Taharuki kuhusu ongezeko la visa vya mimba za wasichana wadogo Murang'a

Angalau visa viwili vya mimba za wasichana wadogo huripotiwa katika kaunti ya Murang’a kila siku.

Katibu wa afya Joseph Mbai anasema walirekodi zaidi ya visa elfu 6,500 mwaka uliopita. 170 kati ya visa hivyo vilihusisha wasichana wa umri wa kati ya miaka 10 na 14 huku waliosalia walikua na umri wa kati ya miaka 15 na 18.

Mbai anasema hii ni licha ya juhudi za serikali ya kaunti kujaribu kukomesha visa hivyo na ili kuokoa wasichana wadogo.

Mbai said he noticed that teenage pregnancies was a serious problem in the county last year after local health facilities recorded 6,579 cases.

Mapema mwaka huu, Mbai alituma barua kwa makanisa yote akiwaelezea kuhusu visa hivyo vya kutisha huku akiwaomba wawashauri vijana.

Mbai anasema kufikia sasa, wanaume wanne tayari wamepokea vifungo vya maisha baada ya kushtakiwa kwa kuwanajisi wasichana wenye chini ya miaka 12.

Katika kijiji cha Mugeka village, mwanaume mmoja anatafutwa baada ya kumpachika mimba msichana wa miaka 16 ambaye ni wa kidato cha pili.

Inasemekana kuwa mwanaume huyo wa miaka 25 alimdanganya na kumpeleka nyumbani kwake kabla ya kushiriki mapenzi naye.

Baada ya kufunguka kuhusu tukio hilo, msichana huyo alipelekwa katika shule ya Murang'a ambapo alipatikana kuwa mja mzito.

“Wasichana wanapaswa kufunzwa kukataa mambo ya kushiriki mapenzi. Wanaume lazima nao wajue kuwa ni makosa kushiriki mapenzi na wasichana wadogo na isitoshe visa vyote vyapaswa kuripotiwa." Mbai alisema akidai kuwa hiyo tu ndio njia ya kumaliza mambo ya mimba za mapema.

Shule zapaswa kuanzisha masomo ya ngono kwani watoto wamekuwa wakijifunza hayo kupitia mitandao ya kijamii. Alilaumu visa hivyo kwa utumizi wa mihadarati na ukosefu wa maadili mema.