tanasha

Tanasha Donna apata kazi mpya miezi michache baada ya kujifungua

Kama jinsi wasanii Sauti Sol walivyoimba, ‘Mungu akileta mtoto analeta pia na sahani yake’ basi kama kuna mzazi anaweza toa ushuhuda huo ni bi Tanasha Donna, mpenziwe msanii Diamond Platnumz.

Bonge la parte! Diamond na Tanasha wampa mwanao sherehe ya kufana (PICHA)

Wiki chache tu baada ya kujifungua mwana wao kwa jina, Naseeb junior, Tanasha ambaye pia ni msanii, amepata kazi mpya!

Tanasha ametuliwa balozi wa kampuni ya kitalii ya ‘Spot on vacations’.

Baada ya kutia mkataba huo, Tanasha alijitosa katika Instagram kutangaza habari hizo njema akidai kuwa “hii leo nitakuwa na habari spesheli”.

Mwanawe wa Diamond na Tanasha ashereheka siku 40 za kuzaliwa

Aliandika;

‘SUPER EXCITED TO ANNOUNCE MY PARTNERSHIP AS BRAND AMBASSADOR OF @SPOTONVACATIONS & TOMORROW WE HAVE A VERY SPECIAL ANNOUNCEMENT FOR YOU!’

tanasha

Spot on Vacations ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza katika sekta ya utalii nchini Kenya na hushughulikia maswala ya kitalii humu nchini na kimataifa kwa wale wanaotaka kujivinjari na kuzuru maeneo mbali mbali duniani.
Watu wengine mashuhuri ambao ni mabalozi wa kampuni za kitalii na safari ni Henry Desagu – Expeditions Maasai Safaris na Eric Omondi ambaye ni balozi wa Bonfire Adventures.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments