Kiongozi wa walio wengi katika senate Kipchumba Murkomen amewashtumu viongozi walio katika mrengo wa rais kenyatta na kiongozi wa ODM Raila odinga kwa kuwa na kamati ya siri yenye ripoti tofauti ya BBI ambayo wanalenga kuipendekeza kwa wakenya .
" Tumehofishwa na ripoti kwamba kuna kamati ya siri yenye ripoti tofauti ya BBI .Tunaitisha uwazi katika mchakato mzima wa kutekeleza mapendekezo ya ripoti ya BBI’ amesema Seneta Murkomen. Murkomen alikuwa akizungumza pamoja na wenzake Susan Kihika (Nakuru), Moses Kuria (mbunge wa Gatundu kusini ) Alice Wahome (mbunge wa Kandara) na wajumbe wengine .
" Badala ya kuzungumzia masuala husika ,mikutano ya BBI ya kisii na Kakamega ilibadilishwa na kuwa ya kumcafulia jina mtu mmoja’ aliongeza Murkomen . " Tunapinga kutumiwa kwa fedha za umma kuendesha mikutano hiyo ya hadhara endapo matumizi ya pesa hizo hayataidhinishwa na bunge au mabunge ya kaunti’
Wanasiasa wameshtumiwa kwa kuliteka nyara suala zima la utekelezaji wa BBI huku wananchi wakinyimwa fursa ya kutoa maoni yao kuihusu ripoti hiyo . wakati wa mikutano ya Kisii na Kakamega ,wengi waliopewa fursa za kuzungumza ni magavana na wabunge .
wanachama wa vuguvugu la mashirika ya kiraia wamesema wanahofishwa na jinsi mchakato mzima wa mikutao ya BBI unavyoendeshwa kwa sababu wananchi wameachwa nje .