TBT : Pata kumjua mtangazaji Jacob 'Ghost' Mulee Zaidi

story za ghost
story za ghost

Alhamisi huwa ni siku ya kurejelea vituko au matukio yaliyotendeka zamani na kuyaleta katika taswira ya leo.

Hufahamika kama TBT nawatu wengi hupenda sana kuzitafuta picha zao za zamani na kuzituma katika mitandao ya kijamii ili marafiki waweze kuona hatua walizozipiga kimaisha.

Hii leo tunaangazia mtangazaji nguli na mahiri katika utangazaji kwenye kituo maarufu hapa nchini anayefahamika kama Ghost Mulee. Huyu sio mwingine ila ni mtangazaji wako ambaye anapenda sana kucheka kicheko kikubwa katika shoo ya Gidi na Ghost Asubuhi.

Katika kitengo cha Patanisho, yeye na mwenzake Gidi huwaleta pamoja wapenzi waliokosana katika ndoa na kutatua kwa kiukamilifu mizozo katika familia.

Kipindi hiki kinachopendwa na wengi huwa kinapeperushwa kila asubuhi kuanzia jumatatu hadi ijumaa kupitia masafa ya redio Jambo iliyo chini ya mwavuli wa Radio Africa media Group katika ofisi zao kuu zilizopo Lions Place, Westlands barabara kuu ya Waiyaki .

Ghost Mulee,53, anayetambulikana kirasmi kama Jacob Mulee, alizaliwa mwaka wa 1968.

Kocha huyu wa kitambo wa soka ni mtangazaji mcheshi na huwa anavutia mashabiki kwa kicheko chake cha aiskrimu.

Gidi ambaye ni mtangazaji mwenza katika kipindi hiki ulazimika mara kwa mara kumsihi aache kucheka la sivyo atamzimia kipaza sauti.

Aliwahi kuwa kocha wa klabu cha Tusker kati ya mwaka wa 1999 na 2009 na akaweza kutawazwa hadhi kuu ya Kenya Premier League mara tatu. Mulee aliwahi kuwa kocha wa kilabu APR ya Rwanda na Young Africans Tanzania.

Katika kombe la kimataifa hapa Africa, mtangazaji huyu alikuwa mhusika mkuu mwaka wa 2004. Mulee aliacha kazi yake ya ukocha mwezi Disemba 2010 baada ya kushindwa kutwaa ushindi kwa timu ya kitaifa katika kombe la CECAFA.