TANZIA: Kijana wa darasa la nne ajitia kitanzi Busia

Mvulana mwenye umri wa miaka 11 amejitia kitanzi katika kijiji cha Masiebi eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia.

Marehemu Raymond Baraza ambaye ni mwanafuzi wa darasa la nne katika shule ya kibinafsi ya St Judes Rakite amepatikana ndani ya nyumba yao akiwa amejitia kitanzi kwa kutumia kamba kutokana na sababu ambazo hazijulikani.

Hayo yakijiri, watu wawili walikamatwa na pembe mbili za Kifaru katika mtaa wa Eastleigh hapo jana.

Paul Jinaro kutoka KWS anasema wawili hao, mwanamme na mwanamke walikuwa wakichunguzwa kwa muda wa miezi mitatu iliyopita. Washukiwa pia walipatikana na karatasi zinazotumika kutengeneza pesa bandia.