastaa wenzake wa kundi la Wasafi.

Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize anazidi kung’ara hata zaidi.

Soma hadithi nyingine;

Yaliyomo: Hali tete Kakamega, jumba laporomoka na kuua watu (+Picha)

Konde Boy ameteuliwa kushindania tuzo ya mwanamuziki bora wa Afrika katika tuzo za muziki za MTV Ulaya.

Mastaa waliokuwa wanabishana levo moja ni Nasty C na Prince Kabyee, Toofan, na Burnaboy kutoka Naijeria.

” Mfalme Kijana wa Muziki Afrika Mashariki , #KondeBoy @harmonize_tz ameteuliwa kwa tuzo kitengo cha mwanamuziki bora wa Afrika 2019 MTV EUROPEAN MUSIC AWARDS,” uliandikwa ujumbe wa MTV Africa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Kupitia uteuzi huu, Harmonize anaweka rekodi ya staa wa kipekee kuteuliwa katika ukanda wa Afrika Mashasriki na kati.

KondeBoy akitwaa ushindi katika tuzo hizi atakwenda sawa na aliyekuwa bosi wake.

Soma hadithi nyingine;

Jacque Maribe alamba dili nono baada ya kuitema runinga ya Citizen

Inaonekana kuwa nyota ya staa huyu inazidi kung’aa baada ya kutema lebo iliyomkuza.

Meneja mmoja wa WCB Sallam SK alitangaza kuwa staa huyu bado yupo WCB kimkataba.

“Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi,”

Soma habari za Abraham kivuva

Rayvanny adondosha Remix ya Tetema na mastaa wakubwa Afrika

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rayvanny amedondosha remix video moto ya wimbo wake Tetema.

Kwa sasa Remix mbili zimefanyika za ngoma hii iliyotikisa Afrika nzima.

Katika kuhakikisha kuwa ameiteka soko la muziki Nigeria, Rayvanny amemshirikisha staa wa Nigeria Patoranking.

Dakika 5 tu niage dunia, Msanii wa nyimbo za injili Roz Haki afunguka

Image result for tetema remix

Maneno yaliyotumika katika ngoma ya kwanza ya Tetema yalionekana machafu hivi kupelekea kufungiwa kwa wimbo huu hapa nchini.

Remix hii imewaleta pamoja Patoranking, Zlatan na Diamond Platnumz.

Ngoma hii inadondoka huku acapella ya Naogopa ikikubwa na ubishi baina yake na msanii chipukizi kutoka mkoa wa Iringa.

Image result for rayvanny patoranking

Aidha, Rayvanny ameshikilia kuwa Naogopa ni wimbo wake.

“Naogopa ni wimbo wangu. Ni utunzi wangu. Kila kitu nimeiandika mwenyewe. Nafikiria huyo dogo popote alipo anajua….” Aliendelea kuongea

Msanii huyu ambaye anafahamika kama Jimmy Msagala amesema aliamua kuufanya wimbo huu baada ya kumuona Rayvanny amelegea.

(+ Picha) Hali halisi, Usahihishaji wa KCSE wasitishwa kituo cha Machakos

“Nilidhani kuwa Ray hana time nayo. Nikafika mkoa maeneo yangu ya kujidai na kuifanya nyimbo. Ni kweli ni kuwa nyimbo sio ya kwangu nyimbo ni ya Rayvanny…” Jimmy Msagala aliiambia Bongo 5.

Video hiyo ya dakika dakika 4 na sekunde 16 imefanywa na Cardoso Imeges.

Kupitia kibao hiki, Rayvanny ametimiza usemi wake wa kuifanyia Tetema remix na wasanii wakubwa Afrika.

Lebo ya WCB kutumia uganga kuzuia mvua Dar Es Salaam, Babu Tale

 

Boss Tale amefungukia Bongo 5 kuwa wanafanya wawezalo ili kuzuia mvua isinyeshe.

WCB ina fiesta kubwa sana Dar Es Salaam ambayo itakuja mastaa kama Wizkid, Tiwa Savage kati ya wengineo.

‘Nikwambie hapa tulipo tunahangaika sana kupigia waganga simu.”

“Unawaza nani anakuzuilia mvua so tunatoka nje ya box…”

“Its normal we are African, ata wewe unafanya usininyoshee kidole…” Alisema Boss Tale.

Unajua yepi kumhusu mbunge mteule Imran Okoth? Soma hapa

Tale alikuwa anazungumzia harakati wanazofanya ili kuhakikisha fiesta ya Wasafi katika uwanja wa posta imekuwa shwari.

Aidha, Tale amefunguka jinsi muziki unavyolipa hela kibao huku akimtaja Diamond Platnumz kama mtu anayependa kuwekeza.

“Diamond anaweza kuwekeza hela kwa msanii bila kuogopa lolote …”

Tale ni mojawapo wa mameneja wa lebo ya WCB akiwemo Sallam SK na Mkubwa Fella.

Tale amesema kuwa anamwangalia Fella kama ndugu yake.

Ametaja mchango mkubwa zaidi wa Fella katika muziki wa Bongo Fleva.

Haya yanajiri huku Mondi akiangusha ngoma kubwa ya Baba Lao itakayokonga nafsi mashabiki wao fiesta la Kijitonyama.

Ngoma hii ilileta utata na kufanana na Soapy ya Naira ila S2Kizzy akaweka wazi.

(+Video ) Boni Khalwale shujaa wa kurusha mawe, achangamsha Twitter

Producer huyu wa mkwaju wa ‘Baba Lao’ ya Mondi ametokezea na kufunguka kuhusu midundo ya ‘Baba Lao’ na ‘Soapy’ ya Naira kufanana.

Akihojiwa na kituo cha Wasafi FM nchini Tanzania, S2Kizzy amesema kuwa waliomba ruksa ya kuimba na mdundo huo.

Producer huyu ameeleza kuwa alivutiwa zaidi na mdundo wa Naira katika ngoma ya Soapy.

Bifu mpya ya Harmonize na media za Kenya, akejeli kikao cha wanahabari

Kikundi cha wanahabari nchini kimeachwa na mshangao mkubwa na kudai kuwa Harmonize alionyesha dharau kubwa kwao.

Staa huyu alitalii nchini katika mchakato wa kupigia debe nyimbo yake mpya ya Uno.\

Harmonize ambaye amepanga msururu wa safari katika nchi mbalimbali kuipa nguvu ngoma hii alisubiriwa na wanahabari hao kwa masaa mengi.

Babu Owino akosekana mkutano wa ODM Kibra, sababu zatolewa

Konde alizungumza kwa dakika 3 na kuondoka na kuwaacha wanahabari.

Jeshi alitakiwa kuhutubia kikao hiki cha wanahabari kabla kuendelea na safari yake.

Katika ziara hii, Harmonize C.E.O wa Konde Gang anapania kuipeleka nyimbo ya Uno hadi iwafikie watu wa tabaka mbalimbali.

Ngoma ya Uno inafanya vizuri katika mtandao wa YouTube muda mchache tu baada ya kutoka.

Harmonize alianza safari hii na gang yake nchini Tanzania.

Alionekana kufunguka zaidi katika mahojiano na vituo vya utangazaji nchini humo tofauti na hapa Kenya.

Janet Mbugua aeleza A-Z masaibu ya kuitema Citizen, asema sio dili freshi

Alimwaga mtama wote A-Z kuhusu lebo ya WCB na baadae akafanya party kubwa ya wanahabari huku akiperform Uno.

Kikao chake na wanahabari Kenya kilisubiriwa saa tano mchano na baadae akasukuma hadi saa tisa alasiri.

Kikao hicho baadae kilisongezwa hadi saa moja jioni. Hii ina maana kuwa wanahabari hao walimsubiri siku nzima.

Je, unadhani ni kitu gani kilimfanya Mmakonde huyu kuwazimia data wanahabari Kenya?

Kama desturi za vikao hivi, wanahabari walikuwa washatua eneo la Blue Door VIP lounge kumsubiri staa huyu.

Kwa tendo la kejeli zaidi, walinzi wa staa huyu walisukuma viti na kumpisha atoke kwenye kikao.

(+Video yavuja) Babu Owino anywesha mtoto supu, avunja dhana potovu

Mtangazaji wa runinga alikerwa na kiburi hiki na kusema,

“Huyu jamaa ako na madharau sana, hutawahi niona kwa event ama press conference yake tena”

Mwingine aliongeza,

“Hivi sivyo mtu anavyopaswa kuishi na watu, hususan vyombo vya habari. Atajua hajui. Kiburi chake hakiwezi kumpeleka mbali. Hakuna siku moja hivi nitafika kuangazia chochote kinachomhusu…”

 

 

(+ Video) Mahangaiko ya Harmonize, Je lebo ya WCB inamnyanyasa ?

Harmonize amesimulia mahangaiko anayopitia baada ya kutangaza kuitema lebo kubwa Afrika Mashariki y WCB.

Katika mahojiano na Clouds, staa huyu amesimulia jinsi amelazimika kuuza nyumba zake kulipa Milioni 22.5 anazodaiwa na lebo ya Wasafi.

Uongozi wa WCB sasa unamtaka alipe hela iliyotumika kurekodi muziki wake na zaidi ya hapo kununua hatimiliki za jina la Harmonize.

Ikumbukwe kwamba staa huyu anayetamba na mkwaju wa UNO hakuwa na jina hilo alipoingia Usafini (WCB)

Jina la Harmonize , Harmonize mwenyewe ni mali ya WCB kulingana na meneja wa Diamond Sallam SK.\

Kufikia sasa Konde Boy ameuza nyumba zake mbili katika juhudi za kumaliza mkataba wake freshi bila matatizo.

“Nimelipa kiasi lakini mpaka hivi sasa bado nadaiwa na sijamalizia kulipa ila bado kiasi kidogo sana cha kumalizia hela hiyo,” Harmonize alidokeza.

Sikuwa na hela, kwa hivyo nikauza baadhi ya ninavyomiliki. Kuna sehemu nilikuwa najenga nyumba zangu 3, nililazimika kuuza. Nilifanya hivo kwa sababu pesa sio kitu. Nishawatumia mpunga kiasi fulani na salio ni ndogo…” Alisema Konde Boy

Ila je? Kuna uwezekano wowote lebo hii ikawa inamnyanyasa Konde Boy.

Msanii Rich Mavoko alipitia njia sawa na Harmonize.

Je, hela wanayodai wasanii hawa inaweza ikaathiri muziki wao wa njia moja ama nyingine?

Ujumbe wa Tanasha kwa mtoto wake, aeleza anavyojihisi

Mpenzi wa nyota wa muziki Tanzania Diamond Platnumz ana furaha riboribo baada ya kupata mtoto wa kiume.

Huyu ni mtoto wa kwanza wa mtangazaji huyu wa redio.

Mama huyu amechapisha katika mtandao wa kijamii furaha aliyo nayo.

Aidha, amesimulia anavyojihisi kuwa mama.

Soma hadithi nyingine:

(+ Video) Makovu ya kupoteza kazi Sportpesa, mama aangua kilio Twitter

 Tukio la Tanasha kuzaa linatokea kama sadfa huku likitokea siku sawa na siku ya kuzaliwa ya Diamond.

Mastaa wakubwa Tanzania wakiwemo Rayvanny, Mbosso na Lavalava miongoni mwa wengine walitoa maneno yao ya moyoni na kumpongeza Chibu Dangote.

Mtoto huyu ambaye ni wa 4 wa Naseeb bado hajapewa jina.

Ikumbukwe kuwa Mondi ana watoto nje ya uhusiano na Tanasha.

“Masaa kumi na saba baada ya wiki 42, kujifungua kwa kawaida…ina msaada kwangu sana. Mimi sasa na mpenzi wangu ni mama wa kijana mtanashati mwenye afya. Asante Mungu 🙏🏽…”

Soma hadithi nyingine:

Machachari sio kipindi tena, Inspekta Mwala na Papa Shirandula kufanyiwa mageuzi

Aidha, Tanasha alimwandia ujumbe mzito mwanawe,

“Happy birthday to my son. God is good. ❤️🙏🏽”

Gusa usome hadithi za Abraham kivuva

Chibu Dangote apiga 30, ampa Tanasha zawadi ya mtoto

Nyota wa Tanzania Diamond Platnumz hapa jana amepata baraka tele baada mpenzi wake Tanasha Donna kujifungua mtoto wa kiume.

Tukio la Tanasha kuzaa linashahibiana na siku ya kuzaliwa ya staa huyu.

Soma hadithi nyingine;

Jacque Maribe alamba dili nono baada ya kuitema runinga ya Citizen

Diamond Platnumz alikuwa wa kwanza kuvuja taarifa hizi katika mitandao ya kijamii.

Mastaa wakubwa Tanzania wakiwemo Rayvanny, Mbosso na Lavalava miongoni mwa wengine walitoa maneno yao ya moyoni na kumpongeza Chibu Dangote.

Mtoto huyu ambaye ni wa 4 wa Naseeb bado hajapewa jina.

Ikumbukwe kuwa Mondi ana watoto nje ya uhusiano na Tanasha.

Soma hadithi nyingine;

Mhubiri msagaji aeleza A-Z sampuli ya wanawake anaowazimikia

Mwanzo alipata watoto wawili na Zari The BossLady mwanamitindo kutoka nchi ya Uganda.

Baadaye akapata mtoto na Hamisa Mobetto.

Diamond alichapisha ujumbe wa furaha katika mtandao wa Insta.

View this post on Instagram

Happy Birthday to us ❤🌹❤

A post shared by Chibu Dangote..! (@diamondplatnumz) on

Jinsi Mbosso, Rayvanny na mastaa bongo walishobokea Mondi kwenye Birthday

Staa na nyota wa nyimbo ya Pepeta Rayvanny amechora ujumbe mzito kwa bosi wake Diamond Platnumz.

Nyota huyu yupo chini ya usimamizi wa lebo kubwa Afrika mashariki ya WCB ambayo inasimamiwa na Mondi.

Haya yamejiri baada ya Diamond Platnumz kutangaza siku yake ya kuzaliwa jana.

Mastaa wengi nchini humo walionyesha tabasamu na kumtakia heri njema Mondi.

Aidha, Harmonize hakuweza kumtakia heri njema aliyekuwa bosi wake.

“Mungu alichagua ukawe kiongozi, kiongozi hana tofauti na dereva wa gari…’_

“Yaani abiria mnaweza kulala usiku kucha, yeye halali kuhakikisha mnafika salama mnapoenda…”

View this post on Instagram

MUNGU ALIKUCHAGUA UKAWE KIONGOZI , KIONGOZI HANA TOFAUTI NA DEREVA WA GARI . YANI ABIRIA MNAWEZA KULALA USIKU KUCHA, YEYE HALALI KUHAKIKISHA MNAFIKA SALAMA MNAPOENDA. UMEASAIDIA WENGI SAAAANA NA BADO UNAWASAIDIA WENGI SANA LAKINI PIA WAPO WANAOTAMANI MSAADA WAKO PIA. WEWE NI KIONGOZI , KUTUKANWA, KIDHALILISHWA, KUSIMANGWA , KUONEKANA UNA MATATIZO NISEHEMU YAKO YA KAZI MAANA LAWAMA SIKUZOTE NI ZA KIONGOZI ,YANI YULE ANAE KAA MBELE SIKU ZOTE NI WAKULAUMIWA TU. NAOMBA MTANGULIZE MUNGU KATIKA MAWAZO NA KILA ULIFANYALO MAANA BINADAMU SIO WOTE WANAOPENDA MAFANIKIO YAKO……… NAAMINI WENGI WANAKUPENDA HATA WANAOKUTUKANA WANAKUPENDA , HATA AMBAO WATU WANAHISI NI MAADUI ZAKO BADO WANAKUPENDA SANA . MATATIZO UNAYOKUTANA NAYO NAOMBA YASI KUKATISHE TAMAA NA KUKUVUNJA MOYO WA KUSAIDIA WENGINE…….. HAPPY BIRTHDAY BIG @Diamondplatnumz

A post shared by VANNYBOY (@rayvanny) on

“Umesaidia wengi sana na bado unawasaudia wengi sana…”

“Nakunywa Pombe nadondoka, Kwa ajili Yako we tazama mpaka Watoto wananicheka, Sababu Yako Wee..” Wengi wao watakuwa wanajiuliza nimeandika kitu gani hapo Juu, ila naimani popote ulipo muda huu Ukisoma hiyo Mistari utakuwa unakumbuka huu wimbo.., Ulitokea kunipenda na kunitabilia mengi tangu siku ya kwanza unaniona narecord huu wimbo .. ‘Nanukuu’..” Boss , Dogo Hapa Kaimba Kama Mimi..” Majibu yalitoka kwa @mkubwafellatmk na Boss Tale@babutale ” Anakupenda Sana na tushamsema sana abadirike na aache Kukuiga atashindwa kutengeneza …” Mbosso.

View this post on Instagram

"..Nakunywa Pombe nadondoka, Kwa ajili Yako we .., Tazama mpaka Watoto wananicheka, Sababu Yako Wee.." Wengi wao watakuwa wanajiuliza nimeandika kitu gani hapo Juu, ila naimani popote ulipo muda huu Ukisoma hiyo Mistari utakuwa unakumbuka huu wimbo.., Ulitokea kunipenda na kunitabilia mengi tangu siku ya kwanza unaniona narecord huu wimbo .. 'Nanukuu'.." Boss , Dogo Hapa Kaimba Kama Mimi.." Majibu yalitoka kwa @mkubwafellatmk na Boss Tale @babutale '' Anakupenda Sana na tushamsema sana abadirike na aache Kukuiga atashindwa kutengeneza Fanbase Yake .. ", na Maongezo hayo yote yanaendelea Mimi nilikuwa bado siamini Kama kweli leo nimemuona @diamondplatnumz Live Bila Ya Chenga Daah !!!.., nafsi yako haikusita ukaingiza Vers moja kali kunibariki mdogo wako japo nilikuwa sijulikani na sijatoa wimbo hata Mmoja kwa lugha rahisi ni UNDERGROUND.. ,ila kutokana na Ubize wa Kazi zako basi ukawatu unanambia Mdogo wangu Wimbo wetu anaupenda sana Mama @mama_dangote na Mtoto Dada Esma @_esmaplatnumz anaitwa @Tahiyaplatnumz na nikitoka kushoot Video ya #Kesho nitakushtua tumalizie Mdogo wangu ..Ukaishia hapo.., kutoka na Speed ya kazi zako tukakosa time ya kumalizia .. ila kitendo cha Kuwa na namba yako tu ya Simu na ile Sauti yako nusu Kwenye CD ya wimbo wangu basi Amshaamsha zangu Temeke kila mtu alijua Mbosso ananamba za Diamond na Washafanya Collabo .." basi kitu kidogo tu Bro DIAMOND KASEMA NISIMPE MTU NAMBA … BRO DIAMOND KASEMA NISIVAE MAKACHA .. BRO DIAMOND KASEMA NISIWE NATEMBEA SANA NA GITAA MGONGONI NITAKUWA SIO MNYAMWEZI 😂 "Asante Sana Bro leo Umewaaminisha wenye macho na Masikio kuwa Mbosso anakipaji na anaweza kufanya Mengi Mazuri .. Nakupenda Sana Bro na bado nakuhitaji sana Kwenye Safari yangu ya mziki.., Mungu akupe Umri Mrefu Wenye neema nyingi Bro inshaallah 🙏 @diamondplatnumz

A post shared by Mbosso (@mbosso_) on

 

 

 

 

Katoto hodari! Tazama picha za mama ya mtoto wake Mbosso

Mwanamziki wa WCB Mbosso Khan ana binti mwingine ambaye ni mama ya mtoto wake wa kiume aliyezaliwa miezi miwili iliyopita.

Mwanamziki huyu alifanya karamu ya kukata na shoka kusherehekea siku ya 40 ya kuzaliwa kwa mtoto wake.

Sherehe hii iitwayo ‘Aqiqah’ hufanywa na waislamu baada ya mtoto kuzaliwa  na kupelekwa kwenye nyumba ya wazazi wake.

‘Pesa chafu’ katika ununuzi wa ngano Narok, CBK yatilia shaka

Karamu  hii ilihudhuriwa na watu waliojulikana sana Tanzania kama Hamisa Mobetto, Esma Khan (dadake Diamond),Fahima (mama ya mtoto wake Rayvanny) na wengi zaidi.

Sherehe hii ilikuwa siku chache baada ya Mbosso kuomboleza kifo cha mama ya mtoto wake mwengine ambaye alikuwa mcheshi.

”Nimerogwa!” Akiri mwizi baada ya kuiba mafuta ya kujipaka

 Tazama picha za kidosho Rukia, mpenzi wake Mbosso

mbosoo 6mboso 2mboso 3mbosso 5 mbosso 7 mbosso 8 mbosso 9 mbosso 10