tekno

Tekno matatani! kwa kucheza na wanawake wakiwa uchi hadharani

Mwanamziki wa Nigeria, Tekno, mwenye umri wa miaka 26 amekamatwa na maafisa wa polisi kwa kosa la kukata densi na wanawake waliokuwa nusu uchi ndani ya lori la maonyesho katikati mwa mji wa Lagos.

tekno
Lori hilo lilikuwa na kioo upande wa nyuma na kuwezesha watu waliokuwa nje kuona waliokuwa ndani walipokuwa wanasubiri kwenye trafiki. Polisi wamethibitihsha kukamatwa kwa nyota huyo ambaye jina lake halisi ni Augustine Kelechi siku ya Jumanne, “kwa kutembeza wasichana waliokuwa uchi” katika eneo la Lekki mjini Lagos.

Habari zaidi:Masaibu bado yamzonga Waititu

Msemaji wa polisi mjini Lagos pia alisema kwamba wanawake hao wawili pia wamekamatwa.
Mwanamziki huyo ambaye alishiriki katika albamu ya hivi punde ya Beyonce, aliacha wengi vinywa wazi wiki iliopita kwa kushiriki katika tangazo la kunadi eneo burudani la wanawake kunengua viuno wakiwa uchi wa mnyama – strip club.

Kenya, Jamaica zajitolea kuthibiti zaidi uhusiano wa kibiashara

Wananchi waliokuwa wamekwama kwa trafiki walishangaa kuona watu wakinengua maungo ndani ya kioo cha lori hilo huku baadhi ya nyeti zao zikiwa wazi. Kwenye video iliyosambaa mitandaoni, Tekno alionekana akiwamwagia manoti warembo hao.

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments