TANZIA: Rais mstaafu Moi aaga dunia

Daniel Arap Moi
Daniel Arap Moi
Rais mstaafu Daniel  Arap Moi ameaga dunia .Rais Uhuru kenyatta  ametoa taarifa akitangaza kifo cha Mzee Moi ambaye ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 95. Mwezi uliopita madaktari katika hospitali ya Nairobi walilazimika kumrejesha Moi katika mashine za kumpa usaidizi wa kupumua .Hali yake ya afya imekuwa maaya tangu oktoba mwaka jana  alipolazwa hospitalini .

 Wakati huo alipolazwa hospitalini ,msemaji wake Lee Njiru  alisema Moi alikuwa amekwenda hospitali kwa ukaguzi wa kawaida  lakini tangia hapo alilazwa hospitalini mara nne.  Kundi lake la madaktari likiongozwa na Daktari  David Silverstein  limekuwa likimpa mkatibabu kwa matatizo yanayojirejeeza na kumfanya kusalia kitandani kwa miezi mitatu .

Hali ya afya ya Mzee Moi ilizidishwa kuwa mbaya na  jeraha la goti alilopata wakati wa ajali iliyohusisha gari lake mwaka wa 2006 huko Limuru .