Tanzia:Askari Kipyegon Kenei aliuwawa familia yake yasema

Ni habari ambazo ziliwashtua wananchi kuhusiana na kifo cha Kenei askari ambaye alikuwa anafanya kazi katika afisi ya naibu rais,Familia ya Kenei imesema kuwa mwana wao aliuwawa na bali hakujiuwa.

Kenei alipatikana alhamisi katika nyumba eneo la Imara Daima akiwa ameaga dunia na kupigwa risasi kichwani mwake.

Ndugu yake Emmanuel Kenei akizungumza alisema kuwa alikuwa na Kipyegon Ijumaa iliyopita na hakuwa na tatizo lolote aliongeza na kusema kuwa walijua habari za kifo cha ndugu yake wakiwa nyumbani mwao Rongai.

"Ijumaa iliyopita Kenei alikuwa humu nyumbani akaenda kumchukua mtoto wake anayesomea shule ya upili ya Baringo na kisha akampeleka mkewe hospitali

Tulijadiliana mambo kadhaa na hakuonyesha dalili zozote kuwa alikuwa na tatizo lolote." Emmanuel Alizungumza.

Aliongeza na kusema kuwa madai ambayo yanasemekana alijipiga risasi  haina msingi wowote, na hakuonyesha dalili kuwa alikuwa na tatizo.

Aliongeza na kusema kama kuna mtu yeyote ambaye alihusika katika kifo chake wanauliza serikali waanzishe uchunguzi wao  ili haki ipatikane.

Kenei,33, alikuwa aende akalipe mahari kwa mkewe Agosti mwaka huu.

"Mara ya mwisho kuja hapa tulienda kumtembelea mzee Chesang kwa maana alikuwa anataka kuanzisha mipango ya kulipa mahari yake

Mkewe alizaa hivi majuzi ndio maana hangefanya mapema huu mwaka." Alisema Emmanuel.

Chesang alisema kuwa amevunjika moyo kwa ajili ya kifo cha mwanawe na ameitisha msaada kote nchini ili mauaji hayo yachunguzwe kwa kina.

"Msizimie wala kulala kwa ajili ya uchunguzi wa mauaji ya Kenei, leo ni mimi kesho ni mwingine." Aliongea Chesang.

Inasemekana Kenei alikuwa katika doria wakati saini za biashara ya vifaa vya jeshi zilikuwa zinasainiwa, Kenei aliaga kabla ya kuandikisha taarifa kuhusu sakata hiyo ya jeshi.

Hadi sasa uchunguzi haujabaini kilicho sababisha kifo cha askari Kenei.