Tazama jinsi mashabiki wa Gor Mahia walivyotawala mazishi ya Lady Maureen (PICHA)

Mashabiki wa klabu ya Gor Mahia na raia wengi walihudhuria na kutawala katika mazishi ya aliyekuwa malkia wa nyimbo za Ohangla, Lady Maureen.

Msanii huyo mashuhuri aliishi maisha ya kipekee na mashabiki wa Gor Mahia waligeuza mazishi yake kuwa mkusanyiko wa umati mkuu, huku polisi wakishindwa kudhibiti waombolezaji hao.

Kutoka Jumamosi asubuhi, mashabiki waliovalia sare za Gor Mahia walikusanyika katika chumba cha kuhifadhi mauti cha hospitali ya Ojele Memorial kuuchukua mwili wa msanii huyo kabla ya kuelekea katika eneo la mazishi, katika kijiji cha Kopanga katika mpaka wa Tanzania na Kenya.

Huku wakipuliza vuvuzela, pikipiki na magari zikipiga honi, mashabiki hao ndio waliotawala mazishi hayo.

Mashabiki pia walipata fursa ya kutangamana na kupiga picha na wasanii mashuhuri wa jamii ya Luo waliohudhuria wakiwemo; Connie Kabary, Dola Kabary, Musa Jakadala, Emma Jalamo, Prince Inda, Odosh Jasuba na wengineo.

 Tazama picha zifuatazo.