Tanzia : MCA wa Lakeview Karanja Mburu afariki katika ajali ya barabarani

MCA
MCA
Bunge la kaunti ya  Nakuru limepata  pigo baada ya kuaga dunia kwa mmojawapo ya waakilishi wake wa kaunti   kupitia ajali ya barabarani  kwenye barabara kuu ya Nairobi Kwenda  Nakuru.

Mwakilishi wa wadi ya  Lake View  Karanja Mburu  alifariki baada ya gari lake kupoteza mwelekeo na kugonga mti  katika eneo la View Point kilomita kumi kutoka mji wa Gilgil jumapili asubuhi .

Mwakilishi huyo wa kaunti alikuwa mshirika wa karibu wa Naibu wa rais William Ruto  na seneta  Susan Kihika  alikuwa pekee yake  akielekea Nakuru kutoka Naivasha  wakati ajali hiyo ilipotokea.

Saa kadhaa  baada ya ajali hiyo   Gavana wa Nakuru  Lee Kinyanjui  ,spika wa kaunti Joel Maina  na waakilishi kadhaa wa kaunti walifika  katika  katika eneo la mkasa ili kumuomboleza   Mburu .

Akithibitisha ajali hiyo OCPD  wa  Gilgil Emmanuel  Opuru  ,amesema mti huo uliogongwa ulifunika sehemu ya mbele ya  gari hilo na  kuwazuia  madereva wengine kuuona .