Tanzia: Watu 5 wameaga dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani

Watu watano wamepoteza maisha yao mapema hii leo baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Machakos kuelekea Kitui. Ajali hiyo ilihusisha matatu na Lori katika mtaa wa Kig'aatuani.

Mashahidi walioshuhudia ajali hiyo walisema kuwa matatu hiyo iligonga Lori kutoka nyuma na kusababisha ajali hiyo.

Waliopatwa na majeraha walipelekwa katika hospitali kwa matibabu huku timu ya uokoaji ikienda kwenye tukio la ajali. Kutoka kwetu wanajambo Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi.

Hizi hapa baadhi a picha za ajali hiyo;