Abby mwanawe naibu wa Rais William Ruto, afanya vyema KCPE 2019

Mwanawe Naibu wa Rais William Ruto amepata alama 406 katika matokeo ya mtihani wa KCPE.

Abby Cherop Ruto alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliotia fora sana katika shule ya msingi ya Greenvale iliyoko kaunti ya Uasin Gishu.

Mamake, Prisca Chemutai Bett, alisema kwamba bintiye amekuwa mwenye bidii sana katika masomo yake.

Jamaa Atishia Kukata Simu Patanisho Ikiendelea, Asema Hasaidiki

Aidha alisema kwamba shukran za mafanikio yake yanamwendea naibu wa Rais William Ruto ambaye amekuwa msaidizi.

“Ninajua amepokea taarifa hizo. Lakini bado hajatuma ujumbe wa kumpongeza na ninaamini atatuma atakapopata muda. Amekuwa akitusaidia na ninapongeza juhudi zake,”  Chemutai alisema.

Chemutai alisema ingawa yu ngali anachambua matokeo, lakini anaamini kwamba Abby Ruto ni miongoni mwa wanafunzi tano bora.

Jumla ya wanafunzi 1,083,465 walifanya mtihani wa KCPE 2019. Kati ya hiyo, 543,582 ni wanaume huku 539,874 wakiwa wasichana.

Mnamo 2017, Chemutai alitaka korti imwamuru Naibu wa rais Ruto kumpa malezi bora.

Harambee Stars Na Togo Watoka Sare Ugani Kasarani

Alimshtumu kwa kumtekeleza yeye pamoja na mwanawe huku wakilalamikia kuishi katika ufukura baada ya kudai kuwa Ruto alikuwa ameacha majukumu yake.

Chemutai alidai kuwa Ruto alikuwa mpenziwe wa kitambo.

“Mwanangu wa umri wa miaka 11, Abby anapata malezi bora kutoka kwangu ikiwemo masomo katika shule ya msingi ya kibinafsi,” Ruto alisema kupitia Twitter.

Aidha alisema kuwa suala hilo lilikuwa limechochewa kisiasa.

 

‘Je wakumbuka tulichokubaliana?’ Ruto amuuliza Uhuru leo ikiwa birthday yake!

Hii leo ikiwa maadhimisho ya miaka 58 tangia rais wa nne wa jamhuri ya Kenya, mheshimiwa Uhuru Kenyatta azaliwe, wakenya wengi wamechukua fursa hiyo kumtakia heri njema akiwemo naibu wake, William Ruto.

Gunia la mabao: Southampton wakalifishwa 0-9 na Leicester

Ruto kupitia mtandao wa Twitter, alimtumia bosi wake ujumbe mfupi akimtakia baraka tele.

Hata hivyo, katika ujumbe wake, alimsifu Uhuru kwa kuwa mtu aliyempa yeye na mamilioni ya wakenya msukumo mkuu kwa kuwa rais mchanga zaidi nchini.

Ujumbe huo haukuishia hapo kwani alimalizia kwa kumkumbusha mkuu wake kuwa anangoja siku watakapostaafu ili wawili hao wafanye walichokubaliana.

‘Nilinyang’anywa mtoto akapelekwa kwa mpango wa kando,’ – Rozie

Ruto aliandika,

Happy birthday to my friend & Boss H.E. Uhuru Kenyatta. You are a great inspiration to me, Jubilee leadership and millions of Kenyans as the youngest President we’ve ever had. As we age, I look forward to what we agreed on to do when we retire. Remember? Ubarikiwe mpaka Ushangae!

 

Tazama jinsi urembo wa mwanao Diana na Bahati unazidi kukolea

Ujumbe huo ulizua maswali mengi miongoni mwa Wakenya huku wengi wakijiuliza iwapo Ruto anapanga kustaafu pindi tu hatamu ya rais Kenyatta itakapoisha, mwaka wa 2022.

Soma baadhi ya ujumbe.

Donald: You are retiring with the boss? I thought you are in the ballot for 2022?

Migwi: Tuambie kenye Mliagree

Prince Kelvin: Unaretire?

Ronoh: Your promises all seems null and void,where are the jobs for the youths? Where are the mighty Stadiums

William Ruto amjibu Waiguru. Tamko la Waiguru halikumpendeza

Siasa za ni nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta zinashadidi na kurindima kama moto jangwani licha ya Kenyatta kuwaonya wanaofanya siasa wakome.

Hali hii imekigawanya chama tawala katika tanzu la Kieleweke na tanzu lingine la TangaTanga.

Kieleweke linaaminika kuwa tawi linalounga mkataba wa Handshake kati ya Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Amollo Odinga.

Soma hadithi nyingine:

Inakuaje mkewe Ken Okoth ni mfuasi sugu wa MacDonald Mariga?

TangaTanga nalo ni tawi la chama tawala linalofanya kila juhudi kuona kwamba Ruto ameuchukua usukani wa urais.

Siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa wanajua kuucheza.

Nikueleze kwamba matakwa ya wanasiasa huwavuta pamoja. Usishangae kuona wanasiasa katika urafiki wa kisiasa wakitengana na kila mmoja kuchukua njia tofauti.

Wakati kambi hizi mbili zinavutana, nguzo kuu na ambalo litatikisa wingu la maamuzi ni jinsi wapiga kura wa mlima Kenya wataamua.

Ikumbukwe kwamba jamii ya Kikuyu ina idadi kubwa ya wapiga kura nchini.

Tunasubiri kuona iwapo jamii ya kikuyu itateuwa mgombeaji wa urais atayempa tumbojoto na wasiwasi William Samoei Ruto.

Soma hadithi nyingine:

Nia ya kuzima ndoto ya Ruto. TangaTanga waelezea hofu yao kuhusu ukimya wa Uhuru Kenyatta

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru mapema wiki hii amenukuliwa katika vyombo vya habari akisisitiza kwamba jamii ya Kikuyu haiko tayari kumchagua tena rais mkikuyu.

Kauli hii ya Waiguru haikumfurahisha Ruto na akaamua kumjibu kupitia mtandao wa Twitter.

“Tulimuunga mkono na kumpigia kura Uhuru akamrithi Kibaki kwa ni misingi ya uchapakazi wala sio ukabila. Yeye sio kiongozi wa jamii yoyote ila ni kiongozi wa Jubilee…”

Urafiki wa kisiasa kati ya Waiguru na Ruto unaonekana kuota mbawa. Sio kama zamani.

 

Nangoja makamu wa Rais William Ruto anipe pesa nifanye harusi

Mcheshi Fred Omondi alifunguka na kusema kuwa anangoja makamu wa Rais William Ruto agharamie harusi yake.

fred omondi

Fred ambaye kwa sasa hana mpenzi alisema kuwa, makamu wa Rais humpa moyo wa kufunga harusi na kumwomba mheshimiwa ampe pesa kiasi ya kugharamia harusi yake.

Zaidi ya hayo, alisema kuwa yeye hufurahishwa sana na vile ambavyo Makamu wa Rais hutoa mchango kwa ukarimu sana kila wakati, makanisani.

“I am trying to wait for the money Deputy President William Ruto contributes during church harambees to get to me,” alisema.

Inakuaje Mkewe Ken Okoth Ni Mfuasi Sugu Wa MacDonald Mariga?

Zaidi ya hayo, Fred alisema kuwa akipewa shilingi elfu mia mbili, (200 000) atafunga ndoa.

“If he gave me just Sh200K, I would do a wedding.”

 Vilevile alisisitiza na kusema kuwa, makamu wa Rais ndiye anayemzuia na kumwambia mheshimiwa akohoe tu, kisha afanye harusi.
”DP, you are the one holding me back, just cough so that I can wed,” alisema.
Alipoulizwa kama amewahi achwa na mpenzi wowote, alisema kuwa, kuna wakati ambao mpenzi wake alimwacha kwa sababu alikuwa na tabia ya kuongea na wasichana wengi sana wakati wa matukio zake za burudani.

“I was once dumped by a woman because I was too social with ladies during my events.”

Hata hivyo, Fred alisema kuwa utenganisho wake na wapenzi wake huwa kwa njia ya utulivu sana na mara kwa mara wanapokata ushirikiano wao wa kimapenzi, wao huenda kuwa marafiki wa dhati.

Kwa sasa, Fred anazingatia Comedy show itakayokuwa kwenye televisheni.

 

Ruto ajitetea kuhusu kauli ya “Kutangatanga”. Asema yupo kufanya maendeleo

Naibu wa rais William Ruto sasa anahoji kwamba juhudi zinazowekwa kuibadilisha katiba hazipaswi kamwe kuwa kisiki kamwe katika mipango ya maendeleo ya serikali .

Ruto amesema kwamba nchi hii haiwezi kubadilishwa kupitia mageuzi ya katiba ila ni kuidhinisha mipango ya maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi kaunti ya Vihiga hapo jumamosi, Naibu wa Rais alisema miito ya mara kwa mara kuifanyia marekebisho katiba haiwezi kuingilia utendakazi na ajenda ya Jubilee.

Soma hadithi hii hapa;

Tupo tayari sasa. Farasi wa ODM atangazwa kusubiria mtifuano Kibra.

“Maendeleo hayatasitishwa na siasa zinazofanyika za kubadilisha katiba. Wakenya wanataka miundomisingi kama barabra,hospitali,shule, bima za afya za hpospitali na nyinginezo ili waboreshe maisha yao na wala sio siasa.” Ruto

Waliokuwepo katika ziara hiyo ya naibu wa rais ni Charles Gimose (Hamisi), Benjamin Washiali (Mumias mashariki), John Waluke (Sirisia), na aliyekuwa gavana wa Vihiga Moses Akaranga na Boni Khalwale.

Ruto alisema kuwa Jubilee ipo tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote bila kujali mrengo anaoegemea wa kisiasa akihoji kuwa huu sio wakati wa siasa.

 

Soma hadithi hii hapa;

William Samoei Ruto atarajiwa kuzuru ngome ya kinara wa ANC Musalia Mudavadi

 

Ruto alisema kuwa viongozi wasishangae kuona akitanga sana nchini.

“Haijalishi ni nani ananialika katika mikutano ya maendeleo kwa sababu ajenda yetu ni kuhudumia wakenya. Ziara zangu nchini sio za kufanya siasa. Kuna wakati wa kila jambo.” William Ruto.

Picha ya siku: Je hii ndio jinsi mpya ya kumsalimu mumeo?

Picha ya bi Rachel Ruto, akimsalimu mumewe naibu wa rais, mheshimiwa William Ruto, imekuwa chanzo cha mazungumzo mengi katika mitandao ya kijamii.

PATANISHO: Tayari nishapata mume mwingine kwa hivyo ajisort

Katika picha ile, bi Rachel anaonekana akiwa mnyenyekevu mno kwani anamsalimu mumewe huku akiwa ameinamisha kichwa chake na mkono wake wa kushoto ukiwa umeshikilia wa kulia. Hii yote ni kuashiria heshima kuu sio tu kwa mumewe bali pia kwa kiongozi.

Je wadhani hii ndio jinsi wake wanapaswa kuwasalimu waume zao?

The new Wolves? Wazito FC wapo tayari kutetemesha msimu mpya wa KPL

picha

” Nitahakikisha hauna nafasi yoyote Kenya,” Ruto amfokea Raila

Naibu wa Rais William Samoei Ruto ammepiga kijembe kiongozi wa upinzani Raila Amollo Odinga leo kwa kumwambia kuwa lengo lake ni kuwafanya wakenya wawe maskini ili wamtegemee.

unnamed__1561985990_75568

Soma hapa:

Tanzia! Tazama jinsi Akothee, King Kaka walivyomuomboleza Bob Collymore

Ruto alionekana kumjibu Raila baada Odinga kusema jumamosi kuwa viongozi wanaotoa kitita kikubwa cha pesa katika harambee za kanisa nchini wanapaswa watangaze asili ya utajiri wao. Ruto alisema haya akiwa katika hafla ya kukuza pato la kina mama Mugirango kaskazini, kaunti ya Nyamira.

“Ulikuwa unapinga Eurobond ukisingizia ufisadi; ukapinga pia Northern Collector Tunnel bado ukisema kuna ufisadi; Ulikuwa unapinga reli ukisingizia ufisadi; bado ulikuwa unapinga kutoa pesa kanisani ukisema ni ufisadi.” alifoka Ruto.

Soma hapa:

Soma ujumbe wa mwisho wa Bob Collymore. Risala za viongozi na mastaa

“Ni kwa sababu wewe ni “mungu wa umaskini” na unataka ukata katika nchi hii. Unapinga kila mradi wa maendeleo nchi hii ili watu wawe maskini ili wazidi kukufuata na mimi nakwambia tutafanya kazi usiku na mchana tuuondoe umaskini. Hautakuwa na nafasi yoyote nchi hii.” Ruto alimwambia Raila.

Ruto mara kwa mara ametetea kitendo chake cha kutoa hela kusaidia miradi kanisani na kusema hawezi goma kufanya hivyo.

Baada ya madai ya mauaji, Ruto atuma ujumbe kwa wabunge wa Jubilee

Naibu wa Rais William Samoei Ruto sasa anawataka wajumbe wa chama tawala cha Jubilee kujiepusha na siasa za mwaka wa 2022. Akizungumza katika maeneo ya mkoa wa Mumias magharibi, kaunti ya Kakamega, Ruto amewasihi wabunge hawa ambao wanaonekana kugawanyika katika mirengo ya TangaTanga na Kieleweke wakome siasa za ukabila na mgawanyiko.

Soma hapa hadithi :

Audio yavuja ! Inasimulia A-Z jinsi mauaji ya William Ruto yatakavyotekelezwa

Soma hapa:

‘Enda ukapikiwe na huyo dem wako!’ Diana amfokea Bahati

Ruto alisisitiza kuwa msingi wa chama cha Jubilee umoja na maendeleo ya taifa.

” Siasa zetu zinatakiwa ziwe za kuyabadilisha maisha ya wakenya. Hilo ndilo jukumu letu.” alisema William Ruto.

Ruto alisema kuwa maendeleo ya taifa hili yanategemea sana siasa zinazoendeshwa na wanasiasa na viongozi serikalini na katika upinzani. Ruto alionekana kukasirishwa na baadhi ya wanasiasa wanaotenga wakati mwingi kwa siasa za chuki badala ya kuchapa kazi.

Soma hapa:

Akothee sasa awaomba wachezaji Taifa Stars wampe mimba

Ruto aliwahimiza wanasiasa wa Jubilee kuongozwa na manifesto ya chama ili pamoja waweze kuupiga vita ukabila nchini.

Audio yavuja ! Inasimulia A-Z jinsi mauaji ya William Ruto yatakavyotekelezwa

Naibu wa rais Dkt. William Samoei Ruto mapema wiki aliibua kisa na ambapo baadhi ya viongozi serikalini walikuwa wanapanga njama ya kumuua. Baada ya madai hayo barua ilizagaa katika mitandao ya kijamii ikiwa na lalama kuwa mawaziri Peter Munya, Cecily kariuki na Joe Mucheru waliwahi kukutana katika hoteli moja jijini ya La Mada na kuhusika katika njama hiyo.

Soma hapa:

Tazama jinsi mastaa na viongozi walivyowapa kongole Harambee Stars

 Naibu wa Rais amehepa kuzungumza kuhusu swala hili katika vyombo vya habari. Siku chache baada ya lalama hizo, kipande cha sauti kimevuja kikieleza mwanzo mwisho jinsi njama hiyo ingefanyika. Sauti katika kipande hicho cha audio inakisiwa kuwa ni ya katibu mmoja wa kudumu akieleza kilichofanyika tarehe 14 mwezi Mei. Audio hiyo inasimulia wakati mawaziri hao walikutana.

Moses Kuria ametokea waziwazi na kusema yeye ndiye aliidhinisha kuwa wakutane katika Hoteli ya La Mada. Aidha, amekana habari zinazohusu njama ya kumuua William Ruto. Makachero sasa wanachunguza madai hayo ya mauaji ya naibu wa rais.

Soma hadithi nyingine:

Orodha: Tazama mastaa wanaoishi chumba kimoja bila kuoana

Waziri Munya ametokea kupiga sauti hiyo.

“Watu waliohusika katika uandishi wa barua ghushi ndio wamerekodi na kuchapisha sauti bandia.” Amesema Munya

“Tulipokuwa tunaingia katika ndani ya La Mada, tuliagizwa tusiingie na simu zetu. Alichukua simu zetu na nakumbuka tuliingia na rafiki yangu na katibu wa kudumu ambaye alikuwa na tarakilishi ikachukuliwa” Sauti ya mwanamme inasimulia katika audio hiyo.

Kuvuja kwa audio hii kunawapa kizungumkuti jopo la makachero linalochunguza madai haya kubaini kuwa ni ya kweli ama ni bandia.

Tangatanga wamjibu Rais Kenyatta

Baada ya Rais Kenyatta kuwanyamazisha kundi la wabunge katika kongamano la waumini wa Akorino Kasarani wikendi iliyopita, baadhi ya waliolengwa na matamshi ya rais wameamua kumjibu.

rais-kenyatta (1)

Soma hapa:

Bajeti iliyosomwa inamtoza mwananchi uchumi wa juu – Gavana Mutua

Katika mahojiano na gazeti maarufu nchini The Star, wabunge hawa wameonyesha jaribio la kuasi na kutofautiana na matamshi kuwa rais aliwatafutia kura.

Kukaidi kwa wabunge hawa wa jimbo la mlima Kenya kunaonyesha ushawishwi alionao naibu wa rais William Ruto katika ngome hiyo .

Kundi hili la Tangatanga linasheheni wabunge kutoka mkoa wa kati. Mbunge wa Kandara, Alice Wahome alionekana kukerwa na matamshi ya rais.

“Ni jambo la kusikitisha kuona rais akitoa matamshi aliyoyatoa katika madhabahu. Sidhani kuwa amenisaidia kuingia katika bunge.” alisema Wahome.

Pata uhondo:

HAPANA! Wenye magari wapinga NTSA kuhusu ukaguzi wa magari ya kibinafsi

Rais aliwaonya wabunge hao wa maeneo ya mlima Kenya jumapili kuwa yeye ndiye kiongozi wa jamii ya wakikuyu na wasichukulie kimya chake kama woga.

Rais Kenyatta aliwaita “wakora” na kusema kuwa wamekosa kumuunga mkono katika mchakato wa kuleta amani hapa nchini (BBI) na kuahidi kufanya mizunguko wanakojificha na kupambana na wao.