Tanzia! Mtu na mkewe wazikwa kwenye maporomoko yanayoshuhudia Wbuye

EWmMSh7XgAALiwX
EWmMSh7XgAALiwX
NA NICKSON TOSI

Tanzia imeghubika familia moja katika eneo la Webuye baada ya jamaa mmoja na mkewe kuzikwa na maporomoko baada ya nyumba yao kuanguka kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini.

Katika taarifa hizo hizo ni kuwa waathiriwa wengine wa mafuriko Nhyando wamepokea misaada hii leo .

Wamepata vifaa vya kujenga upya kama vile blanketi na vifaa vingine baada ya nyumba zao kuanguka.

Kwa sasa familia hizo zimepiga kambi katika shule ya upilki ya Ombaka.

Kwengine ni kuwa Zaidi ya nyumba mia moja katika eneo la Nguluni Matungulu zimefurika na maji baada ya mvua kubwa kunyesha eneo hilo .

Wakaazi wa eneo hilo sasa wanahofia maisha yao baada ya mvua kusababisha nyumba kufurika na wanahofia kuzuka kwa magonjwa kutokana na maji taka .

Kwa sasa Wakazi hao sasa hawana maji safi ya kunywa visima vikifurika