Tanzania yashuku vifaa ambavyo Kenya inatumia kuwapima madereva kutoka taifa hilo

unnamed (11)
unnamed (11)
Asasi kuu za Tanzania sasa zimeanza kushuku vifaa ambavyo Kenya inatumia kuwapima madereva wake. Mkuu wa kata ya Longido Frank Mwaishumbe Alhamisi aliwataka madereva wa Tanzania kufanyiwa vipimo katika taifa lao ambapo watatumia stakabadhi hizo kuingia nchini.

“And if that cannot be possible, the owners of goods being transported to Kenya should come for them at the border as our drivers will have no other option but to leave them in Namanga,” alisema Mwaishumbe akiwa kwa mazungumzo na kituo cha Azam baada ya kuzuru mpaka wa Namanga.

Uongozi wa Tanzania umeshtumu matokea yaliyotangazwa na Rashid Aman Jumanne baada ya kudhihirika kuwa madereva wa tanzania 23 walirudishwa makwao baada ya kupatikana na virusi hivyo.

Aman alisema katika visa vilivyokuwa vimeripotiwa katika kaunti ya Kajiado vyote vilitokana na madereva wanaoingia nchini.

Aliongeza kuwa Kenya inawafanyia madereva vipimo haswa kutoka Tanzania kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.

Taarifa hizi zinajiri huku taifa la Uganda likisajili visa vipya 43 baada ya kuwafanyia madereva vipimo.

Visa hivyo vimetokea katika mataifa yafuatayo.

17 kutoka Uganda, 14 Kenya 5 Tanzania, 4 Eritrea, 2 Burundi na mmoja bado taifa lake halijabainika.

Kwa sasa, Uganda iko na visa  203 baada ya hivi vipya vilivyotokana na madereva.