Talanta si ndumba! Msanii chipukizi anayewapa wasanii ushindani mgumu amepanga kufanya haya

dantez-1-696x696
dantez-1-696x696
Msanii chipukizi Daniel Simiyu almaarufu Dantenz 254, anawapa wasanii wa Kenya ushindani mgumu. Kijana huyo ambaye yuko katika kidato cha tatu amerekodi nyimbo zake nne na kupanga kufanya collabo na wasanii wanane wa nchi tofauti.

Kenya, Nigeria, Cameroon, Afrika Kusini, Jamaica, Rwanda na Ivory Coast.

Dantez ambaye amesajiliwa katika lebo ya Maliza Umaskini atatoa albamu yake ya kwanza Desemba mwaka huu, Usimamizi wa msanii huyo ukiwa katika mahojiano ulisema kuwa Dantez anafuata kalenda ya shule na huwa anasafiri kwenda Afrika kusini kurekodi nyimbo zake.

Waliongeza na kusema kuwa huwa anarekodi nyimbo zake wakati wa likizo. Wakizungumzia uwekezaji wake wa baadaye, usimamizi ulikuwa na haya ya kusema.

“FOR NOW WE ARE INVESTING IN HIS EDUCATION. MALIZA UMASKINI HAS GIVEN HIM A SCHOLARSHIP UP TO UNIVERSITY. WHEN HE STARTS EARNING FROM HIS MUSIC WE WILL COME UP WITH AN INVESTMENT PLAN FOR HIM IN CONJUNCTION WITH HIS MOTHER.”

Kijana huyo alianza kujulikana mnamo mwaka wa 2018, wakati maliza Umsakini ilimuokoa kutoka kwa umaskini. Alikuwa anaishi na ndugu zake na mama yake ambaye alikuwa anawatafutia chakula cha kila siku baada ya baba yao kuaga dunia.

Wasanii wenye umri mdogo ambao huwa wanasafiri ng'ambo kwa ajli ya usanii wao licha ya masomo yao ni Amani G, Wendy Waeni, Nikita Kering na wengine.