TangaTanga na Kieleweke !Fujo na zogo zashuhudiwa kanisani Murang'a

Ndindi-Nyoro-730x414
Ndindi-Nyoro-730x414
Kanisa la katoliki la Gitui kaunti ya Murang'a limegeuka uwanja wa vita na vurumai baada ya mbunge wa eneo bunge la Kiharu Ndindi Nyoro kuingia kwa nguvu na kuamua kusimamia hafla hiyo.

Sherehe hiyo ilikuwa imefika viongozi wakubwa cha chama cha Jubilee tawi maarufu linaloegemea mrengo wa Kieleweke.

Soma hadithi hii nyingine:

Kwa sasa Jubilee inakisiwa kuwa na  tanzu mbili. Moja ya Team TangaTanga inayohusishwa na naibu wa rais na tanzu ya pili Kieleweke inayokisiwa kuwa inaunga mkono ajenda za rais Uhuru Kenyatta.

Nyoro anatokea mrengo wa TangaTanga ambao unajituma sana kuona William Ruto anamrithi Uhuru Kenyatta 2022.

Mbunge huyu aliwasili muda mchache baada ya wabunge wa Kieleweke.

Mbunge mteule Maina Kamanda alitangulia kwa kuwataja wenzake.

Soma hadithi hii nyingine:

Alipochukua kipaza sauti , Nyoro alisema kuwa yeye ndiye mbunge wa mwenyeji na kwa hivyo na anapaswa kuwakaribisha wageni katika kanisa hilo la katoliki jambo na ambalo Kamanda alipinga.

Nyoro aliachanza cheche za maneno na kusisitiza kuwa hataondoka jukwaani.

"Siwezi kuwaruhusu watu kutoka Nairobi kuja hapa na kuanza kuendesha mambo katika eneo bunge langu ilhali wanajua nipo. Nimechaguliwa kama mbunge na kwa hiyo nipewe orodha ya wageni niwatambulishe." Alisisitiza mheshimiwa Nyoro.

Soma hadithi hii nyingine:

Kamanda naye hakusita kumwambia aondoke katika madhabahu na kumtuma afisa kamanda wa polisi Joseph Kinyua kumtoa Nyoro mbele ya kanisa.

Zogo zilianza pale wafuasi wa Nyoro walidhani anatiwa nguvuni na kuzua vurumai kwa muda.

Hatimaye viongozi wa kanisa hilo wametumia uwezo wao na kuleta amani katika kanisa hilo. Kamanda alitoa mchango wake wa 500,000 na mchango wa Uhuru Kenyatta wa 1000,000 na James Macharia wa 200,000. Aidha Kiongozi huyu amesisitiza kuwa watawahutubia wafuasi wao nje ya kanisa.