Temple ya warasta? Mbusii na Lion wabadilika kuwa wahubiri

mbusii.na.lion
mbusii.na.lion
Wiki iliyopita watangazaji maarufu, Mbusii na Lion Deh, waliwashangaza wengi walipoamua kunja jamvi la utangazaji na kuamua kujaribu taaluma ya uhubiri.

Wakali hawa wawili wa kipindi cha Mbusii na Lion teketeke ambacho hupeperushwa kila jioni kuanzia mida ya saa tisa hadi saa moja. Katika kipindi kile, wawili hao hugeuza studio za Radio Jambo na kuwa temple ya warasta.

Kama ilivyo sheria na kanuni, katika hekalu hii, Mbusii ndio pastor na Lion ndio Sheikh.

Hivyo basi, wawili hao walihudhuria kanisa ambalo kwa miaka kadhaa linajulikana kama kanisa ndogo sana la kikatoliki humu nchini. Kanisa hilo ambalo lilijengwa na waitaliano mwaka wa 1942, liko Mai Mahiu katika barabara ya Naivasha.

Watangazaji hao wawili walikuwa wame andamana na Dj Uche adi rasta, na waliamua kueneza neno, ingawa hakukuwa na waumini wengine mle ndani.

Wakiwa hapo mbele, Lion alimwelekeza mwenzake Mbusii kusoma maandiko katika kitabu cha zaburi 24 kisha wakafanya ombi lao maarufu kabla ya kuondoka na kuendelea katika shughuli zao za utalii katika maeneo ya View Point.

Shughuli hizi zote walizichapisha katika mtandao wao wa Facebook kwani walitaka mashabiki wao wajue waliko na wanacho fanya.