Taveta: Idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao yaongezeka

taveta
taveta
Idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao katika kaunti ya Taita Taveta imetajwa kuongezeka huku matumizi ya mihadarati yakilaumiwa pakubwa.

Kulingana na chifu wa Voi Abel Mwangemi, kuna haja ya hamasisho zaidi kufanywa ili kunusuru wanaume ambao wameingia katika ulevi na matumizi ya mihadarati.

Kwa sasa Mwangemi amependekeza kuundwa kwa vikundi ili kukabiliana na dhulma mbalimbali zikiwemo kupigwa na wake zao na kusema kwamba wataungana kuhakikisha serikali inasikia kilio chao.

Hayo yakijiri, wakazi wa kaunti ya Taita Taveta wameapa kujiunga na maandamano makubwa ya wafanyikazi wa idara ya afya kaunti hiyo yanayotarajiwa kuandaliwa hii leo ili kuishinikiza serikali kumalizamgomo wa wiki moja ambao umelemaza huduma za matibabu kaunti hiyo.

Wakiongozwa na mwanaharakati Waki Jarongo, wamemshtumu gavana Granton Samboja kwa kuvumbia macho mgomo huo na kumtaka kukubaliana na wafanyikazi ili huduma za kawaida kurejea hospitalini.

Wafanyikazi hao wanalalamikia kucheleweshwa kwa mishahara pamoja marupurupu.