BATTLE FRONT :Jinsi Hatma ya Waititu inavyozua vita vya ndani kati Uhuru na Ruto .

Washirika wa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto  wapo katika vita vya  chini kwa chini kuhusiana na  kura ya kumwondoa afisini gavana wa Kiambu Ferdinad Waititu  ambaye  anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi . Rais Kenyatta inaripotiwa anataka Waititu aondolewe uongozini ili kuafikiana na uamuzi wa waakilishi wa kuanti ya Kiambu na wakaazi ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu utendakazi wake na kukithiri kwa ufisadi . Naibu wa rais kwa upande wake analenga kumsaidia Waititu kuepuka kibaridi cha kusalia nje ya maamlaka hasa kwa ajili ya  umuhimu wake katika kumsaidia Ruto wakati wa kampeini za kumritihi rais Kenyatta mwaka wa 2022 .

Waituti, mkewe  Susan wangari na wengine wanane wanakabiliwa na mashtaka ya ufisadi kuhusiana na  kandarasi zenye thamani ya shilingi milioni 580  ambazozilitolewa  kwa kampuni zinazodaiwa kutoa hongo . Waakilishi wa kaunti ya kiambu walimwondoa waittu afisini  mwezi uliopita  na sasa senate inangoja kufanya kikao  siku ya jumanne ili kuamua hatma yake .

Tangu mwaka wa 2013 senate imeidhinisha tu kuondolewa maamlakani kwa gavana mmoja . Duru zaarifu kwamba maseneta wanaomwunga mkono rais Kenyatta wanashirikiana na maafisa wenye ushawishi mkubwa katika ikulu ,ili  kuhakikisha kwamba uamuzi wa walkilishi wa kaunti ya Kiambu wa kumfurusha Waititu afisini unatekelezwa . Waititu mwenyewe amepinga vikali kuondolewa kwake akidai kwamba bunge la kaunti halikuwa na idadi inayohitajika ya waakilishi wa kaunti kuufanya uamuzi huo .