UHURU MAGUFULI

Tanzania yaachwa nje huku Kenya ikianza safari za ndege za kimataifa

Tanzania imeachwa nje ya orodha ya kwanza ya nchi 11 zinazoruhusiwa ndege zake kuingia nchini Kenya.

Waziri wa Uchukuzi James Macharia siku ya Alhamisi alitoa orodha ya nchi ambazo ndege zake zinaruhusiwa nchini, zikiwemo Uchina, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe na Ethiopia.

Nchi zingine zilizoruhusiwa ni Ufaransa, Rwanda, Uganda, Namibia na Morroco.

 

Soma habari zaidi;

Conjestina ana machungu sana kuhusu kutengwa na kutopokea usaidizi wowote na serikali

 

kq-pic
Siku ya Jumanne, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilikanusha madai kwamba ujumbe wa Kenya uliokuwa umeenda kuhudhuria mazishi ya hayati rais Benjamin Mkapa ulirejeshwa nchini na mamlaka ya Tanzania kabla hata ndege yao haijatua.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba kiongozi wa wengi katika seneti Samuel Poghisio ambaye alikuwa ametumwa kama mjumbe maalum wa rais Uhuru Kenyatta. Jarida la The Citizen liliripoti kuwa ndege hiyo iliamurishwa kurejea nchini ikiwa katika anga ya eneo la Monduli nchini Tanzania. Serikali ya  Tanzania hata hivyo ilieleza kwamba ndege hiyo ililazimika kurejea Nairobi kutokana na hali mbaya ya anga.

 

Soma habari zaidi;

Wabunge wa Pwani wadai kusalitiwa na ODM

 

Usemi huu ulithibitishwa na wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Kenya.

Kulingana na duru za kuaminika, huenda Tanzania ilihamakishwa na matamshi ya rais Uhuru Kenyatta kuhusu maambukizi ya virusi vya corona aliposhauri wakenya kutojilinganisha na maeneo mengine ambayo yameficha ukweli kuhusu maambukizi ya corona.

TANZANIA (1)

“Tusijilinganishe na kusema kwamba baadhi ya maeneo hayana virusi. Mbona tuko nayo na wao hawana? Wacha niwakumbushe wakenya, tunaishi katika demokrasia, ambapo kuna uhuru wa vyombo vya habari. Kama taifa hatuna uwezo wa kuficha kitu chochote. Kinachofanyika tunawaambia,” Uhuru alisema.

Soma habari zaidi;

Tazama picha za mwanamke aliyeanguka Thompson Falls akichukua picha

 

Uhuru alikaribia kutaja Tanzania, ambayo imeshtumiwa kwa kuficha takwimu kuhusu maambukizi ya covid-19, na kuwekea vyombo vya habari masharti kutotangaza kuwepo kwa janga la corona.

Mara ya mwisho Tanzania kutangaza deta za maambukizi ya covid-19 ilikuwa Aprili 29, ambapo jumla ya watu 480 walikuwa wameambukizwa na 21 wakifariki.

 

Photo Credits: Maktaba

Read More:

Comments

comments