Tangatanga wamjibu Rais Kenyatta

rais-kenyatta (1)
rais-kenyatta (1)
Baada ya Rais Kenyatta kuwanyamazisha kundi la wabunge katika kongamano la waumini wa Akorino Kasarani wikendi iliyopita, baadhi ya waliolengwa na matamshi ya rais wameamua kumjibu.

Soma hapa:

Katika mahojiano na gazeti maarufu nchini The Star, wabunge hawa wameonyesha jaribio la kuasi na kutofautiana na matamshi kuwa rais aliwatafutia kura.

Kukaidi kwa wabunge hawa wa jimbo la mlima Kenya kunaonyesha ushawishwi alionao naibu wa rais William Ruto katika ngome hiyo .

Kundi hili la Tangatanga linasheheni wabunge kutoka mkoa wa kati. Mbunge wa Kandara, Alice Wahome alionekana kukerwa na matamshi ya rais.

"Ni jambo la kusikitisha kuona rais akitoa matamshi aliyoyatoa katika madhabahu. Sidhani kuwa amenisaidia kuingia katika bunge." alisema Wahome.

Pata uhondo:

Rais aliwaonya wabunge hao wa maeneo ya mlima Kenya jumapili kuwa yeye ndiye kiongozi wa jamii ya wakikuyu na wasichukulie kimya chake kama woga.

Rais Kenyatta aliwaita "wakora" na kusema kuwa wamekosa kumuunga mkono katika mchakato wa kuleta amani hapa nchini (BBI) na kuahidi kufanya mizunguko wanakojificha na kupambana na wao.