Tanzia! rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aaga dunia

Aliyekuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa ameaga dunia.

Akitangaza kifo chake Mkapa, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alisema kwamba marehemu mkapa alifariki usiku wa Alhamisi katika Hospitali kuu ya Kitaifa ya Muhimbili mjini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.

Mkapa aliyezalia mwaka 1938 alihudumu kama rais wa tatu wa Tanzania kati ya mwaka 1995 - 2005 baada ya kustaafu kwa Ali Hassan Mwinyi.

Itakumbukwa kwamba marehemu Mkapa alitekeleza wajibu muhimu sana katika kuleta utulivu nchini Kenya baada ya ghasia  za uchaguzi mwaka 2007 -2008.