Ufichuzi huo kuhusu ukosefu wa usawa katika ugavi wa utajiri umo katika ripoti ya kurasa 64 ya Oxfam iliyotolewa siku ya jumatatu wakati wa kongamano la uchumi wa dunia WEF huko Davos, Switzerland. Oxfam ,yenye makao yake jijini Nairobi imesema ukosefu huu wa usawa umesababishwa na ugavi wa kibaguzi wa utajiri unaoegemea jinsia moja na unaowapa kipau mbele wachache walio navyo. Shirika hilo limesema serikali nyingi ulimwenguni hazijachukua hatua za kurekebisha tatizo hilo
“ wanawake na wasichana ni miongoni mwa wanaokosa kunufaika ipasavyo na mfumo wa sasa wa uchumi wa ulimwengu . wanatumia mabilioni ya saa kupika ,kusafisha na kuwatunza watoto na wazee’ amesema afisa mkuu mtendaji wa OXFAM India Amitabh Behar. Ripoti hiyo imesema wanawake na wasichana walitumia saa bilioni 12.5 kufanya kazi wasizolipwa kila siku ambazo zilichangia ($10.8 trillion) kila mwaka katika uchumi wa dunia.
“ Wanawake wanafanya zaidi ya thuluthi nne ya kazi yote ya utunzi isio na malipo .Wao hulazimika kupunguza saa zao za kufanya kazi au kuacha kazi kabisa ili kushughulikia kazi za utunzi’.
“ Kazi kama vile za walimu wa shule za chekechea ,wafanyikazi wa nyumbani na wasaidizi huwa na mlipo ya chini sana na manufaa adimu kando na kwamba zinahitaji muda mwingi wa kuzitekeleza na zinasababisha uchovu wa kimwili’ Ripoti hiyo imeongeza .