Aliyekuwa mbunge wa Nyaribari Masaba Hezron Manduku ameaga dunia katika Nairobi Hospital alikokuwa amelzwa . Mbunge huyo wa zamani amefariki akiwa na umri wa miaka 79 amethibitisha mwanawe Dr Robert Manduku.Dr Manduku amekuwa akiugua ugonjwa usioweza kutibiwa kwa muda mrefu . Viongozi kadhaa wametuma risalam za rambi rambi akiwemo mbunge wa sasa wa Nyaribari Masaba Ezekiel Machogu .
Mbunge wa Nyaribari Chache Richard Tong’i amemtaja marehemu Manduku kama kiongozi aliyekuwa na maono na aliyejizatiti kuboresha hali ya maisha ya wananchi . Marehemu Dr Manduku alichaguliwa kwa mara ya kwanza bungeni mwaka wa 1992 kwa tiketi ya chama cha KANU lakini baadaye akapoteza kiti hicho kwa seneta wa Kisii Sam Ongeri mwaka wa 1997. Baadaye alikihama chama cha KANU na kujiunga na Ford People alipokishinda kiti hicho mwaka wa 2002.
Dr Manduku na Prof Ongeri walihudumu kama wabunge wa Nyaribari Masaba kwa zaidi ya miongo miwili huku kila mmoja akikiri kwamba ni mwingine tu angeyeweza kumshinda mwenzake kutoka uongozi . Baadaye pia alihudumu kama waziri msaidizi wa Mashauri ya kigeni kati ya mwaka wa 1993 na 1997 .