Tahadhari! Dereva wa Uber ashtakiwa kwa kumbaka abiria

uber
uber
Dereva mmoja wa Uber ameshtakiwa  kwa kumdhulumu kimapenzi mteja wake wa kike alipokuwa akimpeleka kwa mpenzi wake.

Antony Macharia  alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu Charles Mwaniki. Macharia anashtumiwa kwa kutekeleza  kosa hilo  Juni tarehe 9 mwendo wa saa nne usiku mtaani Lang’ata, Nairobi.  Abiria huyo aliyedhulumiwa na Macharia ni  mwanamke mwenye umri wa miaka 24 aliyetambulia na stakabadhi za mahakama kama MA.

Kulingana na ripoti ya polisi  mteja huyo aliitisha huduma za teksi ya Uber akiwa katika barabara ya  Crescent Road na ilipowasili aliketi katika kiti cha nyuma.  Mwathiriwa alikuwa akiburudika  na wenzake kabla ya kuitisha teksi hiyo na alipokuwa  safarini kuelekea kwa mpenzi wake alihisi ni kana kwamba mtu alikuwa akimgusa. Muda mfupi baadaye alijihisi kuwa mnyonge. Alishangaa kujipata  akiwa  katika kiti kilicho kando ya dereva ambaye mikono yake ilikuwa ikimshika sehemu zake za siri.

Alishawishi dereva huyo kumpeleka katika nyumba ya mpenzi wake  na walipofika alishuka na kupiga ukemi ili kupewa usaidizi. Mpenzi wake alitoka  nje kutoka nyumba yake kwani tayari alikuwa amearifiwa na mwanamke huyo kupitia ujumbe wa sms.

Alipomueleza mpenzi wake kilichofanyika, alijaribu kutafuta maelezo kutoka kwa dereva huyo wa Uber aliyekana madai hayo na kupelekea ripoti kufikishwa kwa polisi. Mshukiwa aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu au  bondi ya shilingi elfu 50 pesa taslimu. Kesi hiyo itaendelea Julai tarehe  moja.