IMG_20190305_103242_6

Tazama mitaa Sonko wa Redio Jambo atafungia zoezi la kugawa hela nchini

Zoezi la kuwatunuku hela mashabiki wa kituo hiki linatazamiwa kufika tamati Agosti 30 msimu huu. Ikumbukwe kuwa mchakato huu wa kuwapa zawadi mashabiki zawadi hufanyika kila mwaka. Sonko wa Redio hii atakuwa anafunga ziara za kuzunguka miji mbalimbali baada ya kuzuru viunga vya jiji la Nairobi wiki ijayo.

Pata uhondo:

Unachotakiwa kufanya ili ushinde elfu 5 na elfu 1 kutoka Redio Jambo

Kituo hiki kinatazamiwa kuwatembelea mashabiki katikati mwa jiji la Nairobi jumatatu wiki ijayo. Sonko atafagia kabisa University Way, Odeon, Ambassador, Railways, Ngong, Kiserian na baadaye Rongai.

Siku ya pili sonko atavamia Industrial Area, South B na South C. Siku ya tatu sonko atachana kabisa mitaa ya Thika, Juja, Githurai, Kasarani, Mwiki, Babadogo na baadaye Dandora.

Sonko atapumzika baada ya kutinga ziara za mwezi mzima Embakasi, Syokimau,Mlolongo , Kitengela na Kajiado.

Sonko wa Redio Jambo azuru miji ya Kibwezi,Voi na Taveta

Maswali atakayokwenda kuuliza mashabiki sonko huyu ni rahisi sana. Sonko anahitaji kujua iwapo wasikilizaji wanaelewa kabisa maneno machache yanayolipa pesa “The Phrase That Pays”. Iwapo shabiki ataweza kung’amua Redio Jambo Ongea Usikike, sonko huwatuza shilingi 1,000. Aidha, mashabiki wanaozidisha ubunifu na kuyaandika maneno hayo katika bango hutunukiwa shilingi 5,000 pesa taslimu.

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments